Wanafunzi 6000 wa Shule za Msingi Dar
wanufaika na elimu ya usalama barabarani
.Mradi
ulioanzishwa na Total Energies Marketing Tanzania
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MRADI
wa “VIA Creative” unaolenga kuwapatia elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi
wa Shule za Msingi umewafikia takribani wanafunzi 6000 kwenye Shule za
Makuburi, Ubungo, NHC, Buza, Jangwani, Ugindoni na Uzuri katika jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom akizungumza na wageni
waalikwa , wanafunzi kwenye hafla ya kukabidhi tuzo na vyeti kwa wanafunzi na
shule iliyofanya vizuri kwenye shindano wa mradi wa “VIA Creative” wa kutoa
elimua ya usalama barabarani hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni .
Mgeni
rasmi kwenye hafla hiyo ya kukabidhi tuzo wa wanafunzi waliofanya vizuri na
shule iliyofanyika jijini Dar es Salaam
hivi karibuni, Mkuu
wa Idara ya Mafunzo ya Trafiki Kinondoni, A.S.P Rose Bernard Maira aliwapongeza
Total Energies Marketing Tanzania Limited, TotalEnergies Foundation Pamoja na
Nafasi Art Space kwa juhudi zao za kutoa elimu ya usalama barabarani zinastahili
kupongezwa na kuigwa na makampuni mengine ili kuchochea usalama wa watoto
waendapo na watokapo mashuleni.
“Jeshi
la Polisi kikosi cha usalama barabarani tupo Pamoja nanyi kwenye jambo hili na
katika kutoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kuzijua sheria, kanuni na
taratibu za barabarani kwa wanafunzi na watumia Barabara wote.
“Aidha,
tumefurahia kujua kwamba mradi huu pia unalengo la kutimiza mapendekezo ya
kuboresha hali ya usalama kwa wanafunzi wa shule iliyoshinda kama trulivyopata
kuona kwenye filamu ya wanafunzi hao. Pia niwatakie kila la heri washindi hawa
kwenye hatua nyingine ya shindano ambalo wanatarajia kuingia, nawasihi
muiwakilishe Tanzania vizuri na mungae Pamoja na kushinda ngazi za shindano la
VIA Creative zijazo.” Aliongeza.
Mmoja ya wanafunzi wa Makuburi akipokea tuzo yake kutoka kwa Mgeni
rasmi , ASP , Rose Bernard Maira
Alisema
kwamba usalama barabarani ni suala muhimu katika jamii yetu,kila mwaka
tunashuhudia ajali nyingi za barabarani ambazo zinaweza kuzuiliwa kwa njia
rahisi ya kueneza elimu sahihi ya sheria, alama na utumiaji salama wa barabara.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou
Ngom alisema kwamba shindano hilo ambao lilikuwa kwa njia ya sanaa ya
michoro, muziki, maigizo na mashairi kuna ongeza uelewa wa wanafunzi kwenye
mambo ya usalama barabarani na kupunguza ajali.
“Tunayo
furaha kubwa kuwa hapa leo tukisherehekea mafanikio ya mabalozi wetu wa usalama
barabarani kupitia mradi wa VIA Creative amabo tumeshirikiana na Nafasi Art
Space ambao wamekuwa wakiwapatia wanafunzi hawa elimu ya usalama barabarani kwa
kupitia sanaa,”
“Kupitia
mradi huu tumeweza kuunda klabu za mabalozi barabarani 120, 20 kutoka kwenye
kila shule. Pia wanafunzi hawa wameweza kutoa mapendekezo yao ya jinsi ambavyo
usalama wao wa barabara unaweza kuboreshwa nasi tutatekeleza mapendekezo hayo
kwa shule ya msingi ya Makuburi ambao ndio washindi wa kitaifa wa shindano hili
kwa mwaka 2024.” Alisema Bw Ngom
Aliongeza
kwamba usalama barabarani ni suala muhimu katika jamii yetu,kila mwaka
tunashuhudia ajali nyingi za barabarani ambazo zinaweza kuzuiliwa kwa njia
rahisi ya kueneza elimu sahihi ya sheria, alama na utumiaji salama wa barabara.
