Timu Tatu zinazoaminika kuongoza kwa umwagaji wa fedha zinapomuhitaji mchezaji yeyote dunia, Barcelona, Real Madrid na PSG ya Ufaranza zimedhibitisha ya kwamba hazina mpango wa kumsajili Mchezaji hodari na kipenzi cha mashabiki wa Manchester United Wayne Rooney kwa kipindi hiki cha kufungwa kwa dirisha refu la usajili wa wachezaji barani ulaya.

Manchester United wanaweza kusikiliza ofa ya kuanzia Paundi Milioni 50 toka kwa timu yeyote ila pamoja na habari hizi si Barcelona au Real Madrid za Uhispania zilizo tayari kutoa ada hiyo kwa ajili ya kumtwaa nguli huyu wa soka barani ulaya na hata pia wale  wanaosifikia kwa kumwaga fedha nyingi katika usajili PSG pale wanapomhitaji  mchezaji yeyote timu ya PSG ya Ufaransa iliyokuwa imeonyesha nia hiyo  mwanzoni wa kufunguliwa kwa dirisha pia hawako tayari kufanya hivyo.

Hayo yameelezwa wazi kutokana na hali halisi  inavyooneka ya kwamba Sir Alex Ferguson amezidi kupoteza imani   juu ya Rooney na ikizidi kutiwa chachu pia na kuporomoka kwa kiwango cha uchezaji cha Wayne Rooney katika siku hizi za karibuni.  

Habari zimezidi kudokeza ya kwamba mawasiliano pia kati ya Ferguson na Rooney kwa kipindi hiki yamekuwa ni nadra sana tangu kurudi kwa Rooney kutoka mapunziko ya mwisho wa msimu.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.