Na Damas Makangale,
Bank of
Africa Tanzania imekuwa mshirika wa Accelerate Women Summit 2025,
mkutano uliolenga kuchochea kasi ya maendeleo ya wanawake, na imesisitiza
dhamira yake ya kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini kwa kuwajumuisha
rasmi katika mfumo wa kifedha. Benki inaamini kuwa wanawake wakiwezeshwa
kibiashara wataweza kuwa wabunifu, kuibua ajira, na kuimarisha ustahimilivu wa
uchumi wa nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Esther Maruma, amesema wanaamini kuwa mafanikio ya wanawake yanachangia maendeleo ya jamii na uchumi kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of
Africa Tanzania, Esther Maruma (kushoto), akizungumza katika Mkutano wa
Kuchochea Kasi ya Maendeleo ya Wanawake (Accelerate Women Summit 2025)
uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa
Trademark Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Monica Hangi, pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scolastika Kevela."
"Ushiriki
wetu katika mkutano huu ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutengeneza fursa
muhimu kwa wanawake wajasiriamali kupata rasilimali za kifedha, ushauri, na
msaada wa kukuza biashara zao," alisema Esther.

Benki
hiyo imelenga kuondoa vikwazo vinavyowakwamisha wanawake katika kupata huduma
za kifedha na kupanua biashara zao kwa kuanzisha huduma zinazokidhi mahitaji
yao. Pia, benki imejipanga kuwa karibu na wanawake wajasiriamali kwa kuandaa
mikutano na semina zitakazowasaidia kufanikisha maendeleo ya biashara zao.
Mkutano
wa Accelerate Women Summit 2025, wenye kaulimbiu "Hakuna wa
Kumzuia Mwanamke – Unstoppable Woman", ulilenga kuwaamsha wanawake
kuchangamkia fursa zinazoweza kuwawezesha kufanikisha maendeleo yao ya
kibiashara. Bank of Africa Tanzania imejidhatiti kuhamasisha mabadiliko haya
kwa kushirikiana na wajasiriamali wanawake na kukuza mfumo wa kifedha jumuishi,
ambapo kila mjasiriamali, bila kujali jinsia, anapowezeshwa, anapata fursa ya
kufanikiwa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.