August 2014


By DAMAS MAKANGALE, DAR ES SALAAM, TANZANIA 

The World Bank group, Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) has insured nearly $185 million in private sector investment into Tanzania to develop areas of priorities such as infrastructure, energy and mining.
Vice President and Chief Operating Officer, Michael Wormser.

Speaking to reporters in a news conference today in Dar es Salaam, MIGA, Vice President and Chief Operating Officer, Michael Wormser said that the aim of the grant is to stimulate economic growth and job creation in Tanzania.

“I look forward to talk with the government and the private sector to see how MIGA can help mobilize private capital to create jobs and improve infrastructure in particular in transportation, energy and agribusiness,” he said.

He said that a new MIGA guarantee would help tap the potential of Tanzania’s underdeveloped mining sector, helping the country to diversify its economy by also promoting social wellbeing of the people.

Wormser added that in fiscal, 2001, Barrick Gold Corporation of Canada received a $56.25 million MIGA guarantee for its investment in an underground gold, silver and copper mine in Tanzania.

He further said that MIGA mission is to promote Foreign Direct Investment (FDI) into developing countries to support economic growth, reduce poverty, and improve people’s lives.

“We do this by providing political risk insurance (guarantee) against certain noncommercial risks to investments in developing countries, as well as by providing dispute resolution services for guaranteed investments,” 

“We also conduct research and share knowledge as part of our mandate to support foreign direct investment into emerging markets,” he underscored.

Wormser said that they have taken on board the issue of sound environmental performance, sustainability with respect of natural resource management and social responsibility are critical to an investment’s success and its contribution to the host country’s development. 

He said that in the few months to come MIGA will inject nearly $60 million to support the agricultural sector through silver sand project to ensure that the Tanzanians are transforming agricultural sector into green revolution.

Wormer said that MIGA has developed political risk insurance products especially designed to target mining related investor concerns include the revocation of leases, tariff, regulatory and credit risks arising from breach of government contracts as well as dispute related to take off agreements and exploitations rights.

He noted that the risks associated with the mining sector are complex and require careful consideration by potential sponsors and leaders.

According to him mining sites are often in remote or political unstable parts of the world, adding to the cost and uncertainties associated with extractive industries.

He noted that civil disturbances and conflict can disrupt normal operations and social and environmental concerns are prominent and weak macroeconomic environments and inadequate legal and regulatory frameworks can invite unwarranted government intervention.

Wormer noted that the agency helps countries define and implement strategies to promote investment through technical assistance services managed by the investment climate World Bank group.

Since its inception in 1998, MIGA has issued guarantee contracts totaling $1.6 billion for projects in the mining sector. The mining portfolio currently stands $240 million, accounting for 2% of MIGA’s outstanding gross portfolio.






To apply for a Chevening Award, you will need to submit an online application through our online application system. Paper applications will not be accepted.

Applying for a Chevening Scholarship is a simple process. 

How to apply for a Chevening Award

Once you have selected the Chevening Award you wish to apply for, you will be asked a series of questions to asses whether you are eligible to apply. Read more about the Chevening eligibility criteria
If you meet the eligibility criteria you will need to create an account, and provide your name, email address and choose a password. Alternatively, you can create an account by using the LinkedIn or Facebook buttons.
There are ten sections to the application form, and you will need to complete all sections before you can submit your application. The application form guidance explains each section in more detail. You can save your application at any time, and log in to complete it later. Make sure you don’t forget to submit your application before the deadline of 15th November.
Remember: You can only submit one application each year and only your first application will be accepted. Once you have submitted your application, you cannot change your answers to the questions.

Search awards: You can search Chevening Award categories available to you, by clicking on the links below.

Ndugu wanahabari,

Sote tunaelewa kuwa kwa matakwa ya CCM, Bunge Maalum la Katiba (BMK) limeendelea kufanya vikao vyake mjini Dodoma kuanzia Agosti 5 mwaka huu, kinyume kabisa na matarajio ya Watanzania, ambao kupitia fursa mbalimbali wamepaza sauti zao wakisisitiza maridhiano na mwafaka wa kitaifa kutangulizwa mbele badala ya maslahi ya watawala.

