Mo mjasirimali kijana mwenye mafanikio ya kipekee katika bara la Afrika
.Awa
Mtanzania wa Kwanza kutambulika na Jarida la kimataifa la Forbes Afrika
Na
Mwandishi Wetu
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini
Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea
duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali
mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla
taarifa la Jarida hilo limeeleza.
Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la
Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na
(Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa
biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa
mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni
mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani
wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha
biashara yetu toka Millioni 50 za kimarekani hadi dola Billioni 2.1 ndani ya
miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.
Mwisho.
Post a Comment