Wayne Rooney
WAYNE ROONEY alitotelwa nje ya uwanja jana mara baada ya kupata maumivu makali ya kuchanika paja na huenda akauzwa kwa paundi millioni 50 kama ataongeza bidii katika kupandisha kiwango chake cha uchezaji.
Gazeti linaloongoza kwa udaku jijini London, The Sun limedokeza ya kwamba uvumilivu wa Manchester United juu ya gwiji huyu unaonekana kufikia kikomo  kutokana na vitendo vya mcehzaji huyu ndani na nje ya uwanja na sasa klabu inafikiria kumuuza kwa Paundi za Kiingereza millioni £50m endapo kama hawataona mabadiliko yeyote toka kwa mchezaji huyu.
Meneja mkuu wa Manchester United Mzee Alex Ferguson alithibitisha jana kwamba Rooney atakoseka ndani ya uwanja kwa kipindi cha majuma manne ambapo pia itamkosesha kuwemo ndani ya Timu ua Uingereza kwenye mechi mbili za kutafuta nafsi ya kucheza kombe la dunia na timu za mataifa ya Moldova na Ukraine.
Akiendela zaidi Sir. Alex Fersuon alitabanaisha ya kuwa baada ya kurizishwa na kiwango na ujio wa nyota mpya wa Kidachi Robin Van Persie and hamu yake kupenda kuichezea Man United kwa moyo wake, “Kama nitasikia ya kuwa mchezaji amechoka kuwa na sisi, na anataka kuwemo sehemu nyingine sitasita kumsaidia kumwonyesha mlango wa kutokea
Kiwango cha Rooney dhidi ya kipigo cha bao moja bila toka kwa Everton siku ya Jumatatu kilikuwa ni kibovu na Ferguson hakuwa na furaha juu ya kiwango chake. Lakini pia klabu inatambua kiwango cha Rooney cha sasa na tabia yake nje ya uwanja hata kabla ya kurudi kwenye mechi za kujiandaa na msimu mpya wa Ligi na majadiliano pia yameshafanyika hata kwenye ngazi ya bodi ya wakurugenzi wa klabu dhidi yake.








Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.