Kikosi kimoja maalum cha serikali nchini Sudan kimeshutumiwa kwa kutekeleza maujai ya halaiki na ubakaji wa raia katika eneo la Darfur Magharibi tangu mwezi Februari mwaka uliopita.
Rais wa Sudan Omar Al Bashir
Ripoti mpya ya Shirika la kutetea haki za Kibinadamu Human Rights Watch inasema kikosi hicho kijulikanacho kama Rapid Support Forces kilitekeleza kile inachosema ni unyama na ukatili katika vijiji tofauti kwenye eneo hilo.

Walioshuhudia mashambulio hayo wameelezea jinsi vikosi hivyo maalum vya serikali viliwakusanya raia katika vijiji, vikaanza kuwapiga na kuwabaka wanawake wengi. Mmoja wa waathiriwa alisema alishuhudia wanawake kumi na saba wakibakwa katika hospitali moja.

Mwingine alisema aliwaona wanawake na wasichana wakibakwa na kasha kuingiza katika nyumba moja iliyochomwa bado wakiwa ndani.

" Dada zangu watatu walikamatwa, nyanya yangu pia alipigwa vibaya.… Waliwabaka dada zangu. Kisha wakawachukua mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka kwenye nyumba nyingine, na kuwachoma wakiwa hai. Nilisikia kilio chao. " alisema Hassan (sio jina lake la kweli), mwalimu wa umri wa miaka 26 anayefunza katika shule moja iliyoko katika kijiji cha Daya, katikati ya Golo naRockero. amesema
Waliojaribu kuzuia mashambulio hayo waliuuwawa. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu elfu mia moja thelathini wamefurushwa makwao kuanzia Januari mwaka huu. Wengi wao sasa wanaishi misituni.
Baadhi ya waliobakwa pia bado hawajapokea matibabu yoyote.

Human Rights Watch wakati huohuo pia imeshutumu vikali viksoi vya pamoja vya Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa ambavyo vinahudumu katika eneo hilo kwa kutowajibika ipasavyo kuwalinda raia. Ripoti hiyo aidha imependekeza serikali ya Sudan kuondoa vikosi hivyo katika eneo hilo mara moja na kuchunguza madai hayo.

Ripoti hiyo yenye kurasa 88 inasema matukio hayo yalitekelezwa katika eneo kubwa na kwa ukatili mkubwa. Zaidi ya mashahidi mia mbili waliohojiwa, wengine wakiwa katika mataifa ya Chad na Sudan Kusini ambako wamekimbilia hifadhi. "RSF imeuwa, kubaka na kuwatesa raia wengi katika vijiji, katika mashambulio ambayo yalipangwa awali, " alisema mkurugenzi wa HRW barani Africa Daniel Bekele,
" Serikali ya Sudan ni lazima iwapokonye silaha mara moja vikosi hivi na kuwafungulia mashtaka makamanda wote waliohusika." aliongeza

Mapigano yalizuka katika eneo la Darfur, Magharibi mwa Sudan Mwaka wa 2003, baada ya waasi waliojihami kuanza kupinga kutengwa na serikali ya Omar al Bashir. Kiongozi huyo anasakwa na Mahakama ya Kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC kwa madai ya kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za kibindamu katika eneo hilo.

Source: BBC/swahili

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.