MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imekanusha kuhusika na uingizaji wa kontena la samaki wabovu kwa kuwa si juukmu la Mamlaka hiyo kukagua mizigo bandarini.
Msemaj wa Mamlaka hiyo Bibi Janeth Ruzangi ambaye ni Kaimu Meneja  Mawasiliano wamesema TPA haihusiki kwa njia yoyote ile na kontena hilo kinyme na ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vy ahabari ikikuhisha kontena hilo na TPA.

Akifaafanua, alisema jukumu la TPA ni kupakua na kupakia mizigo melini ambapo baada ya kupaukliwa huhifadhiwa katika 

sehemu maalumu mpaka atakapokuja mwenye mzigo kuuchukua baada ya kuwa amekamilisha taratibu zote.

“Kwa mizigo kama hii ya chakula chenye kukaa kwenye barafu au baridi, kawaida huwa inapakiwa kwenye makontena maalumu ya baridi (refrigerated containters) na mara inapokuwa imeshushwa bandarini huwekwa kwenye sehemu ya umeme kwa kiwango cha baridi (reefer points) ambacho mwenye meli ataagiza kiwekwe kulingana na vile ilivyokuwa ndani ya meli kabla ya kushushwa na Maafisa wa Bandari kukagua kila baada ya saa mbili ili kuhakikisha hakuna mabadiliko ya kiwango cha baridi na endapo patatokea hitilafu ya umeme, majenerata yataendelea kutoa umeme,” alieleza Ruzangi.

Katika kuhakikisha mizigo inatoka kwa kufuata utaratibu, Ruganza alisema utartibu unaotumika katika kupokea mizigo baada ya Mamlaka kushusha mizigo, taasisi zingine husika inafanya kazi yake ikiwa ni pamoja na kuhakiki nyaraka na kutoza ushuru stahili kazi ambayo hufanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na kwa mizigo ya chakula ni lazima Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wawepo ili kuhakikisha chakula kilichoingia nchini kinafaa kwa matumizi ya binadamu.

Baada ya mwenye mizigo kupata nyaraka zote husika ndipo TPA itaruhusu mzigo huo kutoka kupitia katika milango yake iliyopo bandarini na si vinginevyo, alisisitiza Ruzangi.

Mwisho……….


Imetolewa na
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
Idaraya Mawasiliano
S.L.P.  9184
DAR ES SALAAM
Simu: 0713 33 43 98
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.