Benki ya
Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni ya kutoa elimu mashuleni ya usimamizi
na utawala wa fedha kwa vijana katika jitihada zake za kuwaelimisha wanafunzi
wa Sekondari nchi nzima umuhimu wa kuwa na utamaduni wa kuweka akiba.
Akizungumza
katika uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki hiyo, Bi Mizinga Melu alipotembelea shule ya Sekondari ya
Benjamini Mkapa ya jijini alisema kampeni ya kujifunza utamaduni wa kujiwekea
akiba ni mkakati wa benki wa kuelimisha vijana mashuleni na jamii kwa jumla
nchi nzima umuhimu wa kuweka akiba kwa ajili ya baadaye.
Alisema
Benki ya Taifa ya Biashara inafahamu kwa kina umuhimu wa kuwekeza na kuelimisha
vijana wa leo wa kitanzania jinsi ya kusimamia mapato yao na kujiwekea akiba
kwa maisha yao baadaye ili kuhakikisha
wanajifunza mbinu wakiwa bado vijana wadogo mashuleni.
Melu
alisisitiza kwamba vijana ndio nguzo pekee kwa maendeleo ya nchi ya kijamii,
kisiasa na kiuchumi kwahiyo inahitajika juhudi za makusudi za kumpatia kijana
wa leo taarifa, elimu ya fedha na ujasirimali katika mitaala ya masomo yao kwa
manufaa ya nchi nzima.
Alisema
kwamba kuna mambo ya muhimu kwenye stadi za maisha hasa katika swala la
kujiwekea akiba kwa ajili ya baadaye kwa hiyo wanafunzi watafundishwa mbinu
sahihi za kutunza fedha na mapato ili kupunguza utegemezi kwa walevi na wazazi
na jamii kwa ujumla.
Melu
alifafanua kwamba kampeni hii ya kufundisha utawala wa fedha na mapato kwa
vijana itatengeneza mazingira mazuri kwa wanafunzi, walimu, wafanyakazi wa
benki ya NBC and jamii kwa ujumla kushirikiana kwa karibu zaidi.
“Sisi
NBC tunatambua umuhimu na nafasi vijana katika kutengeneza jamii ya baadaye kwa
mantiki hiyo kwa kutambua uwepo wao tunajisikia ulazima wa kuwajengea uwezo kwa
maslahi ya kizazi kijacho,’
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Maendeelo ya Vijana na Michezo ambaye alisoma hotuba ya Waziri wa
Habari kwa niaba yake, Profesa Elisante Ole Gabriel alisema serikali itaendelea
kutilia mkazo umuhimu wa elimu kwa vijana katika kusukuma mbele gurudumu la
maendeleo ya taifa.
“Nachukua
nafasi hii kuwashukuru Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kuendesha kampeni
hii, kwani tunaamini kuwa kampeni hii itawafikia vijana wengi, watakaobadili
mwelekeo wao wa kujitegemea na hatimaye kujijengea uwezo wa kujitegemea
kiuchumi, sasa na baadaye,” alisema
Profesa Gabriel aliendelea kuishukuru benki
hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya elimu hapa nchini pamoja
na hivi karibuni kuchangia bweni huko Tabora na Maktaba ya kujisomea huko Lindi
ambayo ni moja ya changamoto kubwa sana kwa nchi na Serikali.
Serikali
kupitia mwaka wa fedha 2013 na 2014 Wizara ya Habari, Utamaduni, Maendeleo ya
Vijana na Michezo ilitenga kiasi cha Tsh 6.1 billioni kwa ajili ya kutoa mikopo
kwa vijana nchini.
Kwa
Upande wake Mkuuwa Idara ya Masoko, Mawasiliano na Mahusiano Mwinda Kiula
Mfugale alisema kupitia programu ya kujitolea kwa jamii kampeni ya kuhamasisha
elimu ya utawala wa fedha na kuweka akiba imefundisha wanafunzi 3,000 na
malengo kufikia wanafunzi 6,000 nchi nzima.
Mwisho..