Uhuru Kenyatta ndiye Rais wa nne wa Jamuhuri ya Kenya
baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza kushinda uchaguzi wa kihistoria wa
Kenya.
Ni baada ya siku tano tangu wakenya kupiga kura
kuwachagua rais, magavana, maseneta , waakilishi wa bunge, waakilishi
wanawake na waakilishi wa wodi.
Uhuru alipata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizohitajika ili kupata ushindi kulingana na mahitaji ya katiba mpya ya nchi.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa Uhuru Kenyatta ameshinda na hivyo kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Tume ya uchaguzi ilichukua zaidi ya masaa matano
kukagua hesabu ya kura hizo kabla ya kutangaza matokeo hii leo siku
tano baada yawakenya kupiga kura.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi
yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila
Odinga akipata 5,340,546
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama
ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa
mwaka wa 2007.
Awali duru zilisema iwapo Kenyatta atakabidhiwa
ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga
atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo
na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya
kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa
amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili
azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo
uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa
tangazo lake la mwisho.
Post a Comment