Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na Uvumi katika Mitandao ya Kijamii kuwa Serikali imeamua kushusha Mishahara ya Madaktari kwa asilimia 30% ili kuendana na dhana ya Hapa kazi tu na kuwa Serikali   imekusudia kufuta malipo ya Posho za Wataalamu wa Afya walio katika Mafunzo kwa Vitendo ufafanuzi kwa Umma wa Watanzania na Watumishi wa Sekta ya Afya kuwa taarifa hizo siyo za kweli.

Taarifa aliyoitoa Katibu Mkuu (Afya) alipokuwa anaongea na Watumishi wa  Hospitali ya Bugando  ililenga kutoa ufafanuzi kwa Watumishi wa Hospitali hiyo kuhusu kufutwa kwa kibali cha Msajili wa Hazina kilichowawezesha  watumishi wa Hospitali hiyo kulipwa Mishahara ya Taasisi zilizo chini ya Msajili wa Hazina tangu mwaka 2012.

Uamuzi huo wa Msajili wa Hazina unatokana na ukweli kwamba Hospitali ya Bugando siyo Shirika la Umma na hivyo wanastahili kulipwa mishahara sawa na watumishi wengine wa Serikali Kuu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo kati ya Serikali na Baraza  la Maaskofu Tanzania  (TEC) ambao ndio wamiliki wa Hospitali ya Bugando.

Aidha, ieleweke kuwa mishahara ya Watumishi wa Sekta ya Afya haizingatii ngazi ya Vituo vya kutolea huduma kama vile Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali, au Hospitali za Rufaa bali huzingatia uzito wa kazi na majukumu ya kada husika. Hivyo, mshahara wa Daktari wa Hospitali ya Wilaya ni sawa na ule wa Hospitali ya Rufaa ngazi ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda.

Kutokana na maelezo haya, uamuzi huo wa Msajili wa Hazina utaihusu Hospitali ya Bugando pekee na siyo Hospitali zote za Kanda kwa kuwa dosari hiyo haikutokea katika Hospitali nyingine za Kanda.
Kuhusu ajira mpya kwa mwaka 2015/2016 ufafanuzi ulitolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba hakutakuwa na ajira mpya hadi hapo Zoezi la Uhakiki wa Watumishi Serikalini litakapokamilika.  Hivyo, vibali vya ajira vilivyokuwa vimetolewa vimefutwa hadi hapo itakapotamkwa vinginevyo.

Kadhalika, kumekuwa na Uvumi kuwa Serikali inakusudia kufuta posho ya ‘Interns' kuanzia mwaka huu wa fedha.  Taarifa hii pia siyo sahihi kwa kuwa hakuna chombo chochote cha Serikali ambacho kimetoa maamuzi hayo.

Wizara inasisitiza kuwa maamuzi ya Serikali hutolewa na Mamlaka husika  kwa nyaraka. Hivyo, watumishi wa Sekta ya Afya na wananchi kwa ujumla wanaaswa kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka za Serikali kuhusu Masuala yanayowahusu ambayo mara nyingi hutolewa kwa nyaraka badala ya Mitandao ya kijamii,

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Afya
14 Julai, 2016
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.