Kutokana na mvua zilizoanza kunyesha hivi karibuni jijini Dar es Salaam, hali ya mazingira ya jiji la Dar es Salaam nayo imenza kuwa tete kutokana na mifereji mingi kutokufanya kazi na kusababisha kadhia kubwa  kutokana  sehemu kubwa ya jiji la Dar es Salaam kujaa maji mengi na kusababisha mafuriko. 

Na hali hiyo haikuwemo tuu kwenye mafuriko pia hali ya usafiri nayo imekuwa ni tatizo kubwa kwa wakazi wa jiji kwani kama ilivyozoeleka  ya kuwa mara baada ya mvua kunyesha hali ya usafiri wa jiji hili pia unakuwa ni tatizo kubwa kwa wakzi wake.

Mwandishi yetu aliyekuwemo kmaeneo ya katika ya jiji aliweza kushuhudia sehemu kubwa hasa maeneo ya posta mpya ikiwa imzingirwa na maji mengi na pia misururu mirefu ya magari na waenda kwa miguu na hivyo kuleta kero  kubwa kw watumiaji wa vyombo hivi ikiwa ni pamoja na waendesha magari, pikipiki na bajaj kama invyoenekana pichani ikiwa pia kuwalazimika watumiaji wa vyombo hivi kutembea masafa marefu kwa miguu.

Pichani  ni baadhi ya picha zilizopigwa maeneo ya posta mpya katikati ya jiji mara tuu baada ya mvua iliyodumu kwa takribani  nusu saa kuacha kuendelea kunyesha na kuacha hali tete kwa wakazi wa jiji hili.


Hali ya maeneo ya Posta mpya jijini Dar es Salaam leo mchana




Maji yakiwa yamefunika barabara








































































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.