Arsenal 0 Swansea City 2
Mchezaji hatari wa Swansea Mhispania Michu jana aliltea hatari kubwa katika uwanja wa Emirates kwa kufunga magoli mawili ya haraka haraka katika dakika za jioni na kuwalaza timu ya Arsenal 2-0 katika uwanja wake wa nyumbani ikiwa ni kipigo cha kwanza tokea ligi hii kwa Arsenal kupoteza mchezo katika uwanja wake wa nyumbani.
|
Wachezaji wa Arsenal wahispania Santi Cazorla na Mikel Arteta wakifunika sura zao kwa huzuni |
|
Muuaji wa Arsenal katika mchezo wa jana Michu |
|
Michu akiipatia Swansea goli la kuongoza |
|
Michu akishangilia kuwatungua Arsenal |
Manchester City 1 Everton 1
Timua ya matajiri ya Manchester City jana ilinganganiwa shati na timu ya Everton kwa kutoa droo ya goli 1-1 iliyofanya wapinzani wake Manchester United kuendelea kushikilia uongozi wa ligi hiyo kwa pointi tatu kamili toka moja. Walikuwa ni Marouane Fellaini aliyeanza kuipatia Everton goli la kuongoza katika dakika ya 33 kabla ya Carlos Tevez kuisawazishia City kwa mkwaju wa penati katika dakika 43 mara baada ya Fellain kumgusa Edin Dzeko na refarii kuamuru ipigwe penati ambayo Carlos Tevez hakufanya ajizi kuingiza mpira kimiani.
|
Kipa Joe Hart akijitahidi bila mafanikio kuzuia mpira wa kichwa wa Fellaini uliozaa bao la kuongoza kwa upande wa Everton |
|
Fellaini akishangilia na wachezaji wenzake |
|
Tevez akiiaptia Man City goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati |
|
Kipa wa Everton Tim Howard akiruka bila mafanikio kuokoa mchomo wa Carlos Tevez ambaye anaonekana kwa taabu pichani |
QPR 1 Aston Villa 1
Boss mwenye historia ya kuokoa timu zinazotaka kushuka daraja, Harry Redknapp jana aliiongoza timua yake ya Queen PArk Rangers kujipatia pint yake ya pili na kinachosubiriwa sasa na mashabiki wa timu hiyio ni je katika mchezo unaofuata dhidi yao na Wigan December 8 atafanikiwa kupata ushindi wa kwanza tokea ligi hiyo kuanza katika jumla ya michezo kumi na mitano waliocheza mpaka sasa.
Ikiwa Harry atafanikiwa kunyakua pointi zote tatu katika mchezo unaokuja na wigan itaifanya timu hiyo kuwa na pointi tisa na kuwa sambamba na wanaoshikilia nafasi ya pili toka mkiani timu ya Reading ambayo jana ililimwa mabao 4-3 na mabingwa wa kihistoria Manchester United.
Kwa kutoka droo na Aston Villa jana QPR ilifanikiwa kuifikia rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Swidon katika msimu wa mwaka 1993-1994 kwa kucheza michezo kumi na mitano pasipo ushindi na kufanya washuke daraja, sasa swali kubwa linalobakia ni jee Harry atafanikiwa kutokushuka daraja kwa rekodi hii au atajutia uamuzi wake wa kuikataa kazi ya kuiongoza timu ya Ursi kuelekea fainali za kombe la Dunia mnamo mwaka 2014 mjini Rio De Janeiro.
|
MackieJamie akishangilia kupata goli la kusawazisha. |
|
Harry Redknapp akiwasalimia mashabiki watimu yake mpya kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Loftus Road |
Fulham 0 Tottenham Hotspur 3
Jermain Defoe jana aliongoza maauji dhidi ya Fulham akitokea benchi katika mchezo wao dhidi ya timu ya Fulham katika uwanja wake wa nyumbani wa Craffen Cottages kwa kuiufungia timu yake ya Tottenham Hotspur mabao mawili kati ya matatu katika ushindi wake wa 3-0 dhidi ya Fulham.
Nyota wa mchezo wa jana baina ya Fulham na Totteham Jermain Defoe.
|
Wachezaji wa Totenham wakimpongeza mchezaji mwenzao raia wa Brazil Sandro kwa kuipatia timu hiyo bao la kuongoza |
|
Jermain Defoe akiandikia Spurs goli la pili |
|
Wachezaji wa Fulham wakiongozwa na Berbotv wakitoka uwanjani kwa huzuni mara baada ya kutandikwa mabao 3-0 na Spurs |
Liverpool 1 Southampton 0
Post a Comment