Baadhi ya wamiliki wa Blogs nchini wakiwa katika warsha hiyo leo

  1. Mwenyekiti: Joachim Mushi
  2. Makamu Mwenyekiti: Francis Godwin
  3. Katibu: Khadija Kalili
  4. Wajumbe: Shamim Mwasha, Mdimu Henry, William Malecela, Othman Maulid 
MWANDISHI wa gazeti la Jamboleo kutoka mkoani Iringa Bw Francis Godwin ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama cha Wamiliki Mitandao ya Kijamii (Blogs) nchini Tanzania.

Godwin ambae ni mmiliki wa blog ya "MatukioDaima" na "FrancisGodwin" ameteuliwa katika nafasi hiyo kama mwakilishi wa wamiliki wote wa blogs za mikoani, huku Joachim Mushi akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Uteuzi huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City baada ya kumalizaka kwa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).
Wengine walioteuliwa ni pamoja na Katibu wa chama hicho Khadija Kalili, ambapo wajumbe ni Mdimu Henry, William Malecela, Othman Maulid na Shamim Mwasha.

Akizungumza mara baada ya uteuzi huo mwenyekiti wa chama hicho Bw Mushi alisema kuwa lengo ni kuhakikisha katiba ya chama hicho inakamilika mapema zaidi ili chama hicho kiweze kusajiliwa rasmi.

Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema kuwa mamlaka yake itasaidia kufanikisha mchakato mzima wa wamiliki wote wa blog nchini kuwa na chama chao na kuwa lengo ni kuwawezesha kufanya maamuzi yao kwa umoja na kuweza kusimamiana wenyewe.

Profesa Nkoma alisema kuwa iwapo wamiliki wa blogs nchini wataanzisha chama chao upo uwezekano mkubwa wa TCRA kuwasaidia mchakato huo na pia kuendelea kuungana na chama hicho kwa kuendelea kutoa elimu zaidi.

Mbali ya kuwataka kuanzisha chama hicho,  bado aliwataka wamiliki wa blog nchini kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa kuheshimu misingi ya maadili badala ya kutumia vyombo hivyo kuvuruga maadili.

Akielezea kuhusu uwajibikaji wa blogs nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, alitaka kuhakikisha wanatoa nafasi sawa kwa vyama na wagombea wote bila upendeleo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya habari (Maelezo) Assah Mwambene aliwataka wanahabari nchini na walimiki wa blogs kuendelea kuutumia vyema uhuru wa vyombo vya habari na kuangalia mambo ya msingi kwa jamii badala ya kugeuza mitandao hiyo kuvuruga amani ya nchi.
Wanahabari na wamiliki wa blogs nchini wakifuatilia warsha hiyo
Mkurugenzi mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma akifungua warsha hiyo leo 
Mwandishi wa BBC nchini Tanzania, Aboubakar Famau (kulia) na mmiliki wa MatukioDaima.com Bw Francis Godwin mara baada ya kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa wamiliki wa Blogs Tanzania

Mtangazaji wa TBC Shaaban Kisu wa pili kulia akifuatilia warsha ya TCRA na Wamiliki wa Blogs nchini
Baadhi ya washiriki wa warsha ya TCRA 

Source by www.wavuti.com
















































Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.