Chama cha Wananchi (CUF), kimesema hakuna Mjumbe katika chama hicho wala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), atakayeshiriki katika zoezi la upigaji kura kwa njia ya mtandao.

Kauli hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samuel Sitta, kuruhusu kura za maoni kutoka kwa wajumbe wahusika ambao wako nje ya nchi kwa sababu maalumu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama (CUF), Yusuph Salum, alisema endapo Sitta, ataruhusu zoezi hilo liendelee hakutokuwapo na Rasimu ya Katiba mpya halali.

“Sitta, kama ana nia ya kuleta migogoro ndani ya vyama, aanze kutatua ile ya chama chake, na endapo anahalalisha kuwa wajumbe wa CUF, wamepiga kura kupitia mitandao ni uongo mtupu kwasababu hayupo hata mmoja kati yetu aliyefanya hivyo kinyume na makubaliano yetu,” alisema Salum.

Aidha, alikanusha taarifa za mjumbe wake, Abubakari Hamis Bakari, kutoshiriki katika zoezi la uandishi wa Rasimu ya Katiba ingawa Sitta, amehalalisha kufanya hivyo.

“Kifupi Bakari, hajashiriki katika zoezi la upigaji kura kwa njia ya mtandao na wala hatafanya hivyo kulingana na sera ya makubaliano yao.”

Mwanachama wa chama hicho, Joran Bashange, alisema kitaratibu kura hizo hazitofungwa kimafungu badala yake ziwekwe wazi ili kuondoa utata baina yao na Kamati iliyoteuliwa.

Kamati hiyo ina wajumbe 16 akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na wajumbe watatu kutoka CUF.

Baadhi ya wajumbe kutoka CCM, ni Balozi Seif Hamid, Mohammed Abood, Omary Yusuf Mzee, Asha Bakari Makame, Mgeni Hassan Juma na Mahmood Hassan Musa.

Wajumbe kutoka CUF ni Abubakari Hamis Bakari, Omary Ally Sheha na Abdallah Juma Ally.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.