Tukiwa viongozi wa kisiasa ambao ni sehemu ya uongozi ndani ya jamii, wenye wajibu wa kuwa na maono chanya na muhimu kwa taifa letu, tumeendelea kufuatilia kwa karibu namna mchakato wa Katiba Mpya unavyoendelea kunajisiwa kupitia vikao hivyo vya BMK linaloendelea mjini Dodoma, likitumia rasilimali za taifa, zikiwemo kodi za Watanzania wanyonge, kujadili vitu visivyotokana na wananchi.

Mtu yeyote makini ataweza kubaini kuwa kwa namna mchakato wa Katiba Mpya unavyopelekwa auunavyokwenda kwa sasa ni matokeo ya kukosekana kwa uongozi wa kisiasa kwa Chama kinachoongoza Serikali, CCM.

Kuna ombwe kubwa la uongozi wa kisiasa katika jambo hili. Ni kama vile mchakato unajiendea tu wenyewe bila mwongozo wowote kutoka kwa watu walioko madarakani ambao wananchi walitarajia wangetumia mamlaka yao ya dhamana ya uongozi ili taifa lipite salama katika wakati huu mgumu na tupate Katiba Mpya na bora.

Vipo viashiria vingi tu vinavyoweka wazi hali hiyo ya ombwe la uongozi wa kisiasa katika mchakato huu wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na kauli kinzani za viongozi wa Serikali na CCM yenyewe.
Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza kama vile kunahitajika mazungumzo zaidi na kwamba suala la muundo wa serikali lilipaswa kupigiwa kura kabla, Mwenyekiti wa BMK anaendelea kuongoza bunge kama vile mchakato ni mali binafsi ya CCM na walioko madarakani.

Wakati baadhi ya viongozi wa Serikali ya CCM wakitoa kauli za kuhitaji kuwa makini na taratibu za kuendesha mchakato huu chama chao kinatoa kauli za kuzidi kuharamisha na kutia najisi mchakato mzima. Mchakato unakwama, nchi inayumba, Watanzania wako katika sintofahamu kwa sababu tu tumekosa uongozi wa kisiasa katika jambo hili.

Kiashiria kingine cha pengo hilo la uongozi wa kisiasa ambacho kwa kweli kwetu sisi kimetusikitisha zaidi kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuendelea na ‘hamsini zake’ kama vile nchi haina tatizo lolote.

Yaani wakati nchi na wananchi wako katika sintofahamu ya hatma ya Katiba Mpya itakayoweka misingi ya wao kujitawala na kuongozwa watakavyo, makundi mbalimbali yakipaza sauti zao, mataifa mengine yakituangalia kwa makini na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wakifuatilia mchakato, Rais Kikwete anapata muda wa kutembelea ranch ya Rais Mstaafu wa Marekani George Bush!

Wakati Rais Kikwete akiendelea kutalii dunia, wenzake wako mjini Dodoma wakichukua posho kwa kazi ambayo wananchi hawajui wanaifanya kwa maslahi ya nani!

Kwa ujumla mambo yote yanayoendelea sasa katika mchakato huu ni matokeo ya ombwe hilo kama tulivyosema.

Inaonesha kuwa CCM wamelewa madaraka na viongozi wanaona dhamana ya uongozi iko juu ya wananchi hivyo hawajali umuhimu na nafasi ya mamlaka ya wananchi katika kuamua mstakabali wa taifa lao kwa ajili ya kizazi cha sasa na kuweka msingi wa vizazi vingi vijavyo.
Hivyo leo tungependa kuzungumza tena kuhusu Rasimu ya Katiba na mchakato wenyewe hapa ulipokwama;

Tunapenda kusema wazi kuwa tumeshangazwa sana na kitendo cha CCM na Serikali yake kulazimisha kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba Mpya, tena kwa mtindo ule ule wa kunajisi na kupuuza maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kama yalivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Wamefanya hivyo pasi na kujali kilio cha wananchi kinachopazwa kutoka kila kona ya nchi, ambapo Watanzania mmoja mmoja na katika makundi mbalimbali wametaka maoni yao yazingatiwe kwa kujadiliwa, kuboreshwa na kisha kupitishwa na Bunge Maalum la Katiba kabla wao hawajayapigia kura ya maoni kwa ajili ya kuipitisha au kuikataa Rasimu ya Katiba Mpya.

