June 2015

Grants

IDRC Research Awards 2016

Call for: Applications
Deadline: August 06, 2015 by 16:00 (04:00 PM) (UTC-05:00) Eastern Time (US and Canada)
Eligibility: This call is open to Canadians, permanent residents of Canada, and citizens of developing countries pursuing a master’s or a doctoral degree at a recognized university OR who have completed a master's or doctoral degree at a recognized university. These research awards may be part of an academic requirement.
Other eligibility requirements include:
  • Your proposed research must focus on one or more developing countries.
  • Candidates cannot receive any other Canadian government scholarship, award, subsidy, bursary, or honorarium, or hold any federal government contract in support of a research/work project for the duration of the award.
  • If you are a non-Canadian residing, relocating, or studying in Canada and are recommended for an award, you will need a valid work permit before working at IDRC.
Duration: January to December 2016 (12 months). Based in Ottawa, Canada (Select placements may be located in one of IDRC's Regional Offices).
Budget: Salary for one year: CA$39,797-CA$46,070
Scope: For payroll purposes, awardees are considered as full-time employees of IDRC. Benefits include Employer contributions to Employment Insurance, Employer Health Tax, Canada Pension Plan, and paid vacation leave. Some travel and research expenses are also supported, up to a maximum of CA$15,000.

As a research award recipient, you will undertake a one-year paid program of research on the topic you submitted to the competition and receive hands-on experience in research management; grant administration; and the creation, dissemination, and use of knowledge from an international perspective.
Access the call document and frequently asked questions (FAQs):
All additional questions should be addressed to awards@idrc.ca

Sengerema. CCM imesema kuwa itahakikisha inarudi Ikulu hata “kwa bao la mkono” wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDTfcaTQ6aR606KE870X5j8HaJ_KqE6e8K4v92HRoIOkrj0pq-aHTqpMFLCsnKwLbzbNm_imwCn9p8ZV0t1ymixBXn0YyzRQeiIKVw2S96AoXXk8yHIXBiViHFRvrHpz1tfGHSenswcLs/s1600/WP_20150623_018.jpg
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Nyehunge wilayani hapa.

Neno “bao la mkono” hutumiwa kama goli lililofungwa kwa kuupiga mpira kwa mkono kinyume cha taratibu za mpira, lakini hukubaliwa kwa kuwa mwamuzi anakuwa hajaona kitendo hicho.

“Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao ni bao tu ili mradi refa hajaona,” alisema Nape.

Nape, aliye kwenye ziara ya katibu mkuu wa CCM, aliwataka wananchi wa Sengerema kusubiri ushindi wa chama hicho na kuwakumbusha kuwa wanapaswa kuiweka CCM kuanzia udiwani mpaka ubunge kwa nafasi ya urais tayari kuna uhakika.

Katika mkutano huo, Nape alisema ana uhakika CCM itashinda baada ya kushuhudia mwitikio wa Watanzania tangu alipoanza kuongozana na Kinana katika ziara zake za kuizunguka nchi na kuzungumza na wananchi pamoja na kusikiliza kero zao.

Amebainisha kuwa amejifunza na kujiridhisha kuwa chama chake bado kinapendwa miongoni mwa wapigakura waliofikiwa tofauti na vyama vya upinzani.

“Tumefika maeneo mengi ambayo upinzani haujafika. Huko tuna hazina kubwa ya wanachama. Hakuna namna Ukawa wanaweza kuingia Ikulu mwaka huu,” alisisitiza.

Wapinzani waja juu

Kauli hiyo ya Nape ilipingwa na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani waliosema kuwa mtendaji huyo anamaanisha kuwa CCM itaiba kura.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa hakutaka kabisa kuzungumzia kauli ya Nape zaidi ya kusema watakutana Oktoba.

“Kwa bahati mbaya kauli za Nape siwezi kuzijibu. Kauli za Nape zichukue kama zilivyo, ingekuwa ni (katibu mkuu wa CCM, Abdulraham) Kinana, ningemjibu lakini ajue kuwa tutakutana Oktoba,” alisema Dk Slaa alipoulizwa na Mwananchi kuhusu suala hilo.

Naibu mkurugenzi wa habari wa CUF, Abdul Kambaya alisema kauli ya Nape inamaanisha kuwa CCM itaiba kura kwani kwa kawaida bao la mkono ni bao haramu.

