Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la MWANANCHI-- Shirika la Viwango (TBS)
limetangaza orodha ya bidhaa 48 ambazo hazitakiwi kuwepo sokoni
kutokana na muda wa kuitumia nembo ya kampuni hiyo katika bidhaa zao
kumalizika na wahusika kushindwa kuwasilisha bidhaa zao kwa ajili ya
uhakiki kabla ya kuruhusiwa tena.
Hatua hiyo ya TBS inatokana na watengenezaji wa bidhaa hizo ambazo awali zilithibitishwa na TBS na kuruhusiwa kutumia nembo yao hiyo ya ubora kumalizika na wahusika kushindwa kuwasiliana na shirika hilo kwa ajili ya uhakiki wa bidhaa zao hizo .
Ofisa Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile aliliambia Mwananchi kuwa bidhaa hizo kuanzia hivi sasa hazitakiwi kuonekana sokoni na msako utaanza wakati wowote kuziondoa na zile ambazo zitakamatwa wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Tumetoa tangazo lakini kabla ya hapo tuliwapa muda wawe wameleta bidhaa zao kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kuruhusiwa kuendelea kutumia nembo yetu,akini wamekaidi ndio maana tumewatangazia kama utaratibu unavyoagiza” alisema Rhoida.

Post a Comment