Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni ya kutoa elimu mashuleni ya usimamizi na utawala wa fedha kwa vijana katika jitihada zake za kuwaelimisha wanafunzi wa Sekondari nchi nzima umuhimu wa kuwa na utamaduni wa kuweka akiba.
Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi Mizinga Melu alipotembelea shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa ya jijini alisema kampeni ya kujifunza utamaduni wa kujiwekea akiba ni mkakati wa benki wa kuelimisha vijana mashuleni na jamii kwa jumla nchi nzima umuhimu wa kuweka akiba kwa ajili ya baadaye.
Alisema Benki ya Taifa ya Biashara inafahamu kwa kina umuhimu wa kuwekeza na kuelimisha vijana wa leo wa kitanzania jinsi ya kusimamia mapato yao na kujiwekea akiba kwa maisha yao  baadaye ili kuhakikisha wanajifunza mbinu wakiwa bado vijana wadogo mashuleni.
Melu alisisitiza kwamba vijana ndio nguzo pekee kwa maendeleo ya nchi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwahiyo inahitajika juhudi za makusudi za kumpatia kijana wa leo taarifa, elimu ya fedha na ujasirimali katika mitaala ya masomo yao kwa manufaa ya nchi nzima.
Alisema kwamba kuna mambo ya muhimu kwenye stadi za maisha hasa katika swala la kujiwekea akiba kwa ajili ya baadaye kwa hiyo wanafunzi watafundishwa mbinu sahihi za kutunza fedha na mapato ili kupunguza utegemezi kwa walevi na wazazi na jamii kwa ujumla.
Melu alifafanua kwamba kampeni hii ya kufundisha utawala wa fedha na mapato kwa vijana itatengeneza mazingira mazuri kwa wanafunzi, walimu, wafanyakazi wa benki ya NBC and jamii kwa ujumla kushirikiana kwa karibu zaidi.
“Sisi NBC tunatambua umuhimu na nafasi vijana katika kutengeneza jamii ya baadaye kwa mantiki hiyo kwa kutambua uwepo wao tunajisikia ulazima wa kuwajengea uwezo kwa maslahi ya kizazi kijacho,’
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Maendeelo ya Vijana na Michezo ambaye alisoma hotuba ya Waziri wa Habari kwa niaba yake, Profesa Elisante Ole Gabriel alisema serikali itaendelea kutilia mkazo umuhimu wa elimu kwa vijana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa.
“Nachukua nafasi hii kuwashukuru Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kuendesha kampeni hii, kwani tunaamini kuwa kampeni hii itawafikia vijana wengi, watakaobadili mwelekeo wao wa kujitegemea na hatimaye kujijengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi, sasa na baadaye,” alisema 
 Profesa Gabriel aliendelea kuishukuru benki hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya elimu hapa nchini pamoja na hivi karibuni kuchangia bweni huko Tabora na Maktaba ya kujisomea huko Lindi ambayo ni moja ya changamoto kubwa sana kwa nchi na Serikali.
Serikali kupitia mwaka wa fedha 2013 na 2014 Wizara ya Habari, Utamaduni, Maendeleo ya Vijana na Michezo ilitenga kiasi cha Tsh 6.1 billioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana nchini.
Kwa Upande wake Mkuuwa Idara ya Masoko, Mawasiliano na Mahusiano Mwinda Kiula Mfugale alisema kupitia programu ya kujitolea kwa jamii kampeni ya kuhamasisha elimu ya utawala wa fedha na kuweka akiba imefundisha wanafunzi 3,000 na malengo kufikia wanafunzi 6,000 nchi nzima.
Mwisho..
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.