Habari zilizopatikana ni kwamba timu ya Manchester United jana walikutana na maofisa wa kampuni ya NIKE kwa ajili ya kuaagalia uwezekano wa kumrudisha Christiano Ronaldo katika timu hyo yenye makazi katika uwanja wa Old Trafford.

Katika kurudi huko mchezaji huo wa zamani wa Manchester ataighairimu Manchester kitita cha takribani Paundi za Kiingereza milioni 75 na hivyo kumfanya aweze kuungana na nyota mwenzake Wayne Rooney ambaye jana kocha wa Manchester united Sir Alex Ferguson alidhibitisha katika habari na waandishi wa habari ya kwamba hauzwi.

Wawakilishi hao wa NIKE walikwenda mjini London pia kwa ajili ya mazungumzo ya kuboresha mkataba wao na timu hiyo ila madhumuni makubwa ya safari hiyo ilikuwa ni namna gani watamrudisha Cristiano Ronaldo jijini Manchester.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.