Picture
Waziri Mkuu na jopo la Mawaziri kikaoni Mtwara leo Jumanne, Januari 29, 2013 (picha: Mtwara Kumekucha blog ya Baraka Mfunguo)

1·   Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini ndugu Wilman Kapenjama Ndile alitamka kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwatumia ujumbe Mawaziri wapatao 6 kuwaita ili kuungana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Emanuel Nchimbi hapo saa 3 asubuhi, ili kufanya kikao cha majumuisho ya “Yatokanayo” na mikutano ya wadau mbalimbali.

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi (Dkt. John P. Magufuli), Waziri wa Uchukuzi (Dkt. Harrison Mwakyembe), Waziri wa Viwanda na Biashara (Abdallah Kigoda), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, - (Dkt. Mary Nagu) na Waziri wa Elimu (Dkt. Shukuru Kawambwa).

2·    Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini ndugu Wilman Kapenjama Ndile alitamka kuwa Waandishi wa habari wamealikwa kwa ajili ya kikao cha muhstasari (briefing) wa “Yatokanayo”.

    Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu kwa Mkoa wa Mtwara, Sheikh Idrissa Lingondo amesema kilichosabababisha vurugu na yote ya uharibifu yaliyotokea katika kipindi hiki, ni kauli mbovu za kuudhi na kuvunja moyo kama vile kukataa kupokea maandamano ya watu na kuwaita wahaini na/au wapuuzi. Majibu kama hayo ndiyo yaliyoamsha hasira.

Akashauri kuwa watu wote (viongozi kwa wananchi) watumie diplomasia. Akatoa wito kwa Wananchi kuwa wasikivu na watulivu katika kipindi hiki ambacho mazungumzo na Viongozi wa juu wa Serikali yanaendelea.

4·  Askofu George Mussa wa Kanisa la TAG (Tanzania Assemblies of God), alisema ukimya wa viongozi na kutokukubali kuzungumza na wananchi na kuwajibu maswali yao, ndiyo uliochochea wananchi kushikwa na hasira iliyosababisha hasara. Akahoji ni kwa nini viongozi wanakuwa kimya kusubiri mpaka maafa yanapotokea ndipo wanajongea kuzungumz a na Wananchi?

Akasisitiza kuwa siyo kwa Mtwara tu, bali nchi nzima, kwamba wananchi wamekuwa wanapuuzwa na hawasikilizwi hoja zao hasa pale wanapotaka kuwasilisha masuala yanayowazunguka. Akaonya kuwa maandiko ya Biblia yanasema Waisraeli waliopacha kusikiliza kilio cha watu wao, Mungu aliruhusu uasi utendeke, ndipo Watawala walipoamka na kuwasikiliza.

Askofu Mussa akasema kuwa mtu yeyote ana haki, hata kama hajaenda shule, kwani hilo halimaanishi kuwa hajui kuhusu yanayomzunguka. Akasema iachwe dharau ya kudhani kuwa Watu wa Kusini hawajasoma au/wala kuelimika. 

Amehoji, ikiwa ahadi walizopewa wananchi –kujenga mitambo ya miradi, kutoa ajira n.k.– haijawekwa wazi, Je, Wananchi wataijuaje? Ni wazi kuwa watahoji.

Alipotakiwa kutoa maoni yake kwa ujumla, alionya dhidi ya matumizi ya nguvu kwa kusema kuwa mara nyingi nguvu za Watawala huzaa uasi wa Wananchi ili kukabiliana na nguvu hizo, akasema ndiyo mifano iliyotokea kwenye nchi ambazo zimejitahidi kutumia mabavu kuongoza wananchi.

Kuhusu nafasi yao kama viongozi kushirikishwa katika masuala ya kijamii, ameuliza, vioangozi wanasubiri mpaka machafuko yatokee ndipo maombe viongozi wa dini wawatulize wananchi?

Mwishowe akaomba na kuwasisitiza Wananchi wawe watulivu, wasikivu, Waitii mamlaka –kama agizo la Mungu katika Biblia linavyosema– na kutokuasi kwani ni laana kwa Taifa.



DONDOO MUHIMU KATIKA MAJUMUISHO kutoka kwa Baraka Mfunguo wa Mtwara Kumekucha blog

- Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Simbakalia kawaomba radhi wananchi wa Mtwara.
  • - Waziri Nchimbi kutumia lugha kibabe na vitisho dhidi ya raia pamoja na taarifa isiyokuwa na tathmini halisi na yenye uwiano pale alipotolea mfano askari aliyevamiwa dukani/baa yake na kuibiwa pesa kiasi cha sh. 1,895,000/= na kupoteza mali ya sh. 200,000,000/= (milioni mia mbili) na kusababisha watu wagune.
  • - Kawambwa kawahimiza wazazi kuwaruhusu watoto kwenda shule kupata elimu sanjari na chuo cha VETA kutoa masomo ya mitaala ya gesi sanjari na uchomeleaji baharini.
  • - Tibaijuka amezungumzia kuhusu upanuzi wa mji wa Mtwara na kuleata kauli mbiu ya "Amani na Maendeleo" kutoka kwao Kagera.
  • - Mwakyembe amezungumzia  upanuzi wa bandari kavu na ujenzi wa reli Mtwara, Liganga, Mchuchuma hadi  Mbamba Bay na kuahidi kuja Mtwara kila baada ya miezi 3 na kujadili na kutathmini changamoto.
  • - Waziri Mkuu ametoa udhuru wa Waziri wa ujenzi Dk Magufuli ambaye alitakiwa kuwepo lakini hakuweza kuhudhuria.
  • - Bi Mapunjo kaahidi mipango mikubwa ya ujenzi wa viwanda mkoani Mtwara.
  • - Mbilinyi kaainisha idadi ya makampuni yaliyoonyesha nia ya kuja kuwekeza Mtwara (sina hakika sana kama ni Mtwara).
  • - Waziri Mkuu katoa majumuisho ya ziara yake ambayo hayana tofauti na haya yaliyojadiliwa.

TAARIFA KWA KINA kutoka kusini blog: PINDA AZIMA MZOZO WA GESI MTWARA

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi wa mkoa wa Mtwara kwa kuwaeleza kuwa kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajenngwa kijiji cha Madimba, mkoani hamo ili mabaki yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda, tofauti na madai ya wakazi hao kuwa kiwanda hicho kitajengwa jijini Dare s Salaam.

Akizungumza katika mkutano wa majumuisho uliofanyika jana (leo), VETA mjini Mtwara baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirisha kwa njia ya bomba.
Wataalam wanasema gesi haiwezi kwa namna yeyote ile kusafirishwa kama ilivyo, lazima ibadilishwe kuwa hewa au barafu…kiwanda cha kusafisha gesi kitajengwa Madimba, gesi yote itakayotoka Mnazi Bay itasafishwa hapo na masalia yote yatabaki huku ili kuvutia viwanda vya mbolea na vingine vinavyotumia malighafi hizo...

Kama tungekuwa tunasafirisha gesi ghafi basi hata kiwanda cha Dangote kisingejengwa hapa…gesi itakayopelekwa Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme…tusaidieni wenzetu kuliokoa Taifa na tatizo la umeme.
Awali, madai ya wakazi wa mkoa wa Mtwara yalikuwa kupinga usafirishaji wa gesi ghafi kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa mpango huo utafukuza uwekezaji wa viwanda mkoani humo, ambao ungechochewa na upatikanaji wa malighafi baada ya kusafishwa kwa gesi.

Pia, wananchi walipinga ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme Kinyerezi jijini Dar es Salaam wakiitaka serikali kujenga mitambo hiyo mkoani Mtwara.
Gesi lazima isindikwe Mtwara, haitoki hadi viwanda vije…nadhani hili ni jambo jema lazima tuliwekee utaratibu …nikawauliza wataalam wangu kwani kiwanda cha kusafisha gesi kinajengwa wapi, wakanijibu Madimda…nikasema kumbe tatizo kubwa ni kutowaeleza wananchi suala la gesi vya kutosha” alisema Waziri Mkuu huku akipigiwa makofi

Nafikiri tatizo ni sisi serikali hatukuwa na mpango mzuri wa kuwaelimisha wananchi.
Aidha, aliwataka wananchi kumsamehe Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakali kwa kauli alizozitoa Desemba 21, 2012 katika kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) pale alipoombwa kuyapokea maandamano ya wakazi wa mkoa huo Desemba 27, mwaka uo huo ambapo aliwaita wapuuzi wananchi hao na baadaye wahaini.
Binadamu kukosea lazima, lakini kubwa zaidi ni kuomba msamaha…amefanya hivyo, sasa tusahau yaliyopita tugange yajayo.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu ilitanguliwa na kauli ya Mkuu huyo wa Mmkoa kuwaomba radhi wakazi wa mkoa wa Mtwara na kwamba alipotoka kutoa kauli hiyo ambayo iliwaudhi wengi. Simbakalia alisema:
Kupitia hadhara hii nawaomba radhi kwa kuwa kwaza, nimesikitishwa kwa kauli yangu imepokelewa kwa hisia kwamba niwadharau.
Waziri Mkuu katika majumuisho yake aliambatana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Emanuel Nchimbi.

Ametoa wito kwa wabunge wa mkoa wa Mtwara kufuta tofauti zao za kisiasa ili waweze kuharakisha maendeleo ya mkoa huo. Waziri Mkuu, Pinda, huku akishangiliwa alisema:
Purukushani hizi ndani ya chama hazina tija, tuseme basi…wabunge hawaelewani, sasda bungeni wanakwendaje... kila mtu na lake …hebu tuseme watu kwanza mimi badaye.
Pinda katika siku zake hizo mbili mkoani Mtwara alikutana na vyama vya siasa vya upinzani, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Viongozi wa dini ya Kiislam na Kikiristo, Wafanyabishara, Madiwani na Wenyeviti wa Mitaa pamoja na Wanaharakati  kutoka AZAKI mbalimbali.

Akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama, Dkt. Nchimbi alisema hali kwa sasa ni shwari na kwamba Wizara yake imejidhatiti kwa nguvu watu na vifaa ili kukabilina na vurugu zozote, huku akikwepa kuzungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya askari wanaodaiwa kuwauwa wananchi wilayani Masasi.

Dkt. Nchimbi alisema katika tukio la Masasi, watu 4 walifariki dunia, kinyume na taarifa ya muuguzi wa zamu hospitali ya Mkomaindo Amina Tumbi aliyoitoa kwa waandishi wa habari siku ya tukio ambapo alisema amepokea miili ya watu 7 kabla ya siku ya pili kuripotiwa kwa kifo cha aliyekuwa majeruhi hospitali ya Ndanda.
Hali ni swari, tumejipanga vya kutosha kwa watu na vifaa…Hii ni tabia mbaya haikubaliki …unapamba na pilisi…itafika wakati watoto wetu watakataa kujinga na polisi…tutapambana kikamilifu misiniharibie kazi mimi nina miaka 41.
Kwa upande wake, Dkt. Kawambwa alisema Wizara yake imeamua kuifanya VETA Mtwara kuwa kituo cha umahiri ili wahitimu wake waweze kuajiriwa katika sekta ya gesi.

Naye Profesa Tibaijuka alisema wizara yake imekamilisha mipango miji kwa mji wa Mtwara ili uweze kuendana na mabadiliko ya kiuchumi na kwamba wananchi wa mkoa huo wawe tayari kuendana na hali hiyo.

Dkt. Mwakyembe yeye alisema bandari ya Mtwara haijauzwa na kwamba inapanuliwa ili iweze kukidhi mahitaji ya baadaye, huku akiahidi kutembela Mtwara kila baada ya miezi 3 ili kutoa taarifa ya maendeleo ya bandari na uwanja wa ndege kwa wananchi.
Tulikuwa na eneo la hekta 70 tu za bandari ya Mtwara, sasa tumepanua na tunayo hekta 2994 , tumetenga hekta 110 ili tuweze kuwa na bandari huru itakayowezesha kuongezeka kwa matumizi ya bandari yetu.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vyama tisa vya siasa mkoani Mtwara, Uledi Abdallah amesema madai ya wananchi yalikuwa mitambo ya kusafisha gesi ghafi ijengwe Mtwara na kwamba iwapo serikali imeamua kufanya hivyo madai yao yatakuwa yamekwisha.
Kama gesi itayosafirishwa kwenda Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa, sisi hatuna tatizo.
Naye Mbunge wa Mtwara Mjini, Asnain Murji alimpongeza Waziri Mkuu kwa hatua yake ya kuwasikiliza wananchi na kwamba mzozo huo uliodumu kwa takribani mwezi mmoja sasa umefikia tamati.

Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mtwara Mjini, Saidi Kulaga alimpongeza Waziri Mkuu kwa hatua aliyoichukua na kumuomba awaachie huru wale waliokamatwa kutokana na vurugu zilizotokea Mtwara na Masasi ili kujengwa mwanzo mpya wa mahusiano mazuri baina ya serikali na wananchi, ombi ambalo Waziri Mkuu alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi ndani ya wiki mbili.









Source:wavuti





























































































































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.