Wafanyabiashara wa mboga mboga, samaki wa kuzindika na bidhaa zingine za kilimo wameombwa kutumia fursa ya kuuza bidhaa zao nje ya nchi kufuatia kuzinduliwa kwa Bohari ya kwanza ya kisasa katika bara la Africa iliyogharimu shilingi bilioni 26 za kitanzania.
Waziri wa Kilimo,  Mifugo na Uvuvi, Dtk Charles Tizeba, akikata utepe, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jengo la Kimataifa na Kisasa la Upokeaji wa Mizigo kutoka nje, lilojengwa na Kampuni ya Swissport Tanzania. Aliyesimama katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Swissport, Bw. Mark Skinner. (Picha na Mpiga Picha Wetu)..

“Matarajio ya ukuaji wa huduma za usafirishaji wa bidhaa za kilimo, chakula na mifugo kupitia bohari hii ya kisasa Zaidi nchini na ni dhamira ya serikali kuhakikisha wafanyabishara katika sekta ya kilimo wananufaika kupitia mradi huu kabambe,” amesema Waziri wa Kilimo, uvuvi na Ushirika, Dkt Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa bohari hiyo ya jana  kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

Sekta ya usafiri wa anga ni nyeti, ambayo uwepo na ukuaji wake unategemea huduma zinazoaminika—kama vile pamoja na mambo mengine utunzaji na usimamizi wa mizigo, bohari, utunzaji na usimamizi wa barua, utunzaji wa nyaraka zinazohusu mizigo iliyopakiwa au kupakuliwa.

Dkt Tizeba aliongeza pia kwamba wizara yake itaanza kuhamamisha wakulima na wafugaji kuanza kutengeneza na kuandaa nyama kuweka katika ubora wa uhakika ili kuweza kuuza nje ya nchi na kuuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Kwa sasa machinjio yetu ya Ruvu wanaweza kuchinjwa takribani ng’ombe 4,000 kwa siku ila tupo katika mpango kabambe kuhakikisha idadi inaongezeka ili waweze kutumia fursa ya bohari hii ya kisasa kutafuta masoko nje ya nchi,” amesema Dkt Tizeba 

Amesema kwamba serikali itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa ndani ili waweze kutumia uwanja huu wa ndege wa Mwl nyerere ili kuuuza mtandao wa kuuza bidhaa zao za kilimo, mboga mboga na maua nje ya nchi.

Alisisitiza kwamba ni muhimu wa Serikali kuendelea kushirikiana na taasisi, sekta binafsi katika sekta ya anga ili kuleta tija na kutumia sekta hii kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi wan chi nzima.

“wafanyabiashara wa maua na bidhaa zingine za kilimo wanapaswa kuendelea kutumia fursa hii adhimu katika kupambana na umaskini na kupunguza tatizo la ajira nchini.

Bw Temu alisema kwamba uzinduzi rasmi wa jengo hilo jipya la kuhudumia mizigo inayoingia na kutoka nchini ni la kisasa barani Afrika na litaongeza ufanisi wa huduma katika sekta ya usafirishaji nchini.

Alisema kwamba kampuni hiyo Swissport ni ya kimataifa ambayo inatoa huduma zake kwa takribani nchini 58 duniani kwa kiwango cha ubora wa kimataifa ya kusafirisha, kuhifadhi na kupokea mizigo ya aina zote na bidhaa mbalimbali.

Bw Temu aliongeza kwamba kitengo cha bohari ya kupakia mizigo kimetengenezwa kwa teknolojia ya juu kabisa katika kuhakikisha ufanisi na uharakishaji wa upakiaji mizigo ambapo kinaweza kupakia tani 30 kwa siku.

Kwa kutambua umuhimu wa huduma Kampuni ya Swissport inayotoa, Bw Temu alisema: “Tumeamua kuboresha huduma zetu za kupakia na kupakua mizigo…kwa kweli, hizi ni nguzo muhimu kwa ukuaji endelevu wa hii sekta nchini Tanzania.”
 
Bw. Gaudence Temu (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania, akifafanua jambo kwa Waziri wa Kilimo,  Mifugo na Uvuvi, Dtk Charles Tizeba, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jengo la Kimataifa na Kisasa la Upokeaji wa Mizigo kutoka nje, lilojengwa na Kampuni ya Swissport Tanzania. (Picha na Mpiga Picha Wetu)

Akielezea uboreshaji ambao umefanyika, Bw Temu alisema kwa sasa chumba maalum cha baridi cha Swissport kimepanuliwa kwa kuongeza huduma mpya kama vile mfumo wa ukaguzi wa mizigo ndani ya chumba chenye mitambo maalum. 
Alisema “chumba hiki maalum kimegawanywa katika maeneo mawili: eneo moja lina ukubwa wa mita 200 za mraba na lingine ni mita 100 za mraba.”

 Akifafanua zaidi, ofisa mkuu huyo wa Swissport alisema kampuni yao imefunga mizani ya futi 20 katika eneo lao kwa kutoa huduma kulingana na mahitaji ya shirika la ndege husika.

Kwa upande wa kuhifadhi mizigo, kampuni ya Swissport imejenga bohari ya kisasa na salama na inayoweza kufiwa kwa urahisi. Imefungwa mitambo maalum ya CCTV na ya ukaguzi wa magari. Pamoja na mambo mengine, bohari hii ina vifaa maalum kwa ajili ya ukaguzi, uangalizi na utunzaji salama wa mizigo.

Uboreshaji uliofanywa hivi karibuni umefanywa kwa lengo la kuisaidia serikali katika jitihada zake za kuboresha huduma za usafiri wa ndege, ambao ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi za ustawi wa mamilioni ya Watanzania, kwa mujibu wa Meneja Mikataba na Masoko-Swissport, Bw James Mhagama.
Mwisho
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.