BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeeleza kwamba
hakuna hata senti moja kutoka kwenye akaunti ya wateja wao ambayo imepotea
baada ya kutokea tatizo la kiufundi katika mifumo ya kibenki kupitia mitandao
ya simu za mkononi (Mobile Banking System) hali hiyo ilijitokeza siku ya
Jumatano wiki hii.
Kaimuy mkuu wa Kitengo cha Biashara na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Bi Rukia Mtingwa akisisitiza jambo wakti wa utoaji wahabari hizo |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Kaimu Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki hiyo, Jimmy Myalize alisema
kuwa matatizo ya kiufundi ambayo yalitokea siku ya Jumatano ni baada ya
kugundua mifumo ya kibenki kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi kushidwa
kufanya kazi.
Alisema kutokana na tatizo wateja hawakuweza
kusoma amana zao au akiba zao kwenye simu zao za mknononi au ilikuwa inaonyesha
sifuri na ilisababisha usumbufu kwa wateja wote wa benki hiyo nchi nzima.
"Mafundi wetu na wataalamu wa mitandao
katika benki wanafanya kazi ili kuhakikisha kwamba wateja wa benki hiyo nchini kote wanaweza kupata taarifa
za amana zao na kuendelea kufanya shughuli zao za kifedha kupitia simu zao za
mkononi," Alisema.
Aliongeza kuwa NBC ni benki ya muda mrefu hapa
nchini tangu mwaka 1967 na wataendelea kutoa huduma nafuu na salama za kifedha nchini kote na
katika jitihada kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa Watanzania.
"Tatizo lilianza asubuhi na mafundi wetu walichukua
hatua ya haraka kwa kutambua na kutatua mara moja, walilazimika kukata huduma
za kibenki kwa njia ya simu ili kuruhusu mafundi wetu kufanya kazi kwa urahisi
ili kutatua kikamilifu tatizo hilo la kiufundi, alisema kaimu Mkuu wa Masoko na
Mahusiano , Rukia Mtingwa.
"Katika tatizo hilo wateja wangependa
kuthibitisha amana au akiba zao, wanaweza kufanya hivyo kwa kutembelea tawi
lolote la NBC au ATM.
"Tungependa kuomba radhi kwa usumbufu wowote
uliosababishwa na mafundi wetu wanaendelea kufanya kazi kwa karibu ili
kuhakikisha kwamba huduma ya kibenki kupitia simu za mkononi zinarudi haraka iwezekanavyo,"
aliongeza Rukia.
Kwa upande mwingine, Benki hiyo imekanusha madai
ya hivi karibuni kupitia Mitandao ya habari (social media) kwamba benki hiyo imekuwa
mwathirika wa wizi wa kupitia mashine zake za ATM na kuomba wateja kuondoa
fedha zao.
Benki hiyo ilisema kwamba taarifa hizo si za
kweli na inapenda kuwajulisha wateja wao na wananchi kwa ujumla kuwa habari
hizo si za kweli kwamba kuna wizi wa mitandao kupitia mashine zake za ATM
nchini.
Uongozi wa benki hiyo ilisema matatizo makubwa
ya wizi kupitia mashine za ATM kushughulikiwa kwa pamoja na Taasisi ya Benki
Tanzania (TBA).
Post a Comment