SHIRIKA
lisilo la kiserikali la Mpango wa chakula duniani (WFP) limetoa msaada wa pampu
210 za maji zenye thamani ya zaidi ya shilingi 94 milioni kwa shule za msingi
na vikundi mbalimbali mkoani Singida.
Pampu
hizo ni kwa ajili ya kilimo cha umwangiliaji bustani.
Hayo
yamesemwa juzi na Mkuu wa Ofisi ndogo ya WFP Dodoma Nima Sitta,wakati
akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matenki 12 ya kuvunia maji ya mvua
yaliyojengwa kwenye shule sita za wilaya ya Singida na wilaya ya Ikungi.Hafla
hiyo ilifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Igaruri wilaya ya Singida.
Alisema
lengo kuu la msaada huo wa pampu za maji,ni kila shule za msingi na vikundi vya
vijana,kuanzisha kilimo cha umwangiliaji maji bustani.
Meneja wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani Kanda ya Kati Nima Sitta |
Nima
alisema kila shule ya msingi yenye chanzo cha maji,itapatiwa pampu si chini ya
mbili,wakati vikundi vya vijana waliomaliza elimu ya msingi na wale waliomaliza
kidato cha nne,watapatiwa si chini ya pampu tatu.
"Kwa
upande wa vijana,kila kikundi kinatakiwa kumiliki ekari sisizopungua tatu na
wawe wamejipanga vizuri,shule za msingi zimepewa sharti la kuwa na shariti la
kumiliki ekari mbili.Hivi sasa tunaendelea kuzizungukia shule ili zile zenye
sifa,ziweze kukabidhiwa pampu mapema iwezekanavyo"alifafanua Nima.
Katika
hatua nyingine,Nima alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika lisilo la
kiserikali la SEMA la mjini Singida, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa matenki ya
kuvunia maji na inayofanana na thamani ya fedha zilizotumika .
"Kwa
kweli SEMA kazi yao ni nzuri mno,wametekeleza kwa kiwango cha juu yale yote
ambayo yapo kwenye mkataba na kufanya mazuri zaidi baadhi ya shughuli ambazo
hazipo kwenye mkataba.Nisema tu kwamba kazi ya SEMA,inapaswa kuigwa na wajenzi
wengine kwa maendeleo ya wananchi",alisema.
MWISHO.
Post a Comment