BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema kuwa
inautambua mchango wa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wadogo katika
kukuza uchumi wa taifa na hivyo itaendelea kuwa karibu nao na kuwapa mafunzo ya
mara kwa mara.
Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu kongamano la
siku mbili la Wajasiriamali Vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam hivi
karibuni, Meneja Ukuzaji wa Biashara Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa na Kati,
Jonathan Bitababaje alisema wajasiriamali wengi waliofanikiwa ni wale
walioanzia ngazi za chini. Business devv man sme banking dept
“Kumbukumbu na nyaraka za kibenki zinaonyesha kuwa
wale walioanza kwa mikopo midogo na kuendelea kufanya biashara na NBC ndio
wamekuja kufanikiwa sana na ndio maana benki hii itaendelea kuwapa mafunzo na
ushauri unaofaa wajasiriamali vijana,” alisema.
Alisema kupitia makongamano, wajasiriamali hupata
nafasi ya kufahamu ni biashara gani inatakiwa kwa wakati, bidhaa gani inatakiwa
na hata washindani wake ni akina nani.
Akizungumza wakati wa semina hiyo iliyofanyika
katika Ukumbi wa Don Bosco kwa niaba ya Waziri wa Vijana, Habari, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mkandala, Naibu Mkurugenzi wa Vijana wizarani hapo, James
Kijugusi aliwashauri wajasiriamali hao kuwa na tabia ya kuziwekea bima biashara
zao.
“Biashara lazima ziwe na kinga. Kwa sasa sema uchumi wan chi na hata wa dunia hauwezi
kukua iwapo wajasiriamali wakijitoa katika biashara hasa katika enzi hizi zaunaTes
Tfanyabiasharsiku ya kwanza biashara wajasiriamali .
Alisema kuwa kwa sasa Serikali ipo
katika mazungumzo na mashirika ya hifadhi za jamii na bima kwa ajili ya kuweka
utaratibu wa kuwasaidia wajasiriamali iwapo watapatwa na majanga ya aina hiyo.
Kongamano
hio liliwajumuisha washiriki 250 kutoka kada mbalimbali za wajasiriamali vijana
wa jijini Dar es Salaam.
Post a Comment