MIWANI PANA YA EDO ~ TATHMINI YA MECHI YA KWANZA YA MAN UNITED KATIKA LIGI

nikiwa mmojawapo wa mashabiki wa mabingwa wa England Manchester United leo nimeamua kuielekeza MIWANI YANGU PANA kuangazia mechi ya kwanza katika ligi ya kocha mpya David Moyes na kilichotokea katika mchezo huo ugenini dhidi ya Swansea
RVP akifunga goli la kwanza

Najua mashabiki wengi wa United walilalamika kuona baadhi ya wachezaji wakianza katika mechi ya Jana huku wale wanaowapenda wakianzia benchi hii ni kawaida kwani mashabiki wanachojua ni ushindi tu bila kufikiria unakujaje huo ushindi.

Lakini kwa miwani yangu pana nilichogundua ni kwamba kuna baadhi ya wachezaji uwepo wao Uwanjani mara nyingi hufanya timu pinzani kuingia hofu hata kutoka kabisa kimchezo. Kuna timu zikisikia mchezaji kama  Ryan Giggs au Rio au Vidic wanaanza huingiwa na hofu na kufungwa hata kabla ya mchezo na hii hutokea katika timu nyingi na kubwa mfano Barcelona jaribu tu kuangalia ikicheza bila kuwa na mastaa wake kama Messi,Iniesta na Xavi.

Hapo ndipo utakubaliana nami kwamba uwepo wa Ryan Giggs katika kikosi kilichoanza jana ni tofauti na angeanza Januzaj au uwepo wa Valencia uwanjani ni tofauti na kama angeanza Wilfred Zaha vivyo hivyo kuanza kwa Danny Welbeck ni tofauti na angeanza Jesse Lingard au Evra ni tofauti kabisa na Buttner. Sio kama Nawadharau wachezaji hao hapana hapa nazungumzia umuhimu wa kuanza na wakongwe.
Kunaweza kukawa na potential katika vijana lakini ni vizuri kama wakianzia benchi na nadhani makocha wenye akili hulitambua hilo na hapa nampa credit David Moyes.

Turudi katika mchezo husika

Magoli Manne katika mchezo wa kwanza si haba kama tukiendelea hivi kwa mechi sita za mwanzo ambazo mimi nadhani ndizo zitakazotufanya tuwe katika nafasi ya kutetea ubingwa itakua poa sana.
Danny Welbeck anaonekana amekua kimchezo japo anahitaji kufanya mengi ili kufata nyayo za aliyekua akivaa namba 19 Dwight Yorke ila ni kati ya wachezaji watakaoisaidia United msimu huu sina shaka na hili.

Wayne Rooney bado anahitajika katika Kikosi na sioni sababu ya Kumuuza au kumruhusu aondoke hapa naziangalia dakika chache alizoingia na kutoa pasi mbili za magoli. Huyu ni aina ya wachezaji ambao United wanawahitaji msimu huu hasa kwa mchango wake katika timu na kuongeza morale katika timu.

Safu ya Ulinzi ilionekana kuimarika japokua niliona kabisa jinsi Jones alivyokua akihangaika kuziba nafasi ya Rafael na sina shaka kama alifanikiwa huku muunganiko wa Vidic na Rio Ferdinand ukionekana kua imara tuombee tu wasipate majeruhi.
Upande wa ufungaji sina shaka na Robin Van Perse kwani anajua nini anachokifanya ikifikia chance za kufunga ila hofu yangu iko katika upande wa Kiungo na mchezaji gani anayeweza kumtengenezea Van Perse pasi za magoli na hapa ndo nimeanza kumwelewa Moyes na mpango wake wa kumnunua Cesc Fabrigas kwani mipira ilikua haikai eneo hilo.

Zaidi ya yote huu ni ushindi muhimu kwa benchi zima la ufundi na timu hasa ili kuanza msimu mpya na kumsahau Ferguson kama bado yupo United.

Mechi inayofuata ni dhidi ya Chelsea Jumatatu Ijayo Nyumbani Old Trafford badae United itasafiri mpaka Liverpool kuikabili Liverpool kabla ya kurudi Old Trafford kuikaribisha Crystal Palace.

Kwa leo haya ndo niliyoyaona katika mechi hiyo na ni mawazo binafsi hayana uhusiano au hayabadilishi chochote kilichotokea.

Chanzo cha habari na blogu ya wapendasoka.blogspot.com
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.