Alisema
kwamba ni jukumu letu sote kuhakikisha
tunafuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo
athari zake kiuchumi na kijamii ni kubwa sana.
“Ningependa
kuchukua fursa hii kuwapongeze wanafunzi
wote 120 walioshiriki kwenye mradi huu na kushindanishwa kwenye shindano la VIA
Creative, nyinyi nyote ni washindi na mabalozi bora wa usalama barabarani.
Tunawaomba muendele kuwafundisha wenzenu, wadogo zenu, na hata wazazi wenu juu
ya utumiaji salama wa Barabara Pamoja na sheria na kanuni zake,” alisisitiza.
Bw Ngom
aliongea kwamba Total Energies wapo pamoja na Jeshi la Polisi kikosi cha usalama
barabarani kwenye jambo hilo na katika
kutoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kuzijua sheria, kanuni na taratibu
za barabarani kwa wanafunzi na watumia Barabara wote.
Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Trafiki Kinondoni, A.S.P Rose Bernard Maira
akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya kugawa tuzo kwa wanafunzi na
shule za jijini Dar es Salaam kwenye mradi wa “VIA Creative” unaolenga kutoa
elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es
Salaam.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space ambaye ni mdau wa
mradi huo, Felix Muchira alisema kwamba waliona ni muhimu kutoa elimu ya
usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa njia rahisi ya maigizo
na uchoraji ili waweze kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi.
“ajali
hapa nchini limeanza kuwa jambo la kawaida na ni jukumu letu sote kuendelea
kutoa elimu kwa kushirikiana na serikali na hasa Jeshi la Polisi Kikosi cha
Usalama barabarani kutoa elimu ya michoro, alama na sheria za usalama
barabarani kwa Watoto wetu,” alisema Bw Muchira.
Mgeni rasmi wa shughuli hiyo, ASP Rose Bernard Maira akigawa cheti/ tuzo
kwa mwalimu wa Shule ya msingi Makuburi iliyoibuka kidedea kwenye shindano la
mradi huo
Shindano
hilo la kimataifa la "VIA CREATIVE" ni shindano linalolenga wanafunzi
wa shule za msingi wa miaka 4 -19 kwa lengo la kuwapatia elimu ya usalama
barabarani kwa njia ya sanaa ya michoro, muziki, maigizo na mashairi na kisha
kuwapa fursa wanafunzi hao kuelezea uleewa wao na mapendekezo yao ya usalama
barabarani kwa njia ya michoro na maigizo.
Mwaka
huo wa VIA Creative umewafikia wanafunzi
6000 kutoka shule za msingi Makuburi, Ubungo NHC, Buza, Jangwani, Ugindoni na
Uzuri zilizopo jijini Dar es salaam na kuendeleza uundaji wa klabu za mabalozi
wa usalama barabarani.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Msingi
Makuburi akipita baada ya kupokea cheti chake mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Total
Energies, Bw Mamadou Ngom
VIA
Creative ni mradi ulioanza mwaka 2022 ambao tangu mwaka huo zaidi ya wanafunzi
22,000 wamefikiwa na mradi huu na kuweza kujenga klabu za mabalozi wa usalama
barabarani kwenye shule 100 jijini Dar es Salaam na Bagamoyo.
Hafla
ya kukabidhi tunzo kwa wanafunzi walioshinda kwenye msimu huu wa tatu wa VIA
Creative zilifanyika kwenye ofisi za TotalEnegies Marketing Tanzania Limited
jijini Dar es Salaam ambapo shule ya msingi ya Makuburi Primary school iliibuka
mshindi wa kitaifa wa shindano lwa shindano hili na muwakilishi wa Tanzania
kwenye ngazi ya kimataifa munamo mwezi Novemba 2024.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Msingi
Makuburi akipita baada ya kupokea cheti chake mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Total
Energies, Bw Mamadou Ngom.
Baadhi ya wafanyakazi wa Total energies wakifuatilia tukio hilo kwenye
hafla hiyo
Mwisho