Majengo pacha yenye ghorofa 35 ya PSPF Towers yaliyopo mtaa wa Sokoine jijini Dar es Salaam yemezinduliwa Septemba 16, 2015 na Rais Jakaya Kikwete.
Imeelezwa kuwa PSPF Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa meta 147.
Ujenzi wa jengo hilo ulichukua miaka minne (2011 hadi 2015) na limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Kitanzania. Lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88, sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na kadhalika.
Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa meta za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi barani Afrika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu alipowasili kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015
Mrisho Mpoto na Mjomba Band wakitumbuiza kwenye sherehe za majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr. Ramadhani Dau alipowasili kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015
Majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es Salaam yaliyozindulia leo Septemba 16, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete hutubia kabla ya kuzindua rasmi majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015
Rais Kikwete na msanii Mrisho Mpoto baada ya kuzindua majengo pacha ya PSPF
Rais Kikwete akikagua sehemu ya majengo hayo
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi na wakuu wa mifuko ya pensheni
Rais Kikwete akiwa na Bodi ya PSPF
Makandarasi wazalendo waliojenga majengo pacha ya PSPF Towers
Watumishi wa PSPF
Rais Kikwete akifunua pazia kuzindua rasmi majengo pacha ya PSPF TOWERS
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi majengo pacha ya PSPF TOWERS
Rais Kikwete akipokea zawadi ya picha ya PSPF Towers na Bw. George Yambesi
Source by www.wavuti.com
Post a Comment