Tokea LAPTOP zimeanza kuingia sokoni zimekua sehemu ya maisha yetu
ya kila siku . Mwanzoni hazikua zinapendeza sana , Kubwa na Gharama .
Lakini siku hizi katika dunia ya ushindani mambo yamebadilika kwa sababu
kuna kampuni nyingi zinazotengeneza Laptop kwahiyo zimekua na gharama
nafuu na mtu anaweza kuchagua aina anayotaka kulingana na viwango au
uwezo wake .
Kuna kampuni nyingi
zinazotengeneza Laptop lakini kwa zinazouza sana ni hizi , DELL , ASUS ,
LENOVO , IBM , HP , SAMSUNG , APPLE , ACER ,CHILLBLAST , ALIENWARE ,
TOSHIBA ,SCHENKER , MSI , GIGABYTE ,SONY , SCAN .
Kama
unataka kununua laptop msimu huu wa sikukuu za mwaka 2014 , huu ni
muongozo unaoweza kukufaa katika kuchagua laptop , ingawa baadhi ya vitu
vinaweza kubadilika kutokana na nchi na soko kwa ujumla .
Ukienda
kwenye Maduka utakuta kuna laptop aina 3 , zile zenye Operating System
haswa windows , ambazo hazina kabisa , na ambazo zimewekwa lakini za
majaribio ukiingia kwenye mtandao unatakiwa kununua .
Bei
za laptop zinategemea moja ya mambo hayo 3 ukiacha mengine yote ,
laptop ambazo hazina kitu kabisa bei yake ni ndogo inapungua zaidi ya
dola 200 kuliko zile ambazo zimeshawekwa Programu kama ni za majaribio
au ambazo zimeshasajiliwa kabisa .
Sasa hivi
kuna Preview ya Windows 10 , unaweza kuingia dukani ukaambiwa ndio toleo
jipya wewe ukakubali kuitumia kumbe ni preview tu baada ya muda itaweza
kukusumbua , kwa sasa usitumie windows 10 , tafuta windows 7 au 8 .
Kabla
ya kuamua kununua laptop hakikisha unajua kile unachotaka kufanya na
laptop husika , kama ni kwa masuala binafsi tu madogo au ya kitaaluma (
kutegemea na taaluma ) . mfano kama unataka kununua ya kuchezea Michezo
(Games ) unatakiwa kuchagua yenye viwango na uwezo mkubwa , kama CPU ,
RAM , zaidi hapo andaa bajeti kubwa .
Kama ni kwa ajili ya
Kuandika vitu vyako tu , kutembelea tovuti mbalimbali unaweza kununua
laptop ya viwango vidogo na utatumia gharama ndogo .
CPU ndio
muendeshaji mkubwa wa Laptop yako kwa ujumla , udogo au ukubwa wa CPU
ndio utaamua kasi ya laptop yako kutokana na matumizi . Kuna Kampuni
nyingi zinazotengeneza CPU Kama Intel , AMD , Motorola na nyingine
nyingi lakini INTEL na AMD ndio zinazonunuliwa zaidi sokoni na kutumika
zaidi kwenye laptop , mwendo wake au Spidi inatakiwa iwe kuanzia 3.4 Ghz
, Core i5 or i7 M .
Uwezo na Ukubwa wa
kuhifadhi vitu wa Laptop yako ni muhimu sana , hii nayo inategemea na
aina ya shuguli unazofanya na vitu vyako , kama unavideo nyingi ,
nyaraka , picha na vitu kama hivyo unashauriwa kua na laptop yenye uwezo
na eneo kubwa la kuhifadhia vitu vyako hii inaitwa HDD – Hard Disk
Drive , inatakiwa iwe na angalau GB 250 , iwe na mfumo wa SATA .
HDD
Kubwa inaendana na RAM wengine huita Memory kubwa , hii inatakiwa
kuanzia GB 4 na kuendelea , kutegemeana pia na shuguli unazofanya ,
laptop inapofanya kazi vitu vyote huhifadhiwa kwenye hii RAM .
Kwa
watu wanaopenda michezo ya Kompyuta , kuchora , kutengeneza filamu
kutumia Kompyuta , suala la VGA , GPU au Graphic Card ni muhimu sana ,
uzuri wa Video unayoiona kwenye kioo unategemea sana hii kadi , Kuna
kampuni nyingi zinazotegeneza hizi kadi kwa ukubwa na viwango tofauti .
Huwezi
kutumia laptop bila ulinzi dhidi ya mashambulio kutoka nje labda kwenye
internet au vitu unavyochomeka kama flash , au unavyoingiza kama CD/DVD
, hapo ndio tunakuja kwenye suala zima la ANTIVIRUS .Mpaka sasa hivi
kampuni nyingi zimeshatoa matoleo mapya ya ANTIVIRUS Zao , kama
Kaspersky 2015 , AVIRA , AVG 2015 , AVAST 9.0 , NORTON , SYMANTEC ,
MCAFEE na Nyingine nyingi .
Ufanyaji mzuri wa
ANTIVIRUS unategemea sana ukubwa na uwezo wa LAPTOP yako na zaidi ni
jinsi unavyoiboresha kwa kuingiza kwenye internet kwa ajili ya kufanya
updates ( boresha )
Kwa wale wanaopenda
kusafiri au sehemu zenye shida ya umeme suala la betri ni muhimu sana
kwenye laptop mpaka mwaka mmoja uliopita betri zilikua zinadumu kwa saa 4
lakini sasa hivi kuna mpaka saa 8 kutegemea na aina ya Laptop na Ukubwa
wake , betri inayokaa muda mrefu itaweza kukusaidia kwa muda mrefu
zaidi .
Screen au Kioo ni muhimu kwa watumiaji
wa laptop hili nalo hutegemea shuguli unazofanya , kwa mtumiaji wa
kawaida anaweza kuamua kutumia kioo cha kawaida ila kwa mchoraji wa
ramani yeye atahitaji laptop yenye kioo kikubwa ili aweze kuona kazi
zake na kuchora vizuri zaidi .
Kwenye laptop
zote za sasa hivi zinavitu ambavyo ni lazima kama NIC (Sehemu ya
Kuchomeka waya wa Mawasiliano ) , WIFI ( Wireless ) , USB , Speaker na
Mic , Cardreader , webcam , FingerPrint .
Warranty
ni kitu muhimu sana kwenye bidhaa yoyote unayonunua sio kwenye Laptop
tu , hii ndio inaeleza jinsi utakavyorudisha laptop dukani kama
imeharibika ndani ya muda Fulani na kitu gani kikiharibika ndio urudishe
.
Kwenye Laptop na Vifaa vingi warranty inakua
ndani ya miaka 3 lakini kwa nchi nyingi za afrika , Tanzania ikiwemo ni
mwaka mmoja .
Mwisho kabisa ni kuongea na
muuzaji wa bidhaa kuhusu shuguli unayoenda kufanya na kifaa chako kabla
ya kununua , ataweza kukushauri zaidi na hata kukuonyesha bidhaa
zilizopo ili uweze kuchagua ili usije kupata taabu baada ya kununua
Post a Comment