Benki ya Barclays Tanzania imezindua mpango wa kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa kuweka dhamana katika huduma zake kwa wateja.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mipango
na Bidhaa na Kaimu Mkurugenzi wa wateja binafsi, Musa Kitoi alisema kuwa katika
mpango huo wa dhamana katika huduma, benki inaahidi kutoa huduma zake kwa muda
na kipimo kinachokubalika.
“Siku
zote tunahakikisha mteja anapoingia katika benki yetu anapata huduma bora kama
anavyotegemea na kwa kupitia dhamana hii ya huduma tunatoa ahadi kuwa huduma
zetu zitakuwa bora maradufu.
“Kwa
kuanzia, mteja yeyote atakayeomba kadi ya ATM, atapatiwa katika muda usiozidi
dakika ishirini na vile vile kwa wanaohitaji vitabu vya hundi watapatiwa ndani
ya siku tano, viwango hivi ni vya juu sana katika soko letu.
“Lakini
pia, pale tutakapogundua kuwa mteja hakupata huduma kama tulivyomuahidi
tutahakikisha tunamlipa fidia ndani ya masaa 24,” alielezea Bw Kitoi.
Alisema
kwamba Barclays inajizatiti kutoa huduma tofauti za kibenki kwa wateja wake
ambazo zinatumia teknolojia ya hali ya juu na pia huduma za viwango vya juu
kupitia wafanyakazi wake.
Kitoi
alifafanua kwamba benki hiyo imepiga hatua kubwa kuboresha njia mbali mbali za
utoaji wa huduma kwa kuzindua mipango ya kupunguza foleni katika matawi yake na
kuondoa utumiaji wa fomu za kibenki ambazo zinachelewesha utolewaji huduma
haraka.
“Nia yetu ni kuwa benki inayotoa huduma haraka
zinazostahili kwa wateja wetu na tutaendelea kuleta mabadiliko mbalimbali yenye
nia ya kuboresha huduma, ziwe za kisasa ili kutimiza azma yetu ya kufanya
huduma za benki kuwa rahisi kupatikana na kwa haraka na hivyo kuwapa wateja
wetu muda zaidi wa kushughulikia biashara zao,”
alielezea zaidi Bw Kitoi.
Kwa
upande wake, Meneja wa Miradi na Mikakati ya Kibenki wa Benki hiyo, Jane Mbwilo
alisema kwamba hivi karibuni Barclays ilizindua huduma ya benki bila kutumia
makaratasi ambayo inaruhusu wateja kuweza kutoa na kuweka fedha kwa kutumia tu
kadi zao na hivyo kupunguza muda mwingi unaotumika kujaza fomu mbali mbali za
kuombea huduma.
Aliongeza
kwamba benki hiyo imewekeza katika technolojia mbali mbali ili kutoa huduma za
kisasa na kwa bei nafuu.
Post a Comment