Baadhi ya wafanyakazi Kampuni ya Kupakua na Kupakia Kontena Bandarini (TICTS) wakiwasili kwenye ufukwe wa bahari ya hindi maeneo Kata ya Kivukoni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kusafisha fukwe hizo katika kuhitimisha kampeni usafi iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd mwishoni mwa juma |
KAMPENI kubwa ya kuhamasisha usafi iliyokuwa inaendeshwa
kampuni ya Green Waste Pro Ltd katika kata tatu za katikati ya jiji imemalizika
kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kufanya eneo hilo kumeremeta tena
Kampeni hiyo ambayo ilianza Septemba 6 mwaka huu
ilifungwa kwa usafi katika kata ya Kivukoni ambapo kampuni ya TICS
ilishiriki kufanya usafi katika fukwe za bahari.
Katika kampeni zilizoshirikishwa wadau mbalimbali wa
mazingira na afya katika kuhamasisha usafi miongoni mwa wananchi pamoja na
kufanya usafi viongozi walitumia nafasi hiyo kufunza watu umuhimu wa kushiriki
katika kufanya usafi na kuwa wasafi.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa
alisema usafi huo umelenga kuweka maeneo ya bandari kuwa masafi na
japokuwa wao wapo Temeke waliona kuna kila sababu ya kushiriki usafi kwenye
maeneo ya bahari ambayo wanafanyia kazi.
Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus
Ruhungu alisema kampeni hiyo ambayo imefanikiwa, ilikuwa inawakumbusha wananchi
wajibu wa kushiriki katika kuweka maeneo safi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TICTS, kampuni ya
usafi ya Green Waste Pro Ltd na watendaji wa halmashauri pamoja na viongozi wa
kata ya Kivukoni wakichukua vitendea kazi tayari kuanza kusafisha fukwe za
bahari ya hindi.
Alisema katika kampeni hiyo wamefanikiwa kushawishi
wananchi kutambua kwamba usafi si kazi ya serikali pekee bali hata wao na
kwamba eneo linapokuwa safi ni sifa ya wananchi na wahusika wengine.
Aliwataka wananchi waguswe kuwa suala la usafi si la
serikali bali la kila mmoja kutokana na ukweli kuwa wanapougua kutokana na
mazingira kuwa machafu ni tatizo binafsi zaidi japokuwa serikali itawajibika
kusaidia tiba.
Alisema pia kwamba ushiriki wa TICTS katika kampeni hizo
siku za mwisho kunadhihirisha kwamba suala la usafi halina mipaka kwani kila
mmoja linamgusa kwa namna moja au nyingine hata kama hakai eneo lile.
Eneo ambalo limefanyiwa usafi ni lile ambapo limetumika
kuuza madafu na bidhaa nyingine huku wala madafu wakiacha vifuu katika
eneo hilo na hivyo kutia aibu kutokana na eneo hilo kutumiwa kama njia kuu ya
viongozi.
Naye Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd,
Abdallah Mbena amesema kwamba wamefurahishwa na kampeni hiyo kutokana na
mabadiliko makubwa yaliyojionesha katika maeneo ambayo wamekuwa wakiyasimamia
usafi.
KAMPENI kubwa ya kuhamasisha usafi iliyokuwa inaendeshwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd katika kata tatu za katikati ya jiji imemalizika kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kufanya eneo hilo kumeremeta tena |
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushiriki wao kwenye zoezi la kusafisha mazingira yanayozunguka fukwe za bahari ya hindi kata ya Kivukoni lililokuwa likiendeshwa na kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Katikati ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena na Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu |
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo alitoa pongezi kwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd kwa kuifanya manispaa ya Ilala kuwa safi na kutaka kampuni zingine za usafi kuiga mfano wa kampuni hiyo na kuwaasa wananchi kutoa ushirikiano wa masuala ya usafi wa mazingira kwa sababu ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mazingira yetu yanayotuzunguka yanakuwa safi wakati wote |
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TICTS na Green Waste Pro Ltd wakishirikiana kusafisha fukwe za bahari ya hindi wakati wa kuhitimisha kampeni ya usafi iliyokuwa ikiendeshwa na Green Waste Pro Ltd |
Post a Comment