Wajumbe wanaotokana na CCM pamoja na makada wengine wapatao 166 wa chama hicho ambao waliteuliwa kuingia kwenye bunge hilo kusimamia maslahi ya CCM kupitia kundi la wajumbe 201, wameamua bila haya mbele ya umma si tu kupuuza rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi bali sasa wameamua kuingiza mambo yao waliyodhamiria tangu mwanzo kwa kadri ya maamuzi na maelekezo ya vikao vya chama hicho vikiongozwa na Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete.

Bila kujali wala kuguswa na miito ya Watanzania mbalimbali wanaotaka jambo hili liongozwe na maridhiano kwa ajili ya mwafaka wa kitaifa badala ya kuweka matamanio ya watawala mbele, CCM na mawakala wao katika mchakato huu wameendelea pia kufuja na kutumia vibaya fedha za wananchi kupitia Bunge Maalum la Katiba kwa kujadili na kuingiza vitu visivyokuwemo au visiyotakiwa kuwa sehemu ya rasimu hii iliyopo sasa.

Hali hiyo imefanyika kwa namna kadhaa ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria inayosimamia mchakato mzima, kubadili kanuni za uendeshaji wa BMK hasa katika taratibu za kujadili na kupitisha ibara na kubwa zaidi kuingiza masuala ya Tanganyika kwenye Rasimu ya Katiba ya Muungano.

Kimsingi masuala wanayoyajadili na kuyachomeka kinyemela kwenye Rasimu ya Pili ya Warioba, mathalan masuala ya Ardhi, Elimu, Maji, Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Serikali za Mitaa nk ni masuala yanayopaswa kuandikwa kwa kina ndani ya Katiba ya Tanganyika na siyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni vyema kukumbuka kuwa Zanzibar walijadili wenyewe mambo Yao ya Ndani na kutengeneza Katiba yao na hatuoni mantiki ya kuruhusu Wajumbe toka Zanzibar kujadili na kuamua mambo ya Tanganyika. BMK haina Sifa ya kujadili yasiyo ya Muungano.

Hivyo tofauti na wanavyotaka kujionesha katika jamii, CCM kupitia BMK wameamua kupindua kabisa rasimu nzima na kuweka maazimio ya vikao vyao kuwa ndiyo Katiba ya Tanzania. Jambo hili haliwezi kukubalika.

Kutokana na uchakachuaji huo wa Katiba Mpya unaoendelea kufanywa na CCM kupitia BMK, UKAWA tumefikia maamuzi yafuatayo;
  • Tunamtaka Rais Jakaya Kikwete asitishe shughuli za BMK mara moja lisiendelee kuvuruga na kuharibu mchakato wa Katiba Mpya na kuiweka nchi katika sintofahamu juu ya jambo hili nyeti;
  • Tunamtaka Rais Kikwete asitishe BMK ili lisiendelee kufuja fedha za Watanzania maskini wanaopigania Katiba Mpya iwapatie matumaini ya kuongozwa na kujitawala wanavyotaka.
  • Tunamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum kwenye matumizi ya fedha za BMK ambayo kuanzia Bunge la Bajeti lililopita tumebainisha wazi kuwa yana uvundo mkubwa wa ufisadi na hayana maelezo sahihi.
  • Iwapo Rais Kikwete atashindwa kutumia mamlaka yake kusitisha BMK na hivyo likaendelea kinyume cha matakwa na maslahi ya wananchi kama lilivyofanya awali na linavyofanya sasa,
  • UKAWA tutawaongoza Watanzania kupaza sauti zaidi kupinga najisi inayotiwa kwenye maoni yao, kupitia maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima.

