Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi. |
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema hana ugomvi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa kuwa amemlea na amemesaidia vitu vingi zikiwamo fedha, gari, kula na kulala nyumbani kwake.
Mbowe alisema CHADEMA haijamtenga Zitto bali alijitenga mwenyewe na kufafanua kuwa Chama hicho hakiwezi kujengwa na viongozi ambao ni wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyasema hayo jana katika Kata ya Kalinzi, Jimbo la Kigoma Kaskazini katika ziara zake za ‘operesheni delete CCM’ kuelimisha wananchi kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa na kuikataa Katiba iliyopendekezwa.
Mbowe alisema hayo baada ya kuruhusu maswali kutoka kwa wananchi ndipo Cheche wa Cheche alipomuuliza kwamba kwa nini Zitto hayumo katika ziara hiyo wala ya
Katibu Mkuu, Dk.Willibrod Slaa.
“Kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa nampiga vita Zitto, siwezi kumpiga vita Zitto kwa kuwa nimemlea, amekula na kulala nyumbani kwangu nami ndiye nilimshauri kugombea ubunge na kumpa fedha pamoja na gari, iweje leo nimpige vita?” alihoji Mbowe wakati akijibu swali hilo.
-----------------------
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuijua historia ya mageuzi ya Mkoa huo ili kuepuka kuwalaumu viongozi wanaosimamia vyama hivyo pindi wanapochukua maamuzi magumu.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakishabikia na kuwahukumu viongozi hao bila kuangalia chimbuko la vyama hivyo, vilikotoka na hatimaye kufikia hatua vilipo sasa hususan katika mkoa huo ambao umekuwa chimbuko la mabadiliko.
Akijibu swali lililoulizwa na mtu ambaye alijitambulisha kwa jina la Cheche wa Cheche, katika mkutano wa hadhara wa ‘Oparesheni Delete CCM’, uliofanyika kwenye kijiji cha Mnanila Manyovu mkoani hapa jana, Mbowe alisema Mkoa wa Kigoma ulizalisha viongozi wengi maarufu katika mageuzi.
Alisema utumishi ndani ya chama hicho haupimwi kutokana na mtu kutoka mkoa gani, bali hupimwa kutokana na ujasiri, uwezo wa mtu na kamwe kiongozi makini hawezi kumpiga vita mtu kwa sababu ya kabila au dini yake.
Akitoa mfano wa viongozi waliotegemewa na wanachi wa mkoa huo katika kuendeleza mageuzi, Mbowe, alisema Daniel Nsanzugwanko, Aman Kabourou na Zitto Kabwe walionyesha umahiri wao katika kuongoza vyama vya siasa enzi zao kabla ya kurubuniwa na kuvisaliti.
Akifafanua zaidi kuhusu lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake na chama anachokiongoza, hususan kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, Mbowe alisema kuwa kamwe hawezi kumzibia kwa kuwa ndiye aliyemtafuta na kumuingiza katika siasa akiwa kijana mdogo.
Labda nilazimike kutoa ufafanuzi huu ili muelewe ukweli wake. Mimi ndiye nilimwingiza Zitto katika siasa akiwa kijana madogo, nilimwita akitokea masomoni Ujerumani, kisha nikamshauri akagombee ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini, nikampa pesa na gari ambalo mpaka sasa hajalirudisha,” alifafanua.
Alisema Zitto ndiye aliyetia mchanga kitumbua chake kwa kusaliti chama kutokana na kukubali kurubuniwa na viongozi wa CCM, jambo ambalo lisingelivumiliwa ndani na nje ya chama.
Huku akishangiliwa na umati mkubwa uliofurika katika Uwanja wa Community Centre mjni Kigoma, Mbowe alisema kuwa, atahakikisha anakilinda chama hicho kwa gharama yoyote bila kumwonea mtu ili kukijengea imani kwa watanzania.
Akizungumzia usaliti wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Dk. Aman Kabourou, alisema kwamba akiwa kijana mwanzilishi wa chama hicho, alishiriki kikamilifu kumpigania Dk. Kabourou kumleta nchini na hatimaye kugombea ubunge mwaka 1993 katika uchaguzi mdogo.
“Nyinyi vijana wengi inawezekana hamjui hiki chama kilianza vipi katika mkoa huu. Mimi nilishiriki kikamilifu kumwezesha Dk. Kabourou kuwania ubunge wa Kigoma Mjini kwa kutoa nauli ya kumleta kutoka Uingereza alikokuwa akiishi, yeye na mkewe na pia nikampa pesa kumwezesha kufanya kampeni, leo hii mnanihukumu Mbowe,” aliongeza.
Alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa anampiga vita Zitto, jambo ambalo si kweli kwa kuwa amemlea, amekula na kulala nyumbani kwake kabla hajakua kiuchumi.
Jana, Mbowe alifanya ziara yake katika jimbo la Manyovu, Kigoma mjini katika uwanja wa Community Centre Mwanga, Munawila na Mahembe ambako aliendelea kuwasisitiza wananchi kuwapa dola upinzani kwa kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa.
- NIPASHE - Mbowe: Sina ugomvi na Zitto
- TanzaniaDaima - Mbowe: Siwezi kumzibia Zitto
Post a Comment