“Kauli hiyo inaonyesha dhahiri kuwa wataiba kura na kwa sababu katiba yetu ni mbovu matokeo yake yatatangazwa kama yalivyo… hiyo ndiyo maana ya bao la mkono,” alisema.

Kambaya alisema hata hivyo CCM isijiaminishe kwa lolote kwani hivi sasa wananchi wamebadilika kimtazamo kutokana na matatizo mengi yanayoiandama nchi kama vile afya, elimu duni na migogoro ya ardhi.

“Lakini CCM wajue kuwa kutatokea machafuko makubwa iwapo wamejipanga kuingia Ikulu kwa njia hiyo ya bao la mkono. Kauli ya Nape ni ya kidikteta na inaonyesha dhahiri kuwa wamejikita kwenye utawala wa mabavu,” alisema.

Kadhalika Kambaya alisema CUF imeshajipanga na kuhakikisha inaziba mianya yoyote ya wizi wa kura kuanzia kwenye Daftari la Wapigakura hadi katika ujanja wa kuwapigisha kura marehemu, askari na wanajeshi kama inavyodaiwa kufanyika Zanzibar.

Katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema Nape anatoa maneno ya kuvutia kwake kama njia ya kuwakatisha tamaa wapinzani na wanachama, hata hivyo alimuonya kuwa siasa za sasa hazitabiriki kwa njia hiyo.

“Lakini ajue kuwa mambo yanabadilika. Anaweza kushangaa mambo yakawa mengine, sasa hivi wananchi wana mwamko mkubwa na wanabadilika,” alisema.

Alisema CCM haina haja ya kujitapa kwa sasa wakati bado haijapata mgombea kwani huenda wakapata ambaye wananchi hawatamuunga mkono hata kidogo.

“Bado CCM wana makundi jambo ambalo kwao ni udhaifu. Lakini pia lazima wajue kuwa wakati wa mchujo utakapofika, wale watakaokatwa hawatafurahia kuachwa na hapo kuna sababu za wapinzani kushinda,”alisema.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema wakati Nape anabishana kwenye majukwaa, NCCR inaendelea kupiga kazi.

“Badala ya kujadili hoja za msingi zenye manufaa kwa wananchi yeye anajadili CCM kupiga bao?” alihoji Mbatia.

Akijibu hoja ya Nape, Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mrikaria alisema kauli ya kada huyo imekaa kisiasa na si kiuhalisia kwani ni kawaida kwa chama cha siasa kujiaminisha kuwa kitashika dola.

“Unajua chama chochote hata kiwe kidogo lazima kikiri kuwa kitashika dola ili mradi ilani yao inakubalika na unakubaliwa na wananchi kwa sababu chama chochote nia yake ni kuingia ikulu,” alisema.

Alisema hata vyama vidogo kama TLP hukiri ushindi kwa kusema kuwa vinataka kuingia ikulu kwa sababu chama hakiwezi kukiri mbele ya wananchi kuwa hakitashinda.

Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu wa India Mheshimiwa Narendra Modi, na Rais Wa IndiaMheshimiwa Pranad Mukherjee wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Rais kikwete kuwasili katika Ikulu ya India kwa mapokezi rasmi, Ijumaa 19, 2015. (picha: Freddy Maro).





Rais Jakaya Kikwete atalihutubia Bunge la 10 mjini Dodoma kati ya Julai 9 au 10 kulingana na ratiba yake.

Bunge hili litakuwa la mwisho kwa Awamu ya Nne ya uongozi wake kabla ya kuvunjwa rasmi katika tarehe itakayopangwa.

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa ya Bunge, Jossey Mwakasyuka alisema hayo mjini hapa jana alipozungumza na Mwananchi.

Mwakasyuka alisema sasa Bunge linaendelea na maandalizi ya ujio wa Rais Kikwete.

“Rais atalihutubia Bunge kulingana na ratiba yake, lakini sisi tumeanza maandalizi ya shughuli hiyo,” 
alisema Mwakasyuka.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Ibara ya 30 (i), Rais anaweza kuhutubia siku yoyote wakati Bunge linapokutana. Hata hivyo, alisema Rais hatavunja Bunge kwa sababu litavunjwa kwa Tangazo la Serikali (GN). 
“Imekuwa ni utamaduni Rais anapomaliza kipindi chake cha uongozi anakuja kulihutubia Bunge, pengine safari hii anakuja kueleza mambo yaliyofanywa na Serikali yake,”
alisema.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama alisema: 
“Suala hilo liko ofisi ya Spika na kamati yake ya uongozi ndiyo watakuwa na ratiba yote.”

Alipotafutwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila kuzungumzia zaidi suala hilo hakupatikana.

Pia kama ilivyokuwa kwa Bunge la tisa, wabunge watatunukiwa vyeti kutambua utumishi wao walioutumikia katika Bunge la 10.

Rais alilihutubia Bunge hilo la 10 kwa mara ya kwanza Novemba 18, 2010 ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuapishwa kushika madaraka hayo kwa kipindi cha pili.

















































Benki ya Tanzania (BOT) imewataadharisha wananchi kwamba sarafu ya shilingi 500 haina madini ya aina yoyote na wala haiuzwi kama inavyodaiwa baadhi ya watu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Zalia Mbeo wakati akitoa ufafanuzi kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu ambaye aliuliza kwamba kuna taarifa kuhusu sarafu hiyo kuuzwa mitaani.

Kaimu Katibu Mkuu huyo ambaye alifungua maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani.

“Watanzania wanatapeliwa sarafu hii haina thamani yoyote ni uzushi,” alisema Zalia.

Aliongeza kusema kuwa wananchi wadanganywa na watu kuwa sarafu hiyo ikiyeyushwa ina madini ambayo yanaweza kuwapatia fedha nyingi wakati si kweli.

TRA would like to recruit dynamic experienced and qualified personnel to fill vacant positions in the Research & Policy, Human Resources & Administration and Board Secretariat & Legal Services Departments. Applications are therefore invited from suitably qualified Tanzanians for the following positions:































Communications Officer - Dar es Salaam, Tanzania

Ref. 19930BR

The DFID-funded Education Quality Improvement Programme in Tanzania (EQUIP-Tanzania) aims to support 47 districts in their efforts to produce a better quality of primary education for more than two million children in over 3700 primary schools.

We currently need a Communications Officer to manager and deliver the day to day information and communication of EQUIP-Tanzania. Proactively identifying opportunities to support the programme outputs, revising the information and Communication strategy under the guidance of our International Communication Advisor.
You will be responsible for managing the information and knowledge produced across the programme, working closely with managers and technical advisers to understand the communication requirements and maintaining EQUIP-Tanzania’s website and social media presence. Additional duties will include the management and delivery of campaigns, messages and materials and the draft and design of printed documents and publications.
You will be educated to degree level or equivalent ideally marketing, social communication or public relations.  With experience gained within a programme environment you will be able to demonstrate an understanding of working within a sector development programme. You will have excellent communication and written skills and be proven in the ability to create compelling copy from technical information, draft news releases, content for leaflets and letters.

 Read the full job description and apply

KATIKA hali isiyo ya kawaida mkulima kutoka Kijiji cha Mjimtala Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Eldoforce Bilohe (43)leo alitinga makao makuu ya Chama cha Mapindizi (CCM) kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kuteuliwa kuwa mgombea bila kuwa na ada huku akiwa amebeba maji ya chupa kwapani.

Bilohe ambaye alisema elimu yake ni ya darasa la saba aliwasili makao makuu ya CCM muda wa saa 5:40 asubuhi na kuelekea Ofisi ya kupokelea wagombea ndani ya ofisi baada ya kuwapita waandishi wa habari wakiwemo wapiga picha waliokuwa wamejipanga kumsubiria lakini aliwapita waandishi bila kumtambua kuwa ni mgombea.

Akiwa amevaa suruali ya khaki na fulana yenye rangi ya kijani na njano alionekana kuduwaza watu wengi ambao walikuwa wakiwasuburi wagombea ambao walikuwa wakichukua fomu jana.

Akiwa kati ya watu waliokuwa kwenye orodha ya kuchukua fomu,  Bilohe alikuwa amebeba chupa ya maji kwapani baada ya kufika na kupokelewa na maafisa ambao walimtambua kuwa ni mgombea na ndipo wapiga picha waligutuka na kuanza kupiga picha.

Kisha aliingia ndani ya ofisi ya kuchukua fomu na alitoka baada ya muda mfupi na kuanza kuhojiwa na waandishi wa habari.

Alisema amefika Dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuteuliwa kuwa mgombea lakini kwa sababu ambazo hazijazuilika ameambiwa akachukue fedha.

