TARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KATIBU MKUU DK. WILLIBROD SLAA ZIARANI BARANI ULAYA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, Dk.
Willibrod Slaa ameondoka nchini Jumamosi Juni 06, 2015 kuelekea Bara la
Ulaya ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nane.
Akiwa ziarani Dk Slaa anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na
viongozi mbali mbali wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) ambapo pia
atakutana na jopo la wataalamu wa masula ya uchumi kwa lengo la
kubadilishana uzoefu katika kupata mifumo sahihi na kujenga taasisi za
kusaidia uwajibikaji na- kusukuma maendeleo ya watu katika nchi za
Afrika hususan zile zenye rasilimali nyingi kama Tanzania ili kuziepusha
na kile ambacho kimezikumba nchi nyingi duniani yaani 'laana ya
raslimali' (resource curse).
Aidha, akiwa na viongozi wa nchi za Ulaya, Dk Slaa atajadiliana nao
kuhusu hali ya Demokrasia, utawala bora na hali ya haki za binadamu
nchini hasa kwa kipindi hiki ambapo Watanzania wanaelekea kwenye
uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Katika ziara hiyo, viongozi hao wa Ulaya watapata fursa ya kujadiliana na Dk. Slaa hali ya siasa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dk. Slaa ameambatana na Mkurugenzi wa
Bunge na Halmashauri, John Mrema na Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano, Tumaini Makene.
Itakumbukwa kuwa Katibu Mkuu Dk. Slaa amekwenda ziarani barani Ulaya
akiwa ametoka kufanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa
ya Kagera, Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga
kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kwa mfumo wa BVR huku pia
akiwahamasisha Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura kuhakikisha
wamejiandikisha. Alitumia pia ziara hiyo kukagua maandalizi ya chama
katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na vyama washirika wenza
katika UKAWA kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Dk. Slaa atarejea nchini tarehe 15.06.2015.
-------------------
Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa CHADEMA
Post a Comment