KOCHA
wa zamani wa Bayern Munich Felix Magath amedai kuwa meneja mpya wa Mabingwa wa Bavarian almaarufu kama Bayern Munich, Josep " Pep"
Gardiola amejitakia mwenyewe matatizo kwa kumsaini kiungo kinda Thiago Alcantara
kuichezea Bayern Munich msimu huu mpya.
Alcantara, Kiungo wa Spain mwenye Miaka
22, aliihama Barcelona Mwezi uliopita na kuhamia Bayern Munich kwa Dau
la Euro Milioni 20 na kuungana na Kocha Mhispania mwenzake aliekuwa
Barcelona, Pep Guardiola, ambae pia ndie alimwinua Alcantara kutoka Timu
B hadi Kikosi cha Kwanza cha Barca.
Lakini Felix Magath, aliekuwa kocha wa
Bayern Munich kati ya wwaka 2004 na 2007, amesema uamuzi wa Guardiola
kumchukua Alcantara utamletea matatizo na atajutia.
Magath ametamka: “naona ni tatizo kwa kocha Mhispania kumsaini Mhispania mwenzake. Pep atapata matatizo na
Thiago. Ama wachezaji wenzake watakasirika kwa kuwa anachezeshwa mara kwa mara au watu watahoji uhamisho wake wa dau kubwa ikiwa hachezi! Kocha Josep Gurdiola almaarufu kama Pep
angeweza kuepuka hili,"
Mbali ya utata huo, Felix Magath, ambae
Msimu uliopita alikuwa Kocha wa Klabu ya Bundesliga Wolfsburg, pia
anaamini Pep Guardiola hatashinda ile vita ya kupiku mafanikio ya Msimu
uliopita ya Kocha Jupp Heynckes ambae aliiwezesha Bayern Munich kuweka
Historia ya kuwa Klabu ya kwanza ya Germany kutwaa ‘Trebo’ yaani,
Ubingwa wa Germany, Ubingwa wa Ulaya na kubeba German Cup.
Magath amedai: “Pep ana tatizo kubwa la
kurithi Timu ambayo ilishinda kila kitu Msimu uliopita. Hivyo hawezi
kuwafanya wawe bora zaidi ya hapo!”
Post a Comment