Dar es Salaam. Rais wa Marekani, Barack Obama juzi alikutana na kundi la wafanyabiashara 20 wakubwa barani Afrika wakiwemo Watanzania watatu ambao utajiri wao ulitajwa katika jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika, kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.

Tumezungumza mengi na Obama, ila ulikuwa mkutano wa ndani na mrefu, tumezungumza mengi kwa kweli.’ Reginald Mengi, Mkurugenzi Mtendaji wa IPP
Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani alikutana na wafanyabiashara hao juzi jioni katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro na kufanya nao mazungumzo kwa saa 1:23, huku waandishi wa habari wakipewa ruhusa ya kupiga picha tu.
Jarida hilo lililotolewa mwaka jana liliwataja wafanyabiashara hao kuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Group, Said Salim Bakhresa, Gulam Dewji, Rostam Aziz, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPP, Reginald Mengi na Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group, Ali Mufuruki.
Hata hivyo, juzi wafanyabiashara waliokuwa katika orodha ya kukutana na Rais Obama ni Bakhressa, Mengi na Mufuruki.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni).
Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).
Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Rais Obama alizungumza tena na wafanyabiashara wengine 170 kutoka Afrika na Tanzania kwa dakika 17, lakini hakuweka wazi walichozungumza na wafanyabiashara hao 20.
Wafanyabiashara wengine waliokuwepo katika kikao hicho ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Africa Finance Corporation, Andwer Alli, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo Afrika, Don Kaberuka..
Wengine ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera, Mwenyekiti wa Econet, Strive Masiyiwa, Mkurugenzi Mkuu wa Equity Benki, James Mwangi, Mwenyekiti wa Export Trading Group, Mahesh Patel.
Mkurugenzi Mkuu wa General Electric, Jay Ireland, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Harith, Tshepo Mahloele, Mwenyekiti wa Heirs Holdings, Tony Elumelu.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Microsoft Afrika, Ali Faramawy, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Prudential Plc, Tidjane Thiam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Peter Sands, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Symbion Power, Paul Hinks, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanjet, Susan Mashibe pamoja na Mwenyekiti wa Benki ya United Afrika, Phillips Oduoza.
Katika meza kuu Obama alikuwa amekaa pamoja na Mashibe, Mahloele, Masiyiwa na Kalumbu.

Habari kwa msaada wa gazeti la mwananchihttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mabilionea-Tanzania-wakutana-na-Obama/-/1597296/1902762/-/qp050rz/-/index.html
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.