Na Happiness Katabazi
BAADHI ya vyombo vya habari leo vimemnukuu Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP- Ernest Mangu akisema jeshi lake limefanikiwa Kumtia nguvuni
mtu mmoja ambaye wanamhutumu alihusika moja kwa moja na tukio la
uvamizi Kituo cha Polisi kilichopo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita,
Septemba 5 Mwaka huu ,usiku na kuua polisi wawili na kuiba silaha
mbalimbali Mali za Jeshi Hilo.
Kwa mujibu wa IGP- Mangu, mtu huyo ambaye hakumtaja jina alikamatwa
Septemba 6 Mwaka huu, usiku huko Mkoani Geita akiwa na silaha
mbalimbali yakiwamo mabomu ya machozi.
Mangu alisema baada ya kumkamata mtu Huyo ambaye hakutaka Kumtaja jina
kwasababu bado wanaendelea na upelelezi, mtu Huyo aliwaonyesha mahali
zilipo bunduki sita aina ya SMG, pump action tatu na mabomu 11 ya
machozi, kitendo ambacho kinaonyesha moja kwa moja alihusika kwenye
tukio la uvamizi wa Kituo hicho Polisi Bukombe na kuua Askari wale
Polisi ambao hatakuwa na hatia.
“Jitihada za kumkamata mtu huyo zilifanywa na polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama,” alisema IGP- Mangu
Jana Katika ukurasa wangu huu wa Facebook niliandika makala iliyokuwa na
kichwa Cha Habari kisemacho ' POLISI MALIZANENI NA MAJAMBAZI WA AINA
HII'.
Maudhuhi ya makala hiyo yalibeba ujumbe wa kulaani tukio la Mauji ya
Polisi ndani ya Kituo Cha Polisi Bukombe baada ya watu wasiyojulikana
kuvamia Kituo hicho wakiwa na silaha za kivita na kuua Askari Hao na
Kisha kutokomeza na silaha mbalimbali.
Nikiwa muumini wa Amani Narudia tena Kusema wazi Kuwa nachukizwa na Uhalifu wa aina yoyote.
Ndani ya makala ya Septemba 7 mwaka 2014 nilieleza wazi kuwa binafsi
ninaliamini Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama pindi
vinapoamua kuacha mzaa na kufanyia Kazi kikamilifu jambo Fulani.Vikiamua
kulivalia njuga jambo Fulani ulifanya kwa haraka na mwisho wa siku
ufanikiwa kutimiza adhima Yao.
Na mfano mzuri ni tamko la IGP- Mangu kwa vyombo vya habari Leo ambapo
Amedai Katika Hatua za awali za wapelelezi toka vyombo mbalimbali Vya
Ulinzi na Usalama wa kishirikina na Jeshi lake, juzi usiku walifanikiwa
kumtia nguvuni mtu mmoja ambaye wanamshuku moja kwa moja alihusika
kutenda unyama ule ambao siyo tu umekatisha uhai wa askari polisi wawili
wa siyo na hatia lakini tu naweza Kusema tukio Hilo limelidhalilisha
pia jeshi la Polisi.
Kwa sasa ' watoto wa mjini' tunasema haiwezekani kupigwa au kufanyiwa uhuni ' Viwanja Vya nyumbani'.
Sasa wahuni / majambazi ambao watoto wa mjini tumewapachika jina Kuwa '
hawana dini', kwa jeuri wameweza kuwafanyia uhuni Polisi Katika
'Viwanja vyao Vya nyumbani' yaani ndani ya Kituo Cha Polisi Bukombe.
Inatisha sana.
Narudia tena tukio Hilo na matukio mengi ya Uhalifu yananikera, naamini
huo ni mwanzo mzuri tena Katika muda mchache tu tangu wahuni Hao
wafanye mauaji hayo na vyombo Vya Ulinzi na Usalama vikafanikiwa
kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye aliwapa ushirikiano polisi akaenda
kuwaonyesha silaha alikokuwa ameziifadhi.
Naamini mtuhumiwa Huyo hakuwa peke yake Katika tukio lile la kinyama
kwasababu kwa mujibu wa maelezo ya Jeshi la Polisi kuhusu tukio lile,
yanadhiirisha wazi waliotenda tukio ile ni zaidi ya mtu mmoja.
Hivyo navitia moyo vyombo vyote Vya Ulinzi na Usalama kuakikisha
wanakamata bila kuonea mtu, mhalifu yoyote aliyeshiriki Kutenda tukio
lile kwasababu Uhalifu huu wa kuvamia Vituo Vya Polisi sasa umeanza
kuonekana ni Fashion mpya ya majambazi kujipatia silaha.
Kwani tungali tukikumbuka tukio Kama Hilo lilitokea Juni 11 Mwaka huu,
Katika Kituo Cha Polisi Mkamba Wilaya Ya Mkuranga Mkoani Pwani, ambapo
majambazi Hao walimua Askari Polisi mmoja Joseph Mbilinyi na kuondoka na
silaha lakini hata HIvyo siku Chache baadae wahalifu Hao walikamatwa na
kufikishwa mahakamani.
Na ninawasikitikia sana Nyie wahalifu mtakao kamatwa na kuhusishwa na
tukio Hilo Kwani ni lazima mtashitakiwa na Kesi zaidi ya Moja.Kesi ya
kwanza itakuwa ni Kuua kwa kukusudia Askari Hao kinyume na Kifungu ha
196 Cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002, Kesi ya Polisi kukutwa
na silaha Mali ya Jeshi la Polisi na makosa mengine ambayo Mwanasheria
wa Kanda atawandalia Kesi nzuri sana 'iliyosimama' na kuwafikisha
mahakamani.
Mkae mkijua kosa la kuua bila kukusudia halina dhamana na wapelelezi
wa Kesi hizo Zenu ni Jeshi la Polisi ambao mlienda kuwavamia na kuwaua
Polisi wenzao kinyama na kuiba silaha kituo chao cha polisi Bukombe
na kuwaua askari wenzao na kuiba silaha zao.
Nawaonea huruma sana Nyie wahalifu wote mtakao kamatwa na kushitakiwa
kwa tukio la kuvamia, kuiba silaha na kuua askari Kituo cha Polisi
Bukombe, kwasababu uenda hamkufahamu madhara mtakayopata baadae baada ya
Kutenda tukio Hilo.Kwa taarifa yenu Polisi ni ' wahuni' sana kushinda
Nyie.Nawasikitikia sana.
Hongera sana vyombo vyote Vya Ulinzi na Usalama vilivyoshirikiana na
Jeshi la Polisi kumkamata Mtu huyo Septemba 6 mwaka huu na silaha hizo
ikiwa ni siku Moja tu tangu tukio Hilo la Uhalifu litokee Septemba 5
mwaka huu, na ninaomba mzidishe kasi Katika upelelezi wa kuwasaka
wahalifu wengine bila ya kumuonea ili mwisho wa siku wakakutane na mkono
wa Sheria.
Uhalifu haupaswi kufumbiwa macho na wala wahalifu hawapaswi kuchekewa.
Waswahili wanasema ' Ukicheka na Nyani utavuna mabua'. Sasa vyombo Vya
Ulinzi na Usalama iwe ni mwiko sasa kucheka Cheka na wahalifu Kwani
mwisho wa siku ndiyo Kama HIvi wahalifu hawa wamevuka mstari na kwenda
kuvamia Vituo Vya Polisi.
Post a Comment