Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya
yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya
uchaguzi. Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda
asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo
kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada
yawakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu
na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya
uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani
wake Raila Odinga akipata 5,340,546 Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama
ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa
mwaka wa 2007.
Waandishi wa BBC wanasema iwapo Kenyatta
atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu
Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi ya mshindi baadaye leo
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo
na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya
kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa
amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili
azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo
uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa
tangazo lake la mwisho.
Post a Comment