Asanteni kwa kutusikiliza.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti CUF

Freeman Aikaeli Mbowe
Mwenyekiti CHADEMA

James Francis Mbatia
Mwenyekiti NCCR Mageuzi

Wilbrod Peter Slaa
Kny Makatibu Wakuu, UKAWA.

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2014/08/photo.jpg
Miss Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto pichani) akiwa kwenye program ya mwezi mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere  ambapo wamepata nafasi ya kwenda  kutembelea  Kiwanda cha Kilimo  kilichoanzishwa mwaka  1972  ambacho kinamilikiwa na Bw. Karl Heinz Knoop , mwenye uzoefu wa miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki pia nchini Tanzania mkoani Kilimanjaro Moshi kitakachofahamika kwa jina la Reila amabavyo pia vipo zaidi ya nchi 11 duniani na  kwa Afrika ni Tanzania pekee tumepata bahati hiyo ya kuletewa Teknlolojia anayotumia ya kutengeneza umeme wa gesi na pia kutunza mazao, hii itasaidia sana kukuza sekta ya kilimo Tanzania

Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (kulia) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea  kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.
Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (kulia) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.

NMB inashiriki maonyesho ya wakulima ya nane nane katika mikoa saba huku huduma zote za kibenki zikiwa zinafanya kazi katika mabanda yake kama kuweka na kutoa fedha, kupata taarifa za mikopo hasa ya kilimo.

NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika mikoa ifuatayo; Lindi ambako yanafanyika kitaifa, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mbeya, Arusha na Kagera.

Wakulima pia wanaotembelea mabanda ya NMB kote nchini watapata fursa ya kukutana na wataalam wa kilimo na pembejeo, vyama vya ushirika na hivyo kuwa na fursa nzuri za wao kupata taarifa sahihi na ushauri wa jinsi ya kutumia benki kunufaisha shughuli zao za kilimo.

Kwa kuwa moja ya malengo ya NMB ni kuhakikisha inasaidia ukuaji wa kilimo na kukifanya kuwa cha kibiashara, yenye malengo la kumkwamua mkulima. Hii ni fursa nzuri kwa wakulima, wafanyakazi wa serikali na wajasiriamali kuweza kufika kwenye mabanda ya NMB ili kujionea huduma ambazo benki inatoa.

Kilimo ni uti wa mgongo kutokana na ukweli kwamba karibia 80% ya watanzania wanajishughulisha na kilimo. Kwa kutambua hilo, NMB ipo karibu yao zaidi katika kipindi hiki cha Nane Nane kwa kuleta huduma za kuwanufaisha.

Kauli mbiu ya ‘Kilimo na Mifungo ni biashara’ kwa mwaka huuimeifanya NMB kushirikiana na serikali katika kufanikisha maonyesho ya nane nane katika mikoa yote saba.

Benki ya NMB inatoa huduma mbali mbali za kilimo ikiwa ni pamoja na akaunti maalumu ya Kilimo yaani ‘Kilimo Account’ ambayo inamruhusu mkulima kuweza kujipatia mikopo mbali mbali ili kuweza kuinua uchumi wa Nchi.

Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (katikati) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya

 

 


Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwajibika katika banda lao kwenye maonesho ya wakulima maarufu kama Nane nane ambayo kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya, katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Askari wakiwa wameimarisha ulinzi kwenye banda ya benki ya NMB katika maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.


