Huwa nakumbuka sana wakati tunasoma shule zetu za Kayumba na pengine hata za sekondari kwamba kulikuwa kuna kufaulu na kufeli, kuwa wa kwanza au kuwa wa mwisho yote haya yalikuwa ni matokeo tu.


 
 Darasani kwetu kulikuwa na wanafunzi waliokuwa wakisoma sana ili waweze kuwa wa kwanza lakini kuna waliokuwa wakifanikiwa katika hilo wengine hawakuwai kufanikiwa ila wote walikuwa wakifaulu.

Sasa tatizo ni wivu ulikuwa kwa hawa "magenius", wakati sisi tukihangaika kuparangana na makaratasi wao walikuwa nje wakivuna karanga na kucheza mpira wa makaratasi (Chandimu) ila shughuli yao utaiona  kwenye mtihani wa mwisho huwakosi nafasi kumi bora wakati mimi na wewe wasomaji hata hatujakaribia nafasi hizo japo tulijihesabia kuwa tumefaulu.


Huwa nikikumbuka na kuwaza hivyo ndipo ninapoona kuwa kila kitu kina "genius" wake na hata soka nalo lina genius wake na ndani yake kuna watu tofauti katika vitengo tofauti.

Watu kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Diego Costa na Luis Suarez ndiyo "magenius" wa magoli hivi sasa. Hawa jamaa wanalijua sana goli yani hata ukiwaamsha usingizini wakacheze mpira lazima watakufunga tu.


Na hivi Sasa katika ulimwengu wa soka magoli hayatimii bila pasi za akili na upendo na katika hili huwezi kupingana na mimi kama kuna "genius" wake na huyu si mwingine ni ANGEL DI MARIA japo najua wako "magenius" wengi ila hata magenius wana madarasa tofauti nami naamini kwa sasa Di maria ni genius wa daraja la juu.

Tusiende mbali sana lakini tujaribu kukumbuka utamu wa huyu jamaa na Mesuit Ozil wakati wako Real Madrid au utamu wa huyu jamaa na mchezaji bora wa dunia kwa sasa ndo utajua kwa nini Di maria ni mpiga pasi wa daraja la kwanza "genius".


Binafsi na huenda ikawa kweli kwamba ukiwa darasa moja na genius lazima utafaulu au utanukia kufaulu maana atakupa hasira ya kusoma japo huwezi kumfikia.

Pale Manchester United neema imewafikia,upendo na baraka uko kati yao sasa yani hata watu ambao walishasahau kufunga sasa neema imewatembelea na watafunga tu. Hivi ulilitazama vizuri goli alilofunga Juan mata,lile goli lingeweza kufungwa kwa staili nyingi tofauti za kiufundi lakini Mata alichagua ufundi ule kutupia nyavu.


Sasa kila akishika mpira Di maria mabeki huwa wanawaza pasi zake za upendo atapewa nani, maana kwa huyu jamaa kila mtu yuko katika nafasi ya kufunga,  sikatai Cristian Ronaldo ndo mchezaji bora wa sasa japo ana uwezo binafsi ila hatokaa asahau pasi za fundi huyu.

Kwa sasa ni zamu ya darasa la mashetani wekundu kusoma na kumtumia genius huyu naamini watafaulu tu na kuingia katika nafasi bora. 


Tabasamu la mwalimu wake Van gaal liliashiria mengi ikiwemo kufurahia kumuona mtu mwenye hasira za miguu lakini mpole wa sura na hata jina, sasa mashetani hao  wana kazi moja tu ya kustahimili maelewano ya timu yao na kuhakikisha di maria anapumzika tu uwanjani akifikiria kumpa pasi Radamel Falcao au Robin Van persie.

Katika fainali za kombe la dunia mjermani alistahili kombe lile japo katika mechi ya fainali hakucheza vizuri katika ubora wake, huwa nawaza kwamba di maria angekuwepo pengine tungekuwa na hadithi tofauti midomoni mwetu. 


Kwa pasi zake za upendo,jinsi anavyounyonga na kuukokota mpira kwa mbwembwe zake kwanini usimshukuru na kwanini usimhifadhi ili kumtumia na kesho, hapa naamini mwalimu Van gaal amepata mwanafunzi bora katika somo lake na sasa ni juhudi za shule na mwalimu huyo wa darasa kubembeleza na kutafuta wanafunzi wengine bora katika masomo mengine.

Asante mpiga pasi wa daraja la kwanza na "genius" Di maria.

Source by www.wapendasoka.blogspot.com
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.