Model atoka nyumbani kwake, aenda kituo cha treni na kupanda treni kwenda kazini akiwa uchi wa mnyama.
Sehemu ambazo angekua na nguo, badala yake ameandika maneno, “shirt”, “jacket” “bra” n.k.
Tukio hilo limetokea katika mji wa Dusseldorf, Ujerumani.

Wasafiri wa treni waliopigwa na butwaa walimkodolea macho msichana huyo akionyesha umbo lake la kuvutia akiwa uchi wa mnyama (bila shaka baadhi walijifanya wanashangaa huku kimoyomoyo wanafurahia na raha zao.)

Hata hivyo, baadhi ya abiria walikua wamepoa utadhani hakuna kitu chochote kisicho cha kawaida kikiendelea. Waliendelea na safari yao bila kushangaa wala kumkodolea macho.

Safari ya model huyo ya uchi ni mojawapo ya project iliyoandaliwa na msanii kutoka Uswizi anayeitwa Milo Moire.

Sehemu ya project hiyo ni tendo alilofanya model huyo la kwenda kazini uchi, ambalo walilipa jina, “Shaking up the ordinary.”

Milo moire amesema model huyo kutembea uchi mjini ilikua na dhumuni la kuwafanya watu wa “think outside the box.”
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.