Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wamewajia juu waliokuwa Wajumbe wa Kamati ya Kukusanya Maoni ya Katiba wakidai kuwa kazi yao ilishaisha, hivyo kuendelea kujadili masuala kuhusu Rasimu ya Katiba si sahihi.


Baadhi ya wajumbe hao walitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana, wakati wakichangia Azimio la Kufanyia Marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalumu iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho.

Mjumbe Dk Hamisi Kigwangwala, ambaye ni Mbunge wa Nzega, alisema ni vyema Mwenyekiti wa
Bunge, Samuel Sitta akashauri wajumbe wa Tume hiyo ambao ni wazee wenzake kwamba jukumu lao limeisha na kwa uungwana waachie Bunge Maalumu lifanye kazi yake:

“Wajumbe wale kazi yao ilishaisha, lakini kila siku wanakosoa, mara midahalo, makongamano. Wazuiwe kufanya hivyo, hata waambiwe tu kibinadamu maana hata sisi hatukuwaingilia wakati wanaendesha mchakato wao.

“Wanatuponda sana kana kwamba hakuna cha kujadili, kama ni hivyo zile siku 70 zilikuwa za nini?” 

Naye Dk Zainab Gama, alisema kazi ya Tume ya Katiba ilishaisha na kwamba kwa wanaopiga kelele
nje ya Bunge Maalumu la Katiba watakuwa na lao jambo nyuma ya pazia.

Mjumbe Hamad Rashid Mohammed, ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema kwa taratibu za mabunge jambo lolote likishawasilishwa bungeni linakuwa chini ya mamlaka ya Bunge, ambalo nalo linafanya kazi kwa niaba ya wananchi.

Dk Pindi Chana akichangia, alisema ambao hawajarudi bungeni hawawatendei haki Watanzania.
Kwa upande wake John Cheyo alisema hakuna haraka ya kupata Katiba na kwamba ni vyema umakini mkubwa ukawepo katika kuhakikisha inapatikana Katiba bora.
“Tusiharakishe suala la Katiba, kama tunaona gharama basi tujaribu fujo, ghasia na kutoelewana, hiyo ndiyo gharama zaidi,” 
alisema. (via HabariLeo)

Mjumbe wa Bunge Maalumu, Kundi la Vyama Vya Siasa, Peter Kuga Mziray, ambaye pia ni Rais Mtendaji wa APPT-Maendeleo, amesema katiba nzuri zote zimetungwa na watu wachache zaidi.
Alisema wanaoandika Katiba ni wazalendo na kwamba hata yeye asipokuwepo katiba lazima itatungwa kwa kuwa katiba si ya mtu mmoja au kundi fulani.

Alisema hayo akijibu hoja za waandishi wa habari kuhusu bunge la Katiba ambalo linaanza ngwe yake ya pili.

Alisema hata yeye akiwepo hapo asiwepo katiba lazima itatungwa na anaamini kwamba Watanzania watapata katiba mpya na bora zaidi.

Bunge la Katiba linaanza leo na kama kusipokuwapo na mabadiliko, japo wabunge wengi wa ukawa wanaonekana mjini hapa, bunge hilo litaendelea kujadili hoja muhimu zilizopo mezani ambaozo zinagusa rasimu takribani 15 zilizobaki.

Alisema Bunge hilo haliwezi kukwamishwa na kutokuwapo kwa ukawa, na wakati mazungumzo yanaendelea ya kuwarejesha ukawa bungeni, bunge litaendelea kwa kuwa ana matumaini koramu itapatikana.

“Mimi nawasihi tu wenzangu warejee, bungeni kila mtu anawaisihi wao wanakataa,” alisema Mzirai na kufafanua kwamba wasiporudi wana lao jambo kwani hiyo katiba wanayosema ni ya wananchi, wananchi wenyewe ukiacghia wanasiasa wachachre wanawasilishwa na taasisi ambazo zimesema warejee bungeni.

“Ukiachia Kakobe, makanisa yote yametaka ukawa warejee Bungeni, taasisi ya umoja wa mataifa imesema, waislamu wamesema,” alizungumza Mzirai na kusema kama wote wamesema wakiendelea kukataa lazima tujihoji nyuma yao kuna nani.

Pamoja na kusisitiza kwamba katiba itapatikana pamoja na matatizo ya kisera ambayo ndiyo yanaozinga muundo wa serikali amesisitiza haja ya vyombo vya habari kuacha kushabikia mambo ambayo yanawatenga zaidi watanzania badala ya kuwarejesha pamoja.

Alisema vyombo vya habari vimekuwa na tabia ya kukatisha tamaa (negativity) ambayo haifai katika suala zima la kujenga uwezo wa kufikia muafaka wa katiba kwa manufaa ya taifa.

