Matukio ya wizi wa Magari yameongezeka nchini kwa siku za karibuni ambapo  kumechangiwa na vitu mbalimbali kama kukosa ajira , aina za maisha ya watu , soko la vipuri au hata aina Fulani ya magari yenyewe kutokana na mahitaji ya soko .

 Matukio haya yamesababisha watu kuumizwa , kuuwawa na kupata madhara mengine , watu hawa wangepata elimu ndogo tu wangeweza kujiokoa wenyewe na wengine kwenye vyombo hivi vya usafiri .

 Lengo la somo hili ni kutoa maelezo ya kile unachotakiwa kufanya endapo umekutwa na tukio hili , popote pale , ukifanya hivyo unaweza kutoka salama mikononi mwa wateka nyara , majambazi au wahalifu wengine .

 Kitu cha kwanza ni vizuri uweke kifaa cha kufuatilia gari lako na uwashe ili liweze kuonekana popote linapoenda pamoja na kuweka kamera za kurekodi matukio nje na ndani ya gari .

 Endapo utatekwa kifaa hichi kitakuwa msaada mkubwa kwa polisi na wenginekujua haswa kilichotokea na muelekeo wa gari au hata wewe ulipo au ulipokuwa mara ya mwisho .

 Kama umekutana na wateka nyara ( wezi wa magari ) ghafla tafadhali usipatwe na hasira , usitishike wala kumtisha mtekaji wala kujaribu kupambana nae kama ana silaha au wako wengi na kama uko mwenyewe kwenye mazingira mabaya ndio kaa kimya kabisa .

 Fanya kile unachoambiwa na wateka nyara kwa lugha nyingine ni tekeleza kila unachoambiwa bila kuhoji wala kujiuliza mara mbili na bila kuchelewa haraka haraka kwa maana wezi wengi wanapenda kufanya shuguli yao haraka wawahi kuondoka na wasijulikane na wewe au wengine .

 Usisite wala kukataa chochote haswa jambazi akiwa na silaha . mpe gari yako na uliache ukae pembeni . jaribu kuweka umbali kati yako na mtekaji ( jambazi ) kadri unavyoweza ila usijaribu kukimbia kwa wakati huo .

 Kama unavitu kwenye gari au karibu yako usijaribu kuvichukua au kuangalia . acha kila kitu kwenye gari au chombo chako cha usafiri kama mko wengi washauri na wenzako kufanya hivyo haraka .

 Uwe mtulivu saa zote na usionyeshe hali yoyote ya ugomvi , ubishi au kukataa waachie kile kitu wawe huru nacho kile wanachotaka kufanya .

 Hakikisha unasikiliza vizuri kila kinachosemwa na jambazi au majambazi na ufuate maelezo yao vizuri kadri unavyoweza ili wasibadilike au kukudhuru .

 Usimwangalie mteka nyara au jambazi usoni . anaweza kuchukulia kitendo hicho kama kitisho kwake kama unataka kumjua au kumtambua kwahiyo anaweza kukudhuru .

 Mikono yako na mguu au sehemu nyingine za mwili zionekane kwa jambazi ili asidhani unajaribu kujificha au kuchika au kufanya lolote dhidi yake kutumia mikono au viungo vya mwili wako .

 Usiongee haraka haraka ( kama unaweza kuongea ) na usijiguse wala kutembea au kujaribu vingine kutumia viungo vyako , kaa hivyo hivyo au lala kama umeambiwa ulale chini au kifudi fudi au kuangalia ukuta .

 Kusanya taarifa nyingi kadri unavyoweza kuhusu majambazi ( wateka nyara hao ) bila kuleta shida wala kitisho kwa majambazi hao kimya kimya .

 Taarifa au vitu unavyoweza kuangalia toka kwa majambazi ni kama ifuatavyo . Wako wangapi kwenye kundi

 Wana silaha ngapi na aina ya silaha

 Majambazi walikuwa wamevaa nguo gani ( rangi zake )

 Wameendesha gari au chombo chako kuelekea njia au eneo gani baada ya kukuibia ?

 Chunguza lugha na lafudhi wanazotumia .

 Inategemea uko kwenye hali gani na eneo ambalo upo lakini kama unapata mawasiliano toa taarifa polisi mapema kadri unavyoweza na uwape taarifa zote za ukweli ulizo nazo .

 Kwa Tanzania namba za polisi ni
 
PIGA (toll free number) 0800110019 (Bure)
 Au 0800110020 (Bure)

 Au POLISI-TRAFFIC 0682887722 -Ina Whatsapp& Telegram(Malipo) au 0800-757575 (Bure)

 Wakati mwingine polisi wanaweza kupata gari yako na kukurudishia lakini wakataka ushirikiano mwingine toka kwako tafadhali toa ushirikiano kadri unavyoweza .

MLINZI WA KWANZA WA AMANI NI WEWE .
 YONA FARES MARO
 0786 806028


Add caption
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.