Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni
ya Taifa gesi imeendesha semina ya mafunzo ya siku moja kwa wafanyabiashara
kwenye soko la feri ya namna bora ya kutumia majiko na mitungi ya gesi kwa
ajili ya kupikia.
Akizungumza
kwenye semina ya mafunzo hayo leo mchana katika soko la feri , Afisa Usalama
kutoka Taifa Gesi, Henry Muya alisema kwamba matumizi ya nishati safi kwa ajili
ya kupikia , usalama na kulinda afya za watumiaji.
“Serikali
ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan inafanya jitihada zote ili
kuhakikisha kwamba watanzania wanaachana na matumizi ya kuni na mkaa na kutumia
nishati safi ya gesi kwa ajili ya kupikia na kulinda mazingira yetu,” alisema
Muya.
Aliongeza
kwamba ni muhimu kwa wafanyabiashara ikiwemo wa Samaki nchini kujifunza kutumia
nishati safi na majiko ya gesi kwa ajili ya kupikia ili kuweza kurahisisha
shughuli zao za uzalishaji mali.
“Matumizi
ya mkaa na kuni yanaweza kusababisha madhara kwenye mfumo wa upumuaji kwa
mtumiaji kwahiyo ni muhimu kwa watanzania kupata elimu ya matumizi ya nishati
safi ambayo yanalinda mazingira kwa nchini yetu kwa ujumla,” alisisitiza Muya.
“kwa
matumizi ya majiko ya gesi yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ya
fedha na kuokoa muda wa upikaji wa chakula sehemu za biashara na majumbani,”
aliongeza Muya
Kwa
upande wake , Katibu wa Soko la Feri, Nassoro George Mbaga alisema kwamba ni
muhimu kwa watanzania kuendelea kutumia nishati safi na salama kwa ajili ya
kutunza mazingira.
Aliongeza
kwamba nishati safi na majiko ya kupikia ya gesi ni muhimu katika kuchochea
ukuaji wa biashara kwa wafanyabiashara wa soko la feri na kukuza uchumi wa
nchini husika.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.