Metl yajipanga kupanua soko lake la mafuta Afrika mashariki na kusini
Na Damas Makangale wa Makangale Sattellite
KAMPUNI ya Mohammed Enterpries (Metl) kupitia kampuni
yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini ya Star Oils Ltd
imepata mkopo wa bilioni 100 kutoka kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya
hafla ya utiliaji saini wa mkopo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,
Afisa Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini, Mhe, Mohammed Dewji (MO)
amesema mkopo utafungua mianya zaidi kwa kampuni ya Star Oils kusambaza mafuta
nje na ndani ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi Mizinga Melu na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Metl, Nhe Mohammed Dewji wakitiliana saini ya mkopo huo wa
bilioni 100
|
Amesema kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya
timu ya wataalamu kutoka Metl makao makuu na maafisa wa NBC kutoka nchini na
Afrika Kusini wamefikia makubaliano ya kupata mkopo huo mkubwa na wa aina yake
katika sekta ya mafuta hapa Tanzania.
Amesema kwamba kampuni ya Star Oils ina mipango ya
kusambaza mafuta katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la Sahara
ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kujipanua kibiashara ndani na nje ya
Afrika.
"Mpango huu utaiwezesha
Star oils kupanua malengo yake katika soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na
kukuza uzalishaji na usambazaji wake katika ngazi ya Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la sahara," amesema
MO
MO aliongeza kuwa hatua
ambayo kampuni hiyo imefikia ni kubwa kwa kuonyesha dhamira ya kuwekeza na
kufanya biashara ya mafuta Afrika mashariki na kusini mwa jangwa la sahara.
"Mkopo huu utasaidia kampuni
ya star oil kuongeza uzalishaji na usambazaji wa
mafuta ya kwenye soko la Afrika mashariki na kusini mwa Afrika,”
"Sisi tuna mipango ya kuanza
kusambaza mafuta na
bidhaa za petroli katika nchini
za Kusini mwa Afrika
kama sehemu ya jitihada za kampuni za
kupanua biashara zake katika soko la
Afrika," amesema.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Star Oils Ltd,
Nazir Haji amesema kwamba mkopo huo utachochea chachu ya uzalishaji, uhifadhi
na usambazaji wa mafuta na kusukuma maendeleo ya sekta mafuta nchini.
Amesema kwamba kampuni ya Star Oils inajipanga kufanya
biashara ya mafuta kuwa endelevu hapa nchini na Afrika mashariki ili uchumi wa
nchi za Afrika mashariki ziweze kukua kwa kutegemea tija ya uzalishaji wa
mafuta.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi Mizinga Melu amesema
kuwa benki hiyo inahitimisha
safari ya majadiliano na kampuni mama ya Star Oils, Mohammed Entrepries
Tanzania Limited (Metl) ya mkopo wa bilioni 100.
"Star oils ni kampuni dada ya METL ni moja ya makampuni yanayokwenda kasi
katika biashara ya ushindani katika Afrika Mashariki na Kusini
mwa jangwa la sahara na rekodi yao ya mauzo na biashara ni ya kuridhisha,"
amesema.
Aliongeza
kwamba METL ni moja ya makampuni yalionyesha rekodi nzuri
katika biashara ya viwanda, nguo, vinywaji, bima na mafuta na wanastahili
kuwezesha kwa kupata mikopo mikubwa na ya muda mrefu kupitia taasisi za kifedha
nchini na nje ya nchi,”
"Sisi kwenye benki ya NBC tunayofuraha kubwa kwa
kupata nafasi ya kufanya biashara na moja ya makampuni yanayokuja kwa kasi
katika bara la Afrika na vile vile NBC ni benki ambayo ipo tayari kusaidia
wateja wake,” aliongeza
Bi Melu alisisitiza
kuwa baada ya NBC kuridhisha
na shughuli za kibiashara na mzunguko wa fedha wa Metl wameamua kutoa mkopo huo
ili waweze kupanua biashara yao katika masoko ya kimataifa.
Star Oils kwa sasa inatekeleza awamu ya pili
ya mradi mkubwa wa kuhifadhi mafuta ya petroli na baadaye kujenga
usambazaji wa mafuta nchi nzima kwa njia
ya mlolongo wa vituo vya karibu
200 ya petroli nchini.
Uwezo wa jumla ya
uhifadhi wa kituo hiki juu ya
kukamilisha mradi itakuwa lita 68 milioni, kuundwa tu kwa ajili ya kuhifadhi ya petroli, gesi mafuta
na mafuta ya taa. Wingi wa bidhaa hizi kwa
sasa ni kuuzwa kwa misingi ya
jumla na mipango ya baadaye soko
yao kupitia vituo vya METL
Group vya rejareja vya petroli.
NBC imetiliana saini ya mkopo wa shilingi za kitanzania
bilioni 100 na kampuni ya kusambaza mafuta ya jijini Dar es Salaam, Star Oils
Ltd katika mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya mafuta nchini.
Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji, Andre Potgieter akizungumza na wageni waalikwa kwa kuonyesha shughuli mbalimbali na bidhaa huduma za benki hiyo |
Mkuu wa Idara wa NBC, Huduma Kibenki akipeana mkono wa
pongezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Metl, Mhe, Mohammmed Dewji.
|
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi Mizinga Melu akizungumza
kwenye hafla hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
|
Baadhi ya wageni waalikwa
|
Post a Comment