Source by: www.wavuti.com


















































JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE MAALUM

RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM KUANZIA TAREHE 05 AGOSTI, 2014 HADI 31 OKTOBA, 2014


IMEANDALIWA NA:

OFISI YA KATIBU WA BUNGE MAALUM

AGOSTI, 2014
__________________


TAREHE
SHUGHULI
MUDA

05 Agosti, 2014
Kujadili na kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum
Siku 1

06 - 27 Agosti, 2014
Kamati kujadili Sura zote za Rasimu ya Katiba
Siku 15

28 Agosti - 01 Septemba, 2014
Kamati kuandaa taarifa za Sura zote za Rasimu ya Katiba
Siku 3

02 – 08 Septemba,2014
Kamati zote kuwasilisha taarifa zake ndani ya Bunge Maalum
Siku 5

09 - 29 Septemba, 2014
Majadiliano ya taarifa za Kamati ndani ya Bunge Maalum
Siku 15

30 Septemba - 06 Oktoba, 2014
Kamati ya Uandishi kuandika upya ibara za Sura zote za Rasimu ya Katiba
Siku 5

09 Oktoba, 2014
Kamati ya Uandishi kuwasilisha taarifa yake katika Bunge Maalum
Siku 1

10 – 21 Oktoba, 2014
Kupitisha ibara za Rasimu ya Katiba kwa kupiga Kura
Siku 7

22 - 28 Oktoba, 2014
Kujadili na kupitisha masharti ya mpito
Siku 5
10.
29 - 30 Oktoba, 2014
Katibu kukamilisha Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kuwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar
Siku 2
11.
31 Oktoba, 2014
Mwenyekiti wa Bunge Maalum kuwasilisha Katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar
Siku 1

NB: Siku za JUMAMOSI, JUMAPILI na SIKU KUU ni mapumziko hivyo hazijajumuishwa katika Ratiba hii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya sababu kubwa zinazokwamisha maendeleo makubwa zaidi na ya haraka zaidi ya Afrika ni uzalishaji mdogo na matumizi ya chini mno ya umeme.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali hiyo inaeleza jinsi ongezeko la uzalishaji na matumizi ya umeme linavyoweza kuharakisha maendeleo ya Afrika na kuleta manufaa ya dhahiri kwa kila familia na kwa kila Mwafrika.

Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Jumatano, Agosti 6, 2014, wakati alipozungumza kwenye
Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama, ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo.

Rais Kikwete amewaambia wakuu wa nchi hizo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa ni dhahiri kuwa bila ongezeko kubwa la uzalishaji na matumizi ya umeme Bara la Afrika halitatoka kwenye uduni.

Rais amesema kuwa kwa mujibu wa Ripoti ya Kanda ya Shirika la Umoja wa Mataifa Mazingira (UNEP) “Efficient Lighting in Sub Saharan African Countries” matumizi ya umeme katika Bara zima la Afrika ni asilimia 31 tu na hivyo kulifanya Bara la Afrika kutumia asilimia tatu tu ya umeme wote duniani.

Rais Kikwete amesema kuwa ili kuelewa udogo wa matumizi ya umeme ya Bara la Afrika ni kuangalia matumizi ya nishani hiyo kwa kila mkazi wa Bara hilo na yule wa Marekani. Amesema kuwa wakati kila raia wa Marekani anatumia kilowati 13, 246 katika Afrika wastani ni kilowati 440.

Ameongeza Rais Kikwete: “Ukiondoa Afrika Kusini, matumizi ya umeme kwa kila raia wa Afrika yanateremka na kufikia kilowati 160 tu.”

Amefafanua Rais Kikwete: “Uzalishaji wa jumla wa umeme wa Bara la Afrika ni gigawati 63 ambazo ni sawa na umeme unaozalishwa na nchi moja tu ya Ulaya – Hispania. Ukiondoa Afrika Kusini, nchi zinazobakia wa Afrika zina uwezo wa kuzalisha gigawati 28 tu, kiasi ambacho kinazalishwa na nchi moja tu ya Marekani Kusini ya Argentina.”

Rais Kikwete ambaye alikuwa anafafanua jinsi utoaji huduma ulio dhahiri unavyoweza kunufaisha wananchi na kujenga mazingira ya taasisi zisizokuwa za kiserikali kushamiri, ametaja mambo mengine ya msingi ambayo ni lazima yawepo ili wananchi waweze kunufaika ikiwemo elimu, ushamiri wa sekta binafsi, sera sahihi za kiuchumi, uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa kilimo.

