Sauti za Busara yaanza kwa Busara Xtra
Tamasha la muziki la Sauti za
Busara linatarajiwa kuanza tarehe 14 ya mwezi wa pili na kuufanya mji
mkongwe wa Zanzibar kung’ara kwa mara nyingine tena.
Ni siku ya kwanza ya ‘Busara
Xtra’, siku ambayo Mji Mkongwe utasheheni maonesho ya biashara
mbalimbali za sanaa na burudani, ngoma, na madarasa ya kucheza muziki,
sambamba na muziki wa reggae ambao utatumbuiza huku ukipata mandhari
nzuri ya kuzama kwa jua. Siku hii yenye mvuto wa kipekee ya maonesho ya
sanaa itafanyika katika mgahawa wa Livingstone ambapo itaanza tarehe
14 Februari na kuendelea kwa siku zote za tamasha, sambamba na kuwepo
kwa vinywaji vya aina mbalimbali, ambapo shughuli zote hizi zitaanza
saa 4 asubuhi.
Itawawia vigumu kwa wahudhuriaji
kuchagua ni wapi pa kwenda, kwani kutakuwa na burudani kabambe katika
maeneo mbalimbali, wakati muziki wa Reggae utaanza saa 10 za jioni huko
Kae Funk Michamvi, Nadi Ikhwan Safaa kikundi maarafu cha muziki wa
Taarabu hapa Zanzibar kitafanya onesho lake NIS Club House, onesho
litakaloanza saa 10 za jioni. Bado kutakuwa na kazi ya ziada kuchagua
kwenda kwenye muziki wa Taarabu wa zamani wa asili au kwenda katika
onesho la Sinachuki Kidumbak Taarabu ya kisasa, ambapo burudani zote
hizi zitakuwa Mji Mkongwe, ndio maana Busara Xtra ipo kwa ajili yako.
Nae Mkurugenzi wa tamasha la
muziki la Sauti za Busara Yusuf Mahmoud amesema kwamba, tamasha mara
zote limekuwa likilenga katika kuwanufaisha wazanzibar, tokea tamasha
lianze mwaka 2004 idadi ya wageni wanaoitembelea Zanzibar mwezi wa pili
imeongezeka hadi kufikia asilimia tano, pamoja na kutoa mafunzo
mbalimbali na ajira kwa wazanzibar na kuongezeka kwa wageni kila mwaka,
kwa kiasi kikubwa Sauti za Busara imekuwa ikisaidia watu wa Zanzibar
na Tanzania kwa jumla. Kuwepo kwa Busara Xtra pia inachangia kukuza
uchumi na utamaduni wa kisiwa cha Zanzibar. “Busara Xtra inaongeza fursa
kwa wasanii wageni kuonesha kazi zao, wageni kutembelea maeneo
mbalimbali ya kisiwa cha Zanzibar, kukutana na wazanzibari na kuongeza
ushikiri katika tamasha kwa jamii ya wazanzibari wa kawaida.
Baada ya kujumuika na tamasha la
Busara Xtra, jukwaa kuu la Sauti za Busara litafunguliwa tarehe 15 ya
mwezi wa pili na kuendelea na burudani mpaka tarehe 17 mwezi wa pili
2013. Pia ratiba ya filamu ya Busara imepangwa kuonyesha filamu tatu
ambazo zitakamilisha jukwaa la muziki. Kwa upande wa amphitheatre hapo
Ngome Kongwe kutaoneshwa filamu za wasanii mbalimbali maarufu wa
muziki, pamoja na filamu ndefu. Kwa maelezo zaidi au kununua tiketi
mtandaoni, tafadhali tembelea wovuti ya www.busaramusic.org
au nunua tiketi mlangoni kuanzia tarehe 13 mwezi wa pili 2013. Tiketi
ni shilingi 3000 kwa watanzania na kiwango maalumu kwa wanaotoka Afrika
Mashariki.
Sauti za Busara inawashukuru
kipekee wadhamini wote ambao ni Goethe Institute, Grand Malt, Memories
of Zanzibar, Diamond Trust Bank, ChemiCotex, Azam Marine, Ultimate
Security, Zanzibar Unique Ltd., Southern Sun, Embassy of France,
Alliance Française, SMOLE II na wengine wote kwa kufanikisha tamasha la
mwaka huu.
Kwa maelezo zaidi na picha downloads: Tafadhali tembelea wovuti ya www.busaramusic.org
* Picha za Hi-resolution kwa waandishi wa habari zinnaweza kupatikana kwa maombi.
* Picha za Hi-resolution kwa waandishi wa habari zinnaweza kupatikana kwa maombi.
Tunaendelea na kuboresha na kuorodhesha orodha ya annuani zetu za barua pepe tulizonazo
this list is only to be used for providing information to press people
Jarida hili la barua pepe limetumwa kwa dmakangale1@yahoo.com.
Unauwezo wa kujiengua kutoka katika listi yetu la jarida hili, kwa kutembelea (URL) kisara hiki:
http://www.busaramusic.org/cgi-bin/dada/mail.cgi/u/habari/
Kama kisara (url) hiki hakibofyeki, chukua muda kunakili kisara hiki kizima kwani wasomaji wengine wa barua pepe hii wanaweza kuuvunja mstari huu kua mistari kadhaa
Unaweza kuwasiliana nasi kwa anuani pepe hii press@busara.or.tz Na kwa wale wanaoweza kutumbelea tupo, njia ya kuelekea uwanja wa ndege tukiangaliana upande wa pili wa barabara na Gofu club Maisara
Busara Promotions, mkabala na Golf Club, Maisara, Njia ya uwanja wa ndege, Zanzibar, Tanzania
Post a Comment