Dk Cuthbert Maendaenda akiwatwanga lekcha wahariri mbalimbali mjini Morogoro |
ULAJI wa supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Dk Cuthbert Maendaenda wakati akitoa mada yake katika semina ya wahariri iliyofanyika mkoani Morogoro iliyojadili nafasi ya wanaume katika kuleta mabadiliko katika jamii juu ya afya ya uzazi na ujinsia.
Dk Maendaenda ambaye alikuwa akijibu maswali pia kuhusiana na dhana hiyo iliyozoeleka kuhusu nguvu ya supu ya pweza, alisema ipo haja ya wanaume kuangalia sababu za kudorora kwa uwezo wao na kufanya marekebisho badala ya kudhani kwamba kuna dawa kutoka katika vyakula hivyo.
Miji mingi nchini kwa sasa nyakati za jioni kuna supu ya pweza na mauzo ya karanga mbichi ambao wauzaji wamekuwa wakinadi kama msaada wa kurejesha heshima katika ndoa.
Alisema ufanyaji mapenzi unaathirika na vitu vingi na jamii lazima kuangalia ukweli huo ili kuwa na watu wanaojiamini katika mapenzi na wale ambao wanamatatizio kupata ushaudi wa kidaktari.
Mwezeshaji huyo kutoka Taasisi ya sweden inayohusu haki za afya ya uzazi na ujinsia (RFSU) tawi la Tanzania ambalo linaendesha mradi wa TMEP wenye lengo la kuwaamsha wanaume kuwa chachu ya mabadiliko na hivyo kuwa na uelewa mpana kuhusu haki za ujinsia.
Alisema mwanaume mwenye afya zake hutoa kiasi cha manii cha CC 3-5 kinachotarajiwa kuwa na mbegu milioni 300-500 katika mshindo mmoja.
Alisema alisema vyakula vyote vinavyoliwa havina uhusiano na uimara au ujazo wa manii kwani, wanachokula watu ni vyakula vya kuongeza nguvu (wanga) na wala si protini inayotakiwa kusuka na mbegu.
Alisema kuna sababu nyingi zinazokwamisha furaha katika burudani ya kufanya mapenzi hukua kisema kwamba asilimia 60 za hali inatokana na tatizo la kisaikolojia, hamu iliyopitiliza ya kufanya mapenzi na kuonesha urijali mahusiano ya mwanaume na huyo anayetaka kufanya naye mapenzi na hasa hofu inayotawala kama atamudu kazi hiyo au la.
Aidha alisema sababu zingine ni za kitabibu zaidi, kama mgonjwa ya shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, kisukari, tatizo la homoni, mgongo na pia magonjw aya kuambukiza.
pamoja na kuzungumzia uwezo wa kufanya mapenzi, Daktari huyo pia alisema kwamba ukosefu wa mimba unahitaji kuchunguzwa kwa makini na wala si kumbebeasha lawama mwanamke.
Alisema watu wengi wanaofanyakazi katika maeneo yenye joto linalozidi kama waendesha magari makubwa ya safari, waendeshapikipiki,wapishi hujikuta na tatizo la uzazi kwa kuwa kitabia mfumo wa uzazi wa mwanaume unahitaji joto la chini kuliko la mwili na kupigwa kila mara na jiotoi la juu husababisha athari katika m fumo wa utengenezaji wa mbegu, idadi na uwezo wa kusafiri.
Pia alisema shauri la mtu kuwa na uume mdogo au mkubwa halina uhusiano na uwezo wa kuzaa wala kufurahisha kimapenzi na tatizo hilo linabaki kisaikolojia zaidi.
Wahariri hao wametakiwa kuwa makini katika kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali kwa kuwaambia ukweli na sio kung'ang'ania dhana dhaifu ambazo mwishoni mwa siku zinasababisha mtafaruku katika jamii, kuongeza magonjwa na kujiamini.
Post a Comment