Na Damas Makangale,
Kitengo
cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (University
of Dar es Salaam Computing Centre – UCC) kimeandaa warsha maalum ya siku
tatu kuanzia tarehe 20 Machi 2025 hadi 24
Machi 2025, itakayolenga kujadili na kuwajengea uwezo wataalamu wake wa
mifumo (Software Developers na Training Instructors)
katika masuala ya usalama wa mtandao (Cyber
Security).
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa UCC, Bi. Leticia Ndongole, alibainisha kuwa lengo kuu ni kuwawezesha
watendaji wa UCC kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazotokana na kasi ya
maendeleo ya teknolojia duniani.
"Katika
ulimwengu wa sasa, teknolojia inabadilika kwa kasi kubwa. Tunaona maendeleo ya
akili bandia (AI), sarafu za kidijitali kama Bitcoin, na mifumo mingine ya
kisasa. Hata hivyo, pamoja na maendeleo haya, tumeona pia ongezeko la uhalifu
wa mtandaoni, changamoto inayotukumba si Tanzania pekee bali dunia nzima.
Kupitia warsha hii, tunalenga kuwajengea uwezo wataalamu wetu ili waweze kulinda
mifumo na data za taasisi na wateja wetu kwa ufanisi zaidi," alisema
Bi. Ndongole.
UCC, ikiwa ni moja ya taasisi kinara wa TEHAMA
nchini Tanzania, imeendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta hii
kwa kutengeneza mifumo mbalimbali ya kidigitali inayotumika serikalini, katika
sekta binafsi, na hata kimataifa. Mbali na hilo, UCC pia inahusika katika kutoa
mafunzo, ushauri wa kitaalamu, na usimamizi wa mifumo ya TEHAMA kwa wadau
mbalimbali.
Warsha
hii inatarajiwa kuwawezesha washiriki kupata ujuzi wa kina kuhusu mbinu za
kisasa za kulinda mifumo dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni, matumizi salama ya
teknolojia, na namna ya kukabiliana na uhalifu wa mtandao.
Warsha hii inaendeshwa na Bwana Yusuph Kileo ambaye mtaalamu wa usalama wa mtandao, mtoa mafunzo, na mshauri wa masuala ya usalama wa kidijitali. Amejipatia umaarufu katika Afrika Mashariki na kimataifa kutokana na mchango wake katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa mtandao.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.