Pia Rais Kikwete ametaja mambo mengine muhimu yanayoweza kusaidia kuboresha maisha ya wananchi kuwa ni uendelezaji na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na kulea na kukuza demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria.

Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa katika Marekani, anaondoka mjini Washington, D.C., leo kwenda Houston ambako atafungua na kushiriki katika mkutano wa uwekezaji katika uchumi wa Tanzania.

Mwisho!

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
07 Agosti, 2014


UAMUZI wa ushirikiano wa wanaotaka Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuamua kususia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba unatishia kusababisha kuvurugika na kuvunjika kwa  mchakato wa kuelekea Katiba mpya.
Viongozi wa wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)

Waraka huu basi ni kwa viongozi, wapenzi na mashabiki wa Ushirikiano huu ambao umekuwa ukitoa mawazo mbadala na yale ya viongozi walioko madarakani chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Kwa vile dalili zote zilizopo zinaonyesha kuwa mchakato huu umegota na kuendelea kwake kunategemea kwa kiasi kikubwa kupiga magoti kwa CCM basi nimeonelea niandike waraka huu wa wazi kwa uongozi wa UKAWA, wanachama na mashabiki.

Lengo la waraka huu wa wazi ni kutoa wito kwa UKAWA kujitoa mara moja kwenye mchakato huu kwani uwezekano wa wao kurudi na kusalimu amri mbele ya matakwa ya wenye nguvu ni sifuri.

Nimewahi kuandika huko nyuma mara baada ya wao kutoka kuwataka warudi wakapambane bungeni huko huko na baadaye warudi kwa wananchi.

Hata hivyo, naamini kama wangefanya wakati ule lingekuwa ni jambo zuri lakini sasa tukichukulia mambo yote ambayo yametokea hadi hivi sasa naamini hawawezi kurudi bungeni bila kuonekana wamegeuka na kula matapishi yao.

Uamuzi wa UKAWA kujitoa kwenye Bunge la Katiba ni wa lazima sasa hivi kwa sababu kubwa mbili; kwanza, kutaokoa mabilioni ya fedha ambayo yanaweza kuliwa tena bila huruma kwa kufanya vikao vya Bunge ambavyo havitaenda popote kwani uwezekano wa kupata Katiba mpya na kukamilisha mchakato huu kabla ya Uchaguzi Mkuu haupo.
Jambo la pili ni kuwa uamuzi huu wa kujitoa ukichukuliwa sasa utatoa nafasi mbili muhimu sana.
Nafasi ya kwanza utalazimisha CCM na uongozi wake wote na wale wanaokubaliana na misimamo ya CCM kuamua kuchukua hatua inayofaa kunusuru mchakato huu.

Ni wazi kuwa wajumbe wote wa UKAWA wakijitoa ni vigumu rasimu ya Katiba kupita kwani itakuwa vigumu kupata wingi wa wajumbe wanaotakiwa kupiga kura kupitisha vipengele na ibara za rasimu ya Katiba.

CCM italazimisha kubadilisha Sheria waliyoitunga bungeni ili kujipa uhalali wa kuendelea na mchakato huu.
Nafasi ya pili itakayotolewa ni kwa UKAWA kujiunganisha zaidi na kujipanga kushinda chaguzi zilizoko mbele – ule wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu – na hivyo kujiweka katika nafasi ya wao kuanzisha mchakato mzuri, sahihi, wa kina na halali wa kuandika Katiba mpya kuliko mchakato huu wa sasa ambao kama nilivyowahi kuonyesha nyuma ni mchakato haramu.

Hivyo, ombi langu kwa UKAWA ni kufikiria kama muungano wao ni wa kimkakati tu au ni muungano wenye lengo la kwenda zaidi ya hapo.
Kama UKAWA – na hili nimewahi kulionyesha nyuma – imeungana kwa lengo tu la kutaka Katiba mpya basi muungano au ushirikiano wao huu ni dhaifu sana na utawasumbua mbele hasa kama CCM itaamua kukubali matakwa ya UKAWA na kuwarudisha bungeni.

Chama cha Mapinduzi kinaweza kabisa kukubali kuwa kitakachojadiliwa iwe ni rasimu ya Warioba tu na maamuzi mengine na hivyo kuwafanya UKAWA wasiwe na hoja tena ya kusimamia.

Matokeo ya hili kimkakati ni kwa CCM kuhakikisha kuwa wajumbe wake kwenye Bunge la Katiba wanafuata maelekezo ya chama na kwa kutumia nguvu za kura – iwe ya wazi au ya siri,  si hoja – kuzima mapendekezo ya UKAWA.

Lakini kama ushirikiano huu ni zaidi ya suala la Katiba mpya; kwamba ni muungano ambao unataka kuleta sera na maono mbadala kwa taifa na hata kushirki uchaguzi basi suala la  kujitoa kabisa kwenye mchakato huu sasa hivi na mara moja na daima haliepukiki.

Haliepukiki kwa sababu kuendelea kwa namna yoyote ile kushiriki katika mchakato huu ni kuupa uhalali ambao sasa hivi unakosekana.
Endapo UKAWA wataamua kurudi na kushiriki wajue kabisa watakuwa chini ya huruma ya watawala.

Tumeshashuhudia kwenye hii midahalo na majadiliano yaliyofanyika siku hizi chache zilizopita na jambo moja liko wazi – tofauti baina ya pande hizi mbili ni kubwa sana kiasi kwamba njia pekee ya kuweza kuwasogeza karibu ni kutengeneza geresha ya kisiasa.

Geresha hii naamini itakuwa ni CCM na uongozi wake kukubali (compromise) bila kukubaliana. Yaani, itaonekana watu wamekubaliana lakini kumbe hawajakubaliana hasa kile wanachotakiwa kukubaliana.

Endapo UKAWA wataingia kwenye mtego huu wa kukubali bila kukubaliana (a compromise that’s not a compromise) watajikuta wanalazimika kuanza tena kubishana na watu wale wale, kuhusu mambo yale yale na wanaweza kuwa na wakati mbaya zaidi kusimamia hoja zao kuliko wakiamua kujitoa.

Wakijitoa sasa wataweza kujipanga kama nguvu ya kisiasa (political force) kukaa chini na kuzungumzia ushirikiano wa kisera na maono ya taifa na hatimaye kuweza kutengeneza ajenda moja ya kisiasa ambavyo ushirikiano huu utasimama pamoja kwenye chaguzi.

Ushirikiano wa aina hiyo utakuwa ni zaidi ya mapatano; utatakiwa uwe ni ushirikiano ambao vyama hivi vitakaa chini na kuandika makubaliano yao (memorandum of understanding) ili angalau kuwe na msingi wa kisheria wa ushirikiano huu kwani hivi sasa sidhani kama hili liko wazi zaidi.

Ni wazi kuwa endapo UKAWA utashindwa kusimama na kujipanga vizuri basi kwa mara nyingine tena Watanzania wanaotaka mabadiliko wanaweza kujikuta mioyo ikivunjika tena kwani nafasi adhimu kama hii haitatokea tena kwa miaka mingi ijayo.

Ni wakati wa wanachama na mashabiki kuanza kuweka shinikizo kwa viongozi wa kisiasa kuonyesha uthubutu zaidi ya ambao wameuonyesha ili hatimaye wao ambao wamekuwa wakidai Katiba mpya kwa miaka mingi sasa waweze kushinda uchaguzi na kuingiza Serikali ambayo kweli kabisa itakuwa tayari kuliongoza taifa kuandika Katiba mpya kutoka kwa wananchi, kwa ajili ya wananchi, na ya wananchi; ambayo itadumu kwa vizazi na vizazi!

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.