“Nilipogiwa simu wakati niko benki ya CRDB nikiwa kwenye foleni nikisubiri kuchukua fedha ndiyo nikakimbia kuja hapa”
 alisema

Alisema amekuwa mwanachama hai wa CCM tangu mwaka 2003 na elimu yake ni ya m msingi na ana uzoefu kutokana na kuwa katika chama kwa muda mrefu.
“Nimekuja kama nilivyo kwa sababu sijawahi kuwa na makundi unayoyaona wewe, mimi ni mwanachama wa kawaida kama wanachama wengine” 
alisema

Alisema ameamua kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho kwa kuamini kama anaweza.

Kwa Mujibu wa mujibu wa moja wa maofisa wa Chama ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema Bilohe amerudisha si kwa sababu hana hela kuna vigezo ambavyo havijafikiwa ikiwemo barua ya utambulisho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya aliyotoka.
“Hajakamilisha taratibu za kumwezesha kuhukua fomu” 
alisema.

Hata hivyo taarifa zilizopatikana baadaye zilisema kuwa tayari mkulima huyo ameshalipa gharama za ada ya fomu kiasi cha Sh. 1,000,000 na atachukua fomu yake kesho saa kumi jioni.


Source by www.wavuti.com

TARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KATIBU MKUU DK. WILLIBROD SLAA ZIARANI BARANI ULAYA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini Jumamosi Juni 06, 2015 kuelekea Bara la Ulaya ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nane.

Akiwa ziarani Dk Slaa anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) ambapo pia atakutana na jopo la wataalamu wa masula ya uchumi kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika kupata mifumo sahihi na kujenga taasisi za kusaidia uwajibikaji na- kusukuma maendeleo ya watu katika nchi za Afrika hususan zile zenye rasilimali nyingi kama Tanzania ili kuziepusha na kile ambacho kimezikumba nchi nyingi duniani yaani 'laana ya raslimali' (resource curse).

Aidha, akiwa na viongozi wa nchi za Ulaya, Dk Slaa atajadiliana nao kuhusu hali ya Demokrasia, utawala bora na hali ya haki za binadamu nchini hasa kwa kipindi hiki ambapo Watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Katika ziara hiyo, viongozi hao wa Ulaya watapata fursa ya kujadiliana na Dk. Slaa hali ya siasa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dk. Slaa ameambatana na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene.

Itakumbukwa kuwa Katibu Mkuu Dk. Slaa amekwenda ziarani barani Ulaya akiwa ametoka kufanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Kagera, Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kwa mfumo wa BVR huku pia akiwahamasisha Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura kuhakikisha wamejiandikisha. Alitumia pia ziara hiyo kukagua maandalizi ya chama katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na vyama washirika wenza katika UKAWA kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Dk. Slaa atarejea nchini tarehe 15.06.2015.
-------------------
Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa CHADEMA

Photos of Nigeria's first lady wearing an expensive watch led some Nigerians to ask whether they undermine President Buhari's "man of the people" image. 
This photo of Nigeria's first lady wearing an expensive-looking watch outraged many on social media
This photo of Nigeria's first lady wearing an expensive-looking watch outraged many on social media

In March, Muhammadu Buhari was elected as Nigeria's new president after a campaign which took a strong anti-corruption stance. Buhari underlined his humble credentials by raising money from ordinary voters. He even had to stretch his finances to pay the fee to register as a candidate.

This image was diluted somewhat when his wife, Aisha Buhari, was pictured wearing an expensive-looking watch at her husband's inauguration last week and these images were shared on the Instagram account of the photographer George Okoro.

Nigerian press described it as a Cartier Baignoire Folle 18-carat white gold diamond timepiece that was estimated to cost around $50,000 - more than £30,000 or about 10m Nigerian naira. Others, however, pointed out that knockoff versions are available for as little as $100.

Source by  http://www.bbc.com



Matukio ya wizi wa Magari yameongezeka nchini kwa siku za karibuni ambapo  kumechangiwa na vitu mbalimbali kama kukosa ajira , aina za maisha ya watu , soko la vipuri au hata aina Fulani ya magari yenyewe kutokana na mahitaji ya soko .

 Matukio haya yamesababisha watu kuumizwa , kuuwawa na kupata madhara mengine , watu hawa wangepata elimu ndogo tu wangeweza kujiokoa wenyewe na wengine kwenye vyombo hivi vya usafiri .

 Lengo la somo hili ni kutoa maelezo ya kile unachotakiwa kufanya endapo umekutwa na tukio hili , popote pale , ukifanya hivyo unaweza kutoka salama mikononi mwa wateka nyara , majambazi au wahalifu wengine .

 Kitu cha kwanza ni vizuri uweke kifaa cha kufuatilia gari lako na uwashe ili liweze kuonekana popote linapoenda pamoja na kuweka kamera za kurekodi matukio nje na ndani ya gari .

 Endapo utatekwa kifaa hichi kitakuwa msaada mkubwa kwa polisi na wenginekujua haswa kilichotokea na muelekeo wa gari au hata wewe ulipo au ulipokuwa mara ya mwisho .

 Kama umekutana na wateka nyara ( wezi wa magari ) ghafla tafadhali usipatwe na hasira , usitishike wala kumtisha mtekaji wala kujaribu kupambana nae kama ana silaha au wako wengi na kama uko mwenyewe kwenye mazingira mabaya ndio kaa kimya kabisa .

 Fanya kile unachoambiwa na wateka nyara kwa lugha nyingine ni tekeleza kila unachoambiwa bila kuhoji wala kujiuliza mara mbili na bila kuchelewa haraka haraka kwa maana wezi wengi wanapenda kufanya shuguli yao haraka wawahi kuondoka na wasijulikane na wewe au wengine .

 Usisite wala kukataa chochote haswa jambazi akiwa na silaha . mpe gari yako na uliache ukae pembeni . jaribu kuweka umbali kati yako na mtekaji ( jambazi ) kadri unavyoweza ila usijaribu kukimbia kwa wakati huo .

 Kama unavitu kwenye gari au karibu yako usijaribu kuvichukua au kuangalia . acha kila kitu kwenye gari au chombo chako cha usafiri kama mko wengi washauri na wenzako kufanya hivyo haraka .

 Uwe mtulivu saa zote na usionyeshe hali yoyote ya ugomvi , ubishi au kukataa waachie kile kitu wawe huru nacho kile wanachotaka kufanya .

 Hakikisha unasikiliza vizuri kila kinachosemwa na jambazi au majambazi na ufuate maelezo yao vizuri kadri unavyoweza ili wasibadilike au kukudhuru .

 Usimwangalie mteka nyara au jambazi usoni . anaweza kuchukulia kitendo hicho kama kitisho kwake kama unataka kumjua au kumtambua kwahiyo anaweza kukudhuru .

 Mikono yako na mguu au sehemu nyingine za mwili zionekane kwa jambazi ili asidhani unajaribu kujificha au kuchika au kufanya lolote dhidi yake kutumia mikono au viungo vya mwili wako .

 Usiongee haraka haraka ( kama unaweza kuongea ) na usijiguse wala kutembea au kujaribu vingine kutumia viungo vyako , kaa hivyo hivyo au lala kama umeambiwa ulale chini au kifudi fudi au kuangalia ukuta .

 Kusanya taarifa nyingi kadri unavyoweza kuhusu majambazi ( wateka nyara hao ) bila kuleta shida wala kitisho kwa majambazi hao kimya kimya .

 Taarifa au vitu unavyoweza kuangalia toka kwa majambazi ni kama ifuatavyo . Wako wangapi kwenye kundi

 Wana silaha ngapi na aina ya silaha

 Majambazi walikuwa wamevaa nguo gani ( rangi zake )

 Wameendesha gari au chombo chako kuelekea njia au eneo gani baada ya kukuibia ?

 Chunguza lugha na lafudhi wanazotumia .

 Inategemea uko kwenye hali gani na eneo ambalo upo lakini kama unapata mawasiliano toa taarifa polisi mapema kadri unavyoweza na uwape taarifa zote za ukweli ulizo nazo .

 Kwa Tanzania namba za polisi ni
 
PIGA (toll free number) 0800110019 (Bure)
 Au 0800110020 (Bure)

 Au POLISI-TRAFFIC 0682887722 -Ina Whatsapp& Telegram(Malipo) au 0800-757575 (Bure)

 Wakati mwingine polisi wanaweza kupata gari yako na kukurudishia lakini wakataka ushirikiano mwingine toka kwako tafadhali toa ushirikiano kadri unavyoweza .

MLINZI WA KWANZA WA AMANI NI WEWE .
 YONA FARES MARO
 0786 806028


Add caption

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.