Alisema uandishi wenye mwelekeo wa kukwamisha kinachoendelea katika bunge si tu hauwapatii watanzania nafasi ya kufanya maamuzi lakini pia inaonesha waandishi nao wamekuwa chama kingine cha siasa kikifurahia mambo yanayokwamisha mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba.


Pamoja na kusema kwamba kazi ipo Mziray alisema anaamini kwamba watanzania watapata katiba wanayoihitaji na matatizo ya sasa yamejikita zaidi katika uroho mwa madaraka na matatizo ya kisera.

“Watu wajifunze kupokea na kutoa… hili suala la kisera si rahisi hivyo… ni lazima kujifunza kutoa na kupokea,” alisema Mzirai akifafanua kwanini anaona ni vyema UKAWA wakarejea bungeni na yafanyia kazi yale yanayowezekana.

Alisema serikali mbili au tatu ni misimamo ya kisera ambayo haiwezi kubadilishwa kwa mtu mmoja lakini yapo mambommengi ya muhimu kwa upande wa upinzani na wananchi ambayo yakifanyiwa kazi inaonesha neema za baadaye.

Alitaja mambo hayo kama Tume Huru ya uchaguzi, mgombea binafsi na raslimaliza taifa.

Alisema anaamini UKAWA wakirejea ukumbini CCM italegeza mambo mengi kwa manufaa ya watu wa taifa hili.

Alisema kwa sasa upinzani ni kundi la minority (wachache) hivyo hawana sababu ya kutaka kila kitu kwani vyote vinawezekana poklepole na kwa elimu.

Alisema ni dhahiri kwa sasa CCM ambayo inasema wazi kwamba imeingia madarakani kwa kunadi sera yake ya serikali mbili haiwezi kuachia hivyo kirahisi kama sera za Chadema na CUF zinavyotaka serikali tatu.

“Kubadili ni lazima kurejea kwa wanachama wao, …lakini yapo ya msingi ya kushughulikia ambayo yanawezekana,” alisema Mzirai.

Alisema Rais amekuwa Mwungwana kuacha watu wazungumze lakini kiukweli ni kuwa wanaokwenda kwa wananchi sasa wanafanya kosa la kisheria kwani rasimu ya kwenda kunadiwa kwa wananchi haijapatikana.

Alisema vitendo vya kuzungumza kwamba kuna rasimu kwa wananchi na kuwataka wafanya si sawasawa klwani rasmu ndio ninatengenezwa sasa.

Aklisema kongamano la tarehe 9 na 10 limelenga kuwaleta pamoja wahusika wote na kuundwa kwa kamati mpya.

Mzirai anasema kama wanasiasa wakiondolewa mzizi utakuwa umeondolewa na waliobaki watatunga katiba.

Naye Diana Chilolo, mjumbe na mbunge wa viti maalumu kutoka Singida amesema ana uhakika kwamba koramu itatimia na mkutano kuendelea kwa kuwa wao wanatekeleza kazi za wananchi na wananchi wanataka vitendo.

Chilolo alisema haelewi Ukawa wanataka kuwafanyia nini watanzania kupitia rasimu hiyo.
Alisema kazi ipo Bungeni na kukaa nje kwao kuna shida kubwa ya kutotekeleza kazi walizoagizwa na wananchi za kuwapatia katiba bora.

“Sisi tumekuja kufanyakazi na kuwajibu katiba ipo na itapatikana” alisema katika viwanja vya bunge jana.

Naye aliyewahi kuwa waziri nchini hapa William Ngeleja alisema kwamba ana matumaini makubwa ya kuendelea kwa kikao kwa kuw amakundi ya uwakilishi yapo bungeni na yamefika kukamilisha kazi.

Mjumbe mwingine Magdalena Likwina amesema kwamba wao wamefika ili kuhakikisha kwamba mahitaji ya wananchi kuhusu ardhi, elimu na afya yanaelezwa kinagaubaga katika katiba.

Alisema suala la serikali kwake halina uzito mkubwa kwani kama serikali mbili haijaweza kutatua matatizo yaliyiopo serikali tatu itatatuaje?

Alisema yeye anaamini katika serikali mbili iliyoboreshwa na anafikiri wanaotaka serikali tatu hawajafanya kazi ya kutosha kuwaeilimisha kwa kuzingatia mahitaji halisi ya watanzania katika nyanja za elimu, afya na ardhi.

Alisema wanaotaka serikali 3 wanatakiwa kueleza kilichondikana ambacho kinahitaji serikali tatu na namna ambavyo kinaweza kutatuliwa kama ndio tatizo la msingi la watanzania. (via Lukwangule)
 
Source: www.wavuti.com
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.