Msichana mwenye umri wa miaka 22 mkaazi wa Mjini Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba amefanyiwa kitendo cha kinyama cha kubakwa na kisha kutelekezwa na dereva wa gari lilikokuwa limempa msaada na kupitishwa sehemu ambayo alikusudia kwenda .
Tukio hilo limetokea juzi majira
ya saa kumi za jioni katika eneo la Weni Wete ambapo msichana huyo (jina linahifadhiwa)
kubakwa na kutelekezwa kutokana na dereva wa gari hiyo kumkimbia baada
kutekeleza kitendo hicho .
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan
amesema tayari jeshi hilo linamshikilia kijana Mohammed Kaithar Ali (45) Mkaazi
wa Wete ambaye anatuhumiwa kuhusika na kitendo hicho .
Amesema kuwa mtuhumiwa huyo
ametekeleza kitendo hicho baada ya kutakiwa kumpa msaada (lift) kwenye gari lake
na alipofika maeneo ya Weni kijana huyo alifunga vioo vya gari lake na kisha
kumtia machepe mdomoni ili sauti yake isitoke .
Kamanda Shekhan amefahamisha
kwamba msichana aliyefanyiwa kitendo hicho amepata maumivu sehemu zake za siri
pamoja na kupata michubuko shingoni ambayo imetokana na harakati za kutaka
kujinasua ili asifanyiwe kitendo hicho .
‘Kwa kweli mtuhumiwa anadaiwa
kutekeleza kitendo hicho tayari yupo mikononi mwa jeshi la Polisi ,na msichana
aliyebakwa yuko chini ya uangalizi wa daktari licha ya kwamba alitibiwa na
kuruhusiwa kurudi nyumbani .
Aidha Kamanda Shekhan amewataka
wananchi kuwa makini na madereva ambao sio waaminifu na kujiepusha kuomba
msaada kwa madareva wasiowafahamu ili kuepusha kutokea kwa matenda ambayo
yanaweza kuepukika.
Akizungumzia operesheni ya kamata
kamata inayofanywa na jeshi hilo kwa madareva , Kamanda Shekhan amefahamisha
kwamba zaidi ya magari 50 yamakamatwa na baada ya kufanyiwa uchunguzi magari 23
yamabainika kuwa hayafai kutembea barabarani .
Amesema kuwa madareva wa magari
hayo wamefikishwa mahakamani ambapo wametozwa faini ya kati ya shilingi elfu 80
na lakai tatu kutokana na makosa yaliyobainika kwenye magari yao .
Amesema kuwa operesheni hiyo
itakuwa ni endelevu na ina lengo la kuhakikisha kwamba madereva , abiria pamoja
na wamiliki wa magari hizo wanatii sharia za usalama wa barabarani bila ya
kushurutishwa.
Na Masanja Mabula –Pemba
Post a Comment