Madereva wa Bajaji washauriwa kutii sheria za usalama Barabarani
MADEREVA wa bajaji mkoani
Singida,wameshauriwa
kujenga utamaduni wa kutii bila shurti sheria za usalama barabarani,ili pamoja
na mambo mengine,kuondoa uwezekano wa kutokea kwa ajali zinazosababisha vifo na
uharibifu mkubwa wa mali.
Aidha, wametakiwa kutii bila shurti kanuni na taratibu
zilizowekwa na SUMARTA,ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa migomo na kufunga
barabara.
Usafiri wa Bajaji |
Wito huo umetolewa juzi na meja Stan wa kitengo cha usalama
barabarani mkoani Singida,wakati akizungumza na madereva wa bajaji wa kituo cha
soko kuu mjini hapa ambao walifunga barabara ya mtaa wa Mukhandi kutumika.
Meja Stan aliwataka kuheshimu maamuzi ya SUMATRA kwa kuwapa
vituo vya kupakia abiria,ili kuepuka kutokea kwa migongano baina yao na bodaboda
na hata hiece.
“Kama wewe SUMATRA imekupangia kituo chako kuwa ni cha stand
ya mabasi cha zamani,sheri,ukipakia abiria anakuja hapa soko kuu,sheria
inakutaka ukimshusha tu,uondoke hapo mara moja kurudi kwenye kituo
chako”,alisema.
Meja Stan alisema abiria huyo akimaliza shughuli zake soko
kuu,atapanda bajaji au usafiri mwingine kwenda anakotaka.
Akifafanua zaidi,alisema kuwa sheria hairuhusu dereva wa
bajaji ambaye soko kuu sio kituo chake asubiri abiria pale,ili amalize shughuli
zake halafu ampeleke sehemu nyingine anakokwenda.Wajibu wake ni kumshusha na
yeye kurudi kwenye kituo chake.
Wakati huo huo,meja Stan amewataka wajenge utamaduni wa
kutumia viongozi wao kuwasiliana na uongozi wa halmashauri ya manispaa ya
Singida,ili kujadiliana pamoja kutatua kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi wa
kudumu,ikiwemo ya ufinyu wa maegesho.
MWISHO.