Watu wasiopungua 48 wameuawa huko Tana River Kenya na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kutokea mapigano ya kikabila.
Taarifa zaidi zinasema, mapigano hayo yaliyotokea kusini mashariki
mwa Kenya yamezihusisha jamii za Pomoko na Orma. Polisi ya eneo
yalipotokea mapigano imetangaza kuwa, mapigano hayo yalianza baada ya
wanachama wa jamii ya Pomoko kuwashambulia wenzao wa jamii ya Orma.
Kamishna Msaidizi wa Polisi Angelus Karuru ambaye anaongoza kikosi cha
usalama katika eneo yalipozuka mapigano amesema kwamba, juhudi za
kiusalama zinafanyika ili kumaliza mapigano hayo. Taarifa zaidi
zinasema, ngombe wasiopungua 60 pia wameteketezwa katika mapigano hayo.
Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limetangaza kuwa, watu waliouawa
katika mapigano hayo ni kati ya 30 na 50. Aidha watu 30 kati ya
waliouawa ni wanawake na watoto wadogo. Baadhi ya watu wametoweka na
hawajulikani waliko.
Source: kwetubongo
Post a Comment