...Kuja na visa , credit kadi na kupanua wigo wa mawakala nchini
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BANK OF AFRICA Tanzania imeahidi kuendelea kujikita katika uwekezaji wa huduma za kibenki kwa wateja kama njia ya kukua kwa pamoja na wateja wake nchini.
Akizungumza kwenye futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa, Wasia Issa Mushi alisema kwamba benki hiyo itaendelea kuboresha huduma zake sambamba na kuja na bidhaa mpya sokoni katika jiihada za kukua pamoja na wateja wao.

“tupo mbioni kuja na bidhaa mpya kwa ajili ya wateja wetu kama vile visa kadi, credit kadi katika juhudi za kupeleka huduma zetu karibu na wateja wetu na kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za kifedha hapa nchini,” alisema
Aliongeza kwamba benki hiyo inathamini mahitaji ya wateja wake na mipango na malengo yao ni kuhakikisha kwamba yanalenga katika ustawi wa jamii ya kitanzania na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchini kwa ujumla.
Mushi aliendelea kusema kwamba mahusiano yao na wateja ni nguzo muhimu ya kibiashara kwa wateja wao wakubwa , kati na wadogo kwa hiyo ni muhimu kuendeleza mahusiano hayo kwa manufaa ya pande zote.

“tunayo furaha kubwa kuona kwamba nyie kama wateja wetu mnaendelea kuwa na imani na benki yetu katika utoaji wa huduma za kifedha hapa nchini na imani yetu mtaendelea kuwa pamoja na sisi,” aliongeza Mushi.
Alisema kwamba benki hiyo kwa sasa ina mawakala zaidi ya 200 nchini nzima na ina mipango kabambe ya kuhakikisha kwamba wanakuwa na mawakala 500 ifikapo mwisho wa mwaka huu.
“tutaendelea kupanua huduma zetu kila siku na kuongeza idadi ya mawakala hapa nchini ili kuhakikisha bidhaa na huduma zetu zinasambaa nchini nzima na kurahisisha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara,” alifafanua
Kwa upande wake, mgeni rasmi wa shughuli hiyo , Katibu wa Baraza la Ulamaa nchini , Shekhe Hassan Chizenge alisema kwamba jumuiya ya waislamu nchini imefurahisha kwa kukutanishwa pamoja na kuweza kufuturu kama sehemu ya mahusiano yao pamoja na benki hiyo.
“Jambo kubwa katika hafla hii ya kufuturu pamoja na mambo mengine ni kufahamiana miongoni mwetu ni jambo la heri ambalo benki hii ya Bank of Africa wameona ni busara ka kufuuru pamoja , nachukua nafasi kuwashukuru sana,” alisema Shekhe Chizenga
Alisema kwamba baadhi ya watu kama yeye walidhani benki hiyo ni ndogo ila baada ya kupitia maelezo kuhusu benki hiyo ni kubwa na imesambaaa kwenye nchini za Afrika na ni moja ya benki kongwe sana.

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji Biashara wa Benki hiyo upande wake Hamza Cherkaoui alisema kwamba wataendelea kushirikiana na wateja wake katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya fedha hapa nchini.
“Bank of Africa ni sehemu ya umiliki BCME Benki ambayo ni kundi la tatu kwa ukubwa zaidi ya kibenki nchini Moroo na inapatikana katika nchini 31 na mabara manne duniani.
Aliongeza kwamba wataendelea kuja na huduma za kidigitali na uvumbuzi wa teknolojia katika kuduma za kifedha nchini na lengo kuu kuwahakikisha kwamba wanainuka kiuchumi pamoja na wateja wao na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchini.

Alifafanua kwamba ni muhimu kuendelea na ushirikiano huo na baada ya mfungo wa Ramadhani kwa kufanya kazi kwa pamoja na kwa benki hiyo itaendelea na mipango yake ya kuwasaidia wateja wadogo kukua kibiashara kwa kutimiza kwa wakati mahitaji ya kifedha sokoni.
BANK OF AFRICA - TANZANIA ni benki ya kibiashara binafsi inayofanya kazi nchini Tanzania ikihudumia wateja wa wakubwa, wa kati na wadogo SME .
Ilianza kazi zake nchini Tanzania mnamo Juni 2007 baada ya kununua Benki ya Eurafrican ambayo ilikuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu Septemba 1995.
BANK OF AFRICA - TANZANIA ni sehemu ya KIKUNDI CHA BENKI YA AFRIKA ambacho kilianza kazi zake mnamo 1982 nchini Mali.
BANK OF AFRICA GROUP ni kundi la benki la kimataifa linalofanya kazi katika nchi 18 za Afrika ikijumuisha; Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Afrika Kati na ofisi za uwakilishi huko Paris, Hispania, London, Uingereza na China.
Tangu mwaka 2010, BENKI YA AFRIKA imekuwa tawi kubwa la umiliki wa BMCE Bank, ambayo ni kundi la tatu kubwa zaidi la benki nchini Morocco, na inapatikana katika nchi 31 na mabara 4.
BANK OF AFRICA - TANZANIA kwa sasa ina mtandao wa matawi 18 ya Rejareja ikijumuisha; 9 Dar es Salaam na 9 mikoani Arusha, Mwanza, Zanzibar na miji mingine mikubwa.

Mwisho .
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.