Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS)
umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za
udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili
waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni
2016. 
 
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni  tarehe 5 Agosti 2016 saa sita
usiku.

Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha maombi yao
kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016, wanaarifiwa kuanza
kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili
kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia muda huu wa
nyongeza ili kuwasilisha maombi.

Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa
vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo
wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha ya majina  ya wenye sifa za
udahili kulingana na nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo
husika kati ya tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. Majina ya waombaji
waliochaguliwa kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni
kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji waliochaguliwa nao
wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwa kubofya hapa.
Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya
wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.

Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE,
Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano kati ya NACTE na Tume ya Vyuo
Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa
waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.

Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 22 Julai, 2016
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.