Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL unasikitika kuwatangazia kuwa kuanzia
leo jioni saa 10 hakutakuwepo huduma ya usafiri wa treni ya Jiji maarufu
kama ' treni ya Mwakyembe' hadi siku Jumatatu Novermba 17, 2014 huduma
itakaporejea kama kawaida.
Ufafanuzi
wa sababu za kusitishwa huduma umeeleza kuwa kichwa kimojawapo ambacho
hutoa huduma kimepelekwa Karakana Kuu ya Morogoro kwa ajili ya ukarabati
maalum na kwamba kinatarajiwa kurejeshwa Dar es Salaam jioni ya siku ya
Jumapili. Novemba 16, 2014 baada ya kukamilika zoezi hilo la ukarabati.
Huduma zitarejea tena siku ya Jumatatu saa 12:30 asubuhi kuanzia kama kawaida kituo cha Ubungo Maziwa.
Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake!
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza!
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL
kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu.
Dar es Salaam,
Novemba 13, 